• UVCCM TAIFA

  SAUTI YA VIJANA,SAUTI YA UMMA.CCM MPYA,TANZANIA MPYA.

 • UVCCM TAIFA

  MWAKA MMOJA WA SERIKALI YA AWAMU YA TANO.

 • This is default featured slide 3 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

 • This is default featured slide 4 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

 • This is default featured slide 5 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

Jumatatu, 30 Septemba 2013

NAIBU KATIBU MKUU UVCCM BARA COM MFAUME KIZIGO AWAFUNDA UVCCM UKONGA
KIZIGO ALIWATAKA VIJANA HAO KUENDELEA KUKIIMARISHA CHAMA NA JUMUIYA ZAKE KWA KUWA HAKUNA MBADALA WA CCM TANZANIA,
ALIFAFANUA MAJUKUMU YAO NA NINI WAJIBU WAKO KATIKA KAZI ZAO.SEMINA HIYO ILIYOJUMUISHA VIONGOZI WA KATA ZOTE 8 ZA UKONGA ILIKUWA YENYE MAFANIKIO NA KUTOA HARI MPYA YA KIUTENDAJI KATIKA JIMBO HILO.

Share:

Jumapili, 29 Septemba 2013

MKT WA UVCCM TAIFA;SADIFA JUMA KHAMIS AWAVURUGA WAPINZANI TEMEKE DSM


katika ziara hiyo bwana Sadifa ameweza kuwapa kadi jumla ya vijan 650na ahadi zake zote alizotoa amezitekeleza kwa kutoa jezi,mipira na pesa tasilimu. suala ambalo lilionekana kuwapa presha vyama vya CUF NA CHADEMA kiasi cha kuchimba barabara kuzuia msafara wa mwenyekiti huyo ulipokuwa unapita, lakini kupitia vijana imara wa CCM waliweza kuhakikisha amani inatawala na kila kitu kinaenda sawa kama kilivyopangwaShare:

Opportunity Education kutoa tablets kwa wanafunzi nchini

salma 74f14
Taasisi ya fursa ya Elimu (Opportunity Education) ya nchini Marekani imeazimia kuanzisha mradi wa laptop ndogo (tablets computer) kuanzia mwezi Januari mwaka 2014 nchini ambazo zitatumika kufundishia ili walimu waweze kufundisha haraka na kwa ufanisi zaidi pia wanafunzi watapata nafasi ya kujifunza zaidi. (HM)

Hayo yamesemwa jana na Joe Ricketts ambaye ni mwanzilishi na mtendaji mkuu wa taasisi hiyo wakati wa hafla ya kuchangia uugwaji mkono wa utoaji elimu barani Afrika iliyoandaliwa na taasisi ya Malaika ya nchini humo na kufanyika katika chuo Kikuu cha Nebraska kilichopo mjini Lincoln .
Ricketts alisema mradi huo kwa mara ya kwanza utaanzia nchini Tanzania ambapo wanafunzi zaidi ya 1000 kutoka shule 10 tofauti watapewa laptop ndogo kwa ajili ya kusomea na baada ya kipindi cha mwaka mmoja watafanya mtihani ili kuangalia tofauti iliyopo kwa wale waliokuwa wakitumia na wasiotumia.
Baada ya majaribio hayo kama kutakuwa na mafanikio basi mradi huo utasambazwa katika shule nyingine nchini Tanzania ili kila mwanafunzi aweze kupata nafasi ya kusoma kwa kutumia laptop hizo na hii itakuwa ni nafasi kwao ya kuweza kujitunza zaidi.
"Kwa mara ya kwanza nilipokuwa nchini Tanzania nilipita Serengeti na kukuta mtu anajitahidi kutengeneza nyumba ambayo ni ngumu kuitengeneza hii inamaana kuwa mwalimu mmoja alikuwa anafundisha wanafunzi zaidi ya miamoja niliamua kuanzisha mahusiano na shule hiyo ambayo niliwapelekea vifaa mbalimbali vya kufundishia".
"Lengo la kuanzishwa kwa Taasisi hii ni kutoa msaada wa kielimu ikiwa na nia ya kufanya upatikanaji wa elimu bora kwa wanafunzi kutoka nchi zinazoendelea ili wale wanaotoka katika familia maskini waweze kusoma na kupata ajira pale watakapokuwa wamemaliza masomo yao na hivyo kujikwamua na hali ngumu ya maisha", alisema Ricketts.
Alimalizia kwa kusema kuwa program zao za kufundishia wanafunzi zimeandaliwa kwa lugha ya kiingreza lakini hivi sasa wameanza kuandaa program hizo kwa njia ya Kiswahili jambo ambalo litazifanya shule ambazo zinafundisha kwa lugha hiyo nazo kunufaika na Taasisi hiyo.
Kwa upande wake Mke wa Rais Mama Salma Kikwete aliishukuru taasisi hiyo kwa kusaidia kuboresha elimu nchini na kuiomba kuangalia uwezekano wa kuzifikia shule, walimu na wanafunzi waliopo vijijini ambao nao wanahitaji kupata njenzo nzuri za kufundishia na material mazuri ya kusoma kama ilivyo kwa wanafunzi wa mjini.
Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeeo (WAMA) alisema kuwa kupitia taasisi hiyo ameweza kuwasaidia watoto wa kike ambao ni yatima na wanaotoka katika mazingira hatarishi ambao hawakupata nafasi ya kupata elimu kuwapatia ufadhili wa masomo na hivyo kuendelea na masomo yao.
Pia ameweza kuinua uchumi wa wanawake jambo ambalo limewafanya waweze kuimarisha hali zao za maisha kwa kuwapatia elimu ya ujasiriamali na kuwaongezea mitaji ya vikundi vyao vya maendeleo.
Mama Kikwete alisema, "Nakupongeza Bwana Ricketts kwa kazi unayoifanya ya kuzisaidia shule zaidi ya 400 nchini Tanzania msaada unaoutoa wa vifaa vya kufundishia unawafanya walimu waweze kufundisha masomo yao vizuri naamini tutajenga mahusiano mazuri kati ya Taasisi yako na WAMA ili kuhakikisha kuwa program hii inafanikiwa na kutimiza malengo yake".
Taasisi hiyo ilianzishwa mwaka 2005 na kusajiliwa nchini mwaka 2006 walianza kufanya kazi na shule moja ya msingi na hadi kufikia sasa shule 434 zikiwemo za Sekondari 33 zimenufaika kwa kupata vitabu, DVD na zana za kufundishia.
Kwa upande wa shule za sekondari wanatoa mwongozo wa mwalimu ambao unamuongoza kirahisi jinsi ya kuwafundisha wanafunzi , laptop ambazo zinamasomo yaliyorekodiwa ambayo ni ya sayansi, hesabu, kiingereza na maarifa ya jamii ,projecta na Televisheni ambazo zinasaidia kuonyesha masomo na vitabu na video inawasaidia wanafunzi kujifunza somo la kiingereza kwa njia ya kusikiliza na kusoma.
Mama Kikwete alipata nafasi ya kutembelea makao makuu ya Taasisi hiyo yaliyopo katika mji wa Omaha na kujionea nyenzo mbalimbali za kufundishia vikiwemo vitabu na DVD zikiwa zimefungwa kwa ajili ya kupelekwa katika nchi mbalimbali zinazoendelea za bara la Afrika na Asia ikiwemo Tanzania. Chanzo: Anna Nkinda – Maelezo, Lincoln
Share:

Alhamisi, 26 Septemba 2013

KENYA NI NDUGU ZETU,KENYA NI JIRANI ZETU


Share:

Wanasiasa wametakiwa kuacha kauli zinazohatarisha usalama wa nchi


pix_2_85b85.jpg
Waziri wa Manedeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Sophia Simba akitoa maelezo juu ya kauli zenye kuashiria uvunjifu wa sheria na tabia za vurugu katika jamii ambazo zilitolewa na baadhi ya wanasiasa hivi karibuni katika vyombo vya habari hapa nchini.(P.T)
pix_4_e5b06.jpg
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Manedeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Sophia Simba wakati akitoa maelezo juu ya kauli zenye kuashiria uvunjifu wa sheria na tabia za vurugu katika jamii ambazo zilitolewa na baadhi ya wanasiasa hivi karibuni katika vyombo vya habari hapa nchini.

Na Eleuteri Mangi-MAELEZO-Dar es Salaam.
SERIKALI imeshtushwa na baadhi ya ujumbe wa maneno uliopelekwa kwa wananchi na baadhi ya vyama vya siasa hapa nchini ambao unaweza kuleta kuhatarisha amani na usalama wa Tanzania.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Sophia Simba leo jijini Dar es salaam wakati wa mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake.
Waziri Simba amesema kuwa kauli zilizotolewa hivi karibuni na baadhi ya vyama vya siasa vilivyofanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya Jangwani zimeishtua Serikali na zinaweza kuleta madhara makubwa kwa jamii hususani wanawake, wazee, walemavu na watoto.
Waziri Simba amesema kauli zilizotolewa na viongozi hao ni pamoja na "Vijana msikubali wakati wa kufanya mazoezi umefika" kauli hii inahitaji tafakari na kuhoji kwa makini inawahamasisha vijana kutii, jambo ambalo linaweza kuwafanya walete vurugu..
Amesema kuwa kauli hiyo na nyingine zilizotolewa na viongozi hao wa juu wa vyama hivyo zinazowachochea wananchi kutotii na ni ishara ya uwepo wa njama mbaya za kuwashawishi wananchi ili siku hiyo wajichukulie sheria mikononi, kinyume cha katiba, sheria na haki za binadamu.
Aidha, Waziri Simba alisema jamii inahitaji kutafakari juu ya kauli hizo na mustakabali wa Tanzania.
Amesema kuwa jamii ya Watanzania inatakiwa kutambua kuwa amani na usalama ndio mtaji namba moja wa maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kidemokrasia. Ustawi wa jamii ya Watanzania unahitaji amani, utulivu na usalama.
Mwisho.
Share:

Jumatano, 25 Septemba 2013

MKT WA UVCCM TAIFA SADIFA JUMA KHAMIS AFUNIKA IRINGA,CHADEMA WAPATA HOFU NA ZIHARA YAKE

katika ziara yake hiyo juzi aliambatana na baadhi ya wajumbe wa kamati ya utekelezaji na maofisa wa makao makuu akiwamo Seki Kasuga ambae pia ni mjumbe wa baraza kuu Taifa akiwakilisha mkoa wa Iringa.

pamoja na kuyatikisa matawi ya chadema Iringa hali iliyomfanya mbunge wa CHADEMA kupiga simu mara kwa mara kwa baadhi ya vijana Iringa akiwaomba vijana wake wasishiriki ziara hiyo jambo ambalo halikufanikiwa.

Mwenyekiti Sadifa alifungua kambi ya vijana Iringa na kutembelea chuo cha Ihemi,alipokea bendera mpakani mwa wilaya ya  Iringa vijijini na Mufindi,alikutana na vijana katika mikutano ya ndani na nje.

huu ni muendelezo wa mashambulizi yanayofanywa na CCM na jumuiya zake kila kona ya nchi kufuta uongo na uzushi uliosambazwa na vyama vya upinzani hasa chadema
Share:
 • APONGEZA WANANCHI WA KATA YA NATTA KWA KUSHIRIKIANA
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Wazee wa kata ya Isenya wilaya ya Serengeti waliokuja kumpokea.
 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza mwalimu wa masomo ya sayansi Ndugu Silvester Joseph , Katibu Mkuu alitembelea shule ya Natta Secondary na kushuhudia jinsi masomo ya sayansi yanavyopewa kipaumbele.
 Mwanafunzi wa Kidato cha Nne Peter Semion wa shule ya sekondari ya Natta iliyopo kata ya Natta wilaya ya Serengeti akimuelekeza namna ya kutengeneza sabuni Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipotembelea shule hiyo ya Natta iliyopo wilaya ya Serengeti.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na vijana wajasiriliamali wa kuendesha boda boda na ukulima wa mboga mboga mara baada ya kuzindua kikundi hicho ambapo aliwasihi lazima wapate elimu ya biashara wajue namna ya kuweka na kukopa na kulipa madeni kwa wakati.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoka ndani ya ukumbi wa mkutano wa MUGUMU CCM ambapo alikutana na vijana wajasiriamali wa wilaya hiyo. 
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Natta mara baada ya kumaliza kikao na balozi wa shina namba 11 Tawi la Natta Majengo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoa shukrani kwa wazee wa Natta baada ya kumpa heshima ya kuwa Mzee wa Natta.

Share:

Serikali kuanzisha benki ya vijana;

Serikali kuanzisha benki ya vijana;

baloz_c42c8.jpg
SERIKALI ina mpango wa kuanzisha benki ya vijana amabyo itakuwa ikiwapatia mikopo nafuu ili kuwawezesha kujiajiri wenyewe ikiwa ni hatua ya kuongeza uzalishaji na kukuza uchumi wa nchi.
Kauli hiyo imetolewa leo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi wakati wa uzinduzi wa chapisho la mgawanyo wa idadi ya watu na jinsi kwenye sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere ,jijini Dares Salaam.(P.T)
Makamu huyo wa Rais alisema hayo kufutia chapisho hilo kuonesha kwamba kundi la vijana wenye umri wa kuanzia miaka 15 hadi miaka 35 kuwa ni watu milioni 15.6 sawa na asiliamia 34.7 ya watu wote nchini.
" Idadi hii ya vijana ikitumiwa vizuri itaongeza uzalishaji na hatimaye kukuza uchumi wa nchi na kupunguza umasikini ," alisema Balozi Seif.
Aliongeza kuwa Serikali na watu wengine wataendelea kuifanya Sera ya Maendeleo ya Vijana ya mwaka 2007, ikiwemo kuhamasisha vijana kujiunga na vikundi vya uzalishaji mali ni mojawapo ya mikkati ya kuendeleza vijana.
" Kwa kuzingatia rasilimali zilizopo Serikali ina dhamira ya Kuimarisha viwanda na Kilimo Kwanza kama njia nyingine za kuwazesha vijana kupata ajira na kuongeza kipato. Vijana wa tabia ya kungojea ajira kazi za maofisi ambazo haziko nyingi, bali wajiunge na kushiriki katika shughuli za uzalishaji mali ili waweze kujaipatia kipato kwa ajili ya kuendesha maisha yao," alisisitiza.
Aidha aliongeza kwamba kupitia chapisho hilo, limeonesha kuwa kundi jingine la wazee wenye umri wa miaka 60 au zaidi amabo ni milioni 2.5 sawa na asilimia 5.6 ya watu wwote nchini. Hivyo kulingana na Sera ya Wazee kundi hilo linahitaji huduma maalum kama vile, matibabu, malazi na huduma nyingine muhimu.
"Serikali na wadau wengine wataendelea kuwapatia wazee hawa huduma muhimu kulingana na hali ya uchumi wan chi," alisema.
Balozi Seif alizita Wizara ,Idara na Taasisi zote za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuboresha sera zilizopo na kutumia takwimu hizi katika kupanga mipango ya maendeleo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS) Dk. Albina Chuwa alisema chapisho hilo linaonesha kuwa umri unaoanzia miaka 0 hadi 4 kuashiria kuwa kiwango cha uzazi bado ni kikubwa.
Alifafanua kuwa kwa kumujibu wa Utafiti wa Mama na Mtoto wa mwaka 2010 kiwango cha uzazi ni wastani wa watoto 5.4 kwa kila mama mwenye umri wa miaka 15hadi 49, hivyo uzazi wa mpango utaendelea kusisitizwa.
Naye Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia (UNFPA)Mariam Khan alisema chapisho hilo litasaidia kujua iddai ya watu wanaojiandikisha shule, wastaafu, kupanga uzazi wa mpango na mipango mingineyo.
Mwisho.
Share:

MAADHIMISHO A MIKA 50 YA SEKONDARI YAWERUWERU

MAADHIMISHO A MIKA 50 YA SEKONDARI YAWERUWERU

Bashir Nkoromo at WATU NA MATUKIO, MAKALA - 3 days ago
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda , Mkewe Tunu (wapili kulia),Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka (kulia), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dr. Mary Nagu (kulia) kwa Waziri Mkuu na Mkuuwa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama wakitazama vitu mbalimbali vya mazoezi katika maabara ya Baiolojia katika maadhimisho ya Shule ya Sekondari ya Wasicha ya Weruweru yaliyofanyika shuleni hapo. Septemba 21, 1013 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua Bwalo la Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Weruweru ya Moshi Vijijini ikiwa na sehemu ya maadhimisho ya mi... more »
Share:

Jumanne, 17 Septemba 2013

KINANA AKOMAA NA MAWAZIRI

 • Sasa kuongozana na Mawaziri mguu kwa mguu
 • Asema kazi yake ya kuijenga chama inahitaji watu makini kama mtu hawezi kasi yake awapishe.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikaribishwa kwa kahawa katika kijiji cha  Budalabujiga wilaya ya Itilima mkoani Simiyu ambapo Katibu Mkuu alifanya ziara ya siku moja wilayani hapo.
  Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akikaribishwa kwa kahawa katika kijiji cha  Budalabujiga wilaya ya Itilima mkoani Simiyu, Katibu wa Itikadi na Uenezi ameongozana na Katibu Mkuu wa CCM katika ziara ya mkoa wa Simiyu.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akipata maelezo wakati akikagua Bwalo la chakula la shule ya sekondari ya kata ya Kanadi, wilayani Itilima mkoa wa Simiyu.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya kata ya Kanadi baada ya kutembelea bwalo na bweni la shule hiyo ambapo aliwasihi wanafunzi kusoma kwa bidii na kuahidi kuwapatia sola.
 Katibu Mkuu wa CCM akiwa amembeba mtoto Dhahabu katika kituo cha afya cha Nangale wilaya ya Itimila mkoani Simiyu.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye mavazi yake ya uchifu baada ya kusimikwa Uchifu na kutambulika kama Chifu Machibola katika kijiji cha Migato wilaya ya Itilima mkoa wa Simiyu, Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya mkoa wa Simiyu ambapo moja ya lengo la ziara yake ni kukagua na kuimarisha uhai wa chama na kusimamia ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi ya mwaka 2010.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akinywa maji kwa kutumia kipeyu katika kijiji cha Migato wilaya ya Itilima mkoa wa Simiyu.
 Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya ujenzi wa ofisi za halmashauri ya wilaya mpya ya Itilima kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri Dk. Leornard Masale
 Katibu Mkuu ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupiga lipu kwenye ujenzi wa ofisi za Halmashauri za wilaya ya Itilima mkoani Simiyu.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda mti kwenye uwanja wa ofisi za halmashauri ya wilaya ya Itilima mkoani Simiyu.
 'SIASA CHINI YA MTI' Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe wa halmashauri ya CCM wilaya ya Itilima kama sehemu ya kujenga na kukiimarisha chama.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Itilima katika viwanja vya Gangabilili na kuwaeleza wananchi wa eneo hilo kuwa mipango ya kuijenga wilaya hiyo inaendelea na CCM itasaidia sana katika kuleta mabadiliko ya kiuchumi hasa kwa wakulima wa zao la pamba na wafugaji.
 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa wilaya ya Itilima katika viwanja vya Gangabilili na kuwaambia wananchi hao muda wa viongozi kukwepa kutatua kero umekwisha na kuwataka viongozi kuwajibika moja kwa moja na kuahidi kuwa atakuja mkono kwa mkono na Waziri wa Nishati na Madini pamoja na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi kutatua mgogoro mkubwa wa wafugaji na hifadhi pamoja na wakulima.
Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahma Kinana akipokea kadi kutoka vyama mbali mbali ambao wemerudi CCM zaidi ya watu 120 wamerudisha kadai katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Gangabilili willaya ya Itilima mkoani Simiyu.
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Gadget

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu