Unordered List


Wanasiasa wametakiwa kuacha kauli zinazohatarisha usalama wa nchi


pix_2_85b85.jpg
Waziri wa Manedeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Sophia Simba akitoa maelezo juu ya kauli zenye kuashiria uvunjifu wa sheria na tabia za vurugu katika jamii ambazo zilitolewa na baadhi ya wanasiasa hivi karibuni katika vyombo vya habari hapa nchini.(P.T)
pix_4_e5b06.jpg
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Waziri wa Manedeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Mhe. Sophia Simba wakati akitoa maelezo juu ya kauli zenye kuashiria uvunjifu wa sheria na tabia za vurugu katika jamii ambazo zilitolewa na baadhi ya wanasiasa hivi karibuni katika vyombo vya habari hapa nchini.

Na Eleuteri Mangi-MAELEZO-Dar es Salaam.
SERIKALI imeshtushwa na baadhi ya ujumbe wa maneno uliopelekwa kwa wananchi na baadhi ya vyama vya siasa hapa nchini ambao unaweza kuleta kuhatarisha amani na usalama wa Tanzania.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Sophia Simba leo jijini Dar es salaam wakati wa mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake.
Waziri Simba amesema kuwa kauli zilizotolewa hivi karibuni na baadhi ya vyama vya siasa vilivyofanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya Jangwani zimeishtua Serikali na zinaweza kuleta madhara makubwa kwa jamii hususani wanawake, wazee, walemavu na watoto.
Waziri Simba amesema kauli zilizotolewa na viongozi hao ni pamoja na "Vijana msikubali wakati wa kufanya mazoezi umefika" kauli hii inahitaji tafakari na kuhoji kwa makini inawahamasisha vijana kutii, jambo ambalo linaweza kuwafanya walete vurugu..
Amesema kuwa kauli hiyo na nyingine zilizotolewa na viongozi hao wa juu wa vyama hivyo zinazowachochea wananchi kutotii na ni ishara ya uwepo wa njama mbaya za kuwashawishi wananchi ili siku hiyo wajichukulie sheria mikononi, kinyume cha katiba, sheria na haki za binadamu.
Aidha, Waziri Simba alisema jamii inahitaji kutafakari juu ya kauli hizo na mustakabali wa Tanzania.
Amesema kuwa jamii ya Watanzania inatakiwa kutambua kuwa amani na usalama ndio mtaji namba moja wa maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kidemokrasia. Ustawi wa jamii ya Watanzania unahitaji amani, utulivu na usalama.
Mwisho.

Chapisha Maoni

0 Maoni