Ijumaa, 18 Oktoba 2013

RAIS KIKWETE MKOA WA NJOMBE

jk_njombe_c4f24.jpg
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewasili mjini Njombe jana jioni, Alhamisi, Oktoba 17, 2013, kuanza ziara ya wiki moja kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Njombe.
Miongoni mwa shughuli kubwa ambazo Rais Kikwete atazifanya katika ziara hiyo, ya kwake ya kwanza tokea Njombe kutangaza kuwa Mkoa, ni kuuzindua rasmi Mkoa huo.
Katika siku yake ya kwanza leo, Ijumaa, Oktoba 18, 2013, mbali na kuzindua Mkoa wa Njombe pia atazindua Kiwanda cha Chai katika eneo la Ikanga na kuzungumza na wananchi.
Katika ziara hiyo ambako Rais Kikwete atatembelea wilaya zote za mkoa huo ambazo ni Njombe, Wanging'ombe, Ludewa na Makete, pia atazindua Chuo cha Veta cha Mkoa.
Aidha, Rais atatembelea na kupata taarifa kuhusu maendeleo ya mradi wa chuma wa Liganga.(P.T)
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu