Unordered List


KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AKAGUA MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI KAHAMA

 

1Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kufyatua matofali pamoja na wananchi kwa ajili ya ujenzi wa tanki la maji katika kata ya Kagongwa Wilayani Kahama wakati alipoanza rasmi ziara yake ya siku nne katika mkoa wa shinyanga leo na kushiriki shughuli mbalimbali za maendeleo na za kukiimarisha chama katika mkoa huo, Katika picha wanaoshuhudia kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa halmashauri kuu ya CCM (NEC) Itikadi, Siasa na Uenezi na katikati ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Ndugu Khamis Mngeja.PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-KAHAMA 2Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kufyatua matofali kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa halmashauri kuu ya CCM (NEC) Itikadi, Siasa na Uenezi 3Nape Nnauye Katibu wa halmashauri kuu ya CCM (NEC) Itikadi, Siasa na Uenezi naye akishiriki kufyatua matofali kwa ajili ya ujenzi wa tanki hilo la maji katika kata ya Kagongwa 4Hili niyo tanki linalojengwa katika kata ya Kagogwa wilayani Kahama 05Wananchi wa mjini Kahama wakiwa katika mkutano wa hadhara mjini humo. 5Nape Nnauye Katibu wa halmashauri kuu ya CCM (NEC) Itikadi, Siasa na Uenezi akisoma ujumbe katika mabango yaliyoandikwa na wana CCM kuelezea kero zao Nape amepokea kero ya wanaCCM hao na kuahidi kulishughulikia mara moja. 6Umati uliojitokeza katika mkutano wa hadhara mjini Kahama. 7Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara mjini Kahama. 8 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Ndugu Khamis Mngeja akiwahutubia wananchi katika mkutano huo. 9Nape Nnauye Katibu wa halmashauri kuu ya CCM (NEC) Itikadi, Siasa na Uenezi akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Kahama leo. 12Kikundi cha ngoma kikitumbuiza katika kata ya Kagongwa wilayani Kahama 13Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikbidhi kadi kwa mwanachama mpya wa CCM Ndeke Mdaki katika kata ya Isaka Wilayani Kahama. 17Ndugu Ezekiel Maige mbunge wa Msalala akiwahutubia wananchi katika Kata ya Isaka Wilayani Kahama. 19Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kuashiria uzinduzi wa awamu ya kwanza ya ujenzi wa jengo la Kituo cha afya katika kata ya Mwendakulima kijiji cha Mwendakulima iliyojengwa na kampuni ya Kuchimba madini ya mgodi wa Buzwagi wilayani Kahama , kulia ni Mwakilishi wa Mkuu wa mgodi wa Buzwagi Bw. Richard Otendo wa pili kutoka kulia. 20Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozwa na mwakilishi wa mkuu wa mgodi wa Buzwagi Richard Otendo wakati alipotembelea jengo la kituo cha afya cha Mwendakulima lililojengwa na mgodi huo. 21Hili ndilo jengo lenyewe. 22Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananc hi katika kata ya Mwendakulima mara baada ya kutembelea ujenzi wa jengo la kituo cha afya cha kata hiyo kulia ni Nape Nnauye Katibu wa halmashauri kuu ya CCM (NEC) Itikadi, Siasa na Uenezi na katikati ni Diwani wa Kata hiyo kutoka TLP Bw. Ntabi Majabi. 23Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda mti katika kituo cha afya cha Mwendakulima. 24Nape Nnauye Katibu wa halmashauri kuu ya CCM (NEC) Itikadi, Siasa na Uenezi naye akishiriki kupanda mti katika kituo cha afya cha Mwendakulima. 25Wana CCM wakiwa katika mkutano wa Ndani mjini Kahama. 27Kikundi cha Sarakasi kikionyesha uwezo wao katika sarakasi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Sinjita mjini Kahama.

Chapisha Maoni

0 Maoni