Mkurugenzi
wa Ubunifu,Uendelezaji na Ufuatiliaji wa GODTEC Bwana Aloyce Maganga
akitoa mada kuhusu namna mfumo wa utajirishaji uanvyo weza kutekelezwa
na wadau wa maendeleo
Baadhi ya washiriki wa semina kuhusu namna ya utekelezaji wa mfumo wa utajirishaji wakifuatilia kwa makini mada iliyokuwa inafundishwa na mmoja wa watoa mada katika (hayupo pichani) jana jijini Dar es Salaam.(hd)
Mwenyekiti
Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika
Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA) na
Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchini Rwanda, Sheikh Mussa Fazil Harerimana
(katikati) akizungumza na wajumbe wa RECSA (hawapo pichani) katika
mkutano wao unaofanyika katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi ambaye
leo anatarajiwa kukabidhiwa uenyekiti RECSA ambapo anatarajiwa kuiongoza
kwa kipindi cha miaka miwili. Kulia ni Katibu Mtendaji wa baraza hilo,
Theoneste Mutsindashyaka. Mkutano huo unafanyika katika Ukumbi wa
Mikutano wa Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam leo.
Wajumbe
wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika
Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA)
wakiwa katika chumba cha mkutano wakijadili masuala mbalimbali ya jinsi
ya Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu katika
nchi wanachama ambazo ni Burundi, Congo, Djibout, Ethiopia, Eritrea,
Kenya, Rwanda, Sudan, Uganda na Tanzania. Mkutano huo unafanyika katika
Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam ambapo
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (meza kuu-kushoto)
anatarajiwa kukabidhiwa uenyekiti wa RECSA kutoka kwa Mwenyekiti
anayemaliza muda wake leo, Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchini Rwanda,
Sheikh Mussa Fazil Harerimana (meza kuu-katikati).
Wajumbe
wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Maziwa Makuu na Pembe ya Afrika katika
Mapambano ya Kuzuia na Kudhibiti Uzagaaji wa Silaha Haramu (RECSA)
wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mkutano wa unaofanyika
katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam kufunguliwa. Wapili
kushoto waliokaa ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel
Nchimbi ambaye leo anatarajiwa kukabidhiwa uenyekiti wa RECSA kutoka kwa
Mwenyekiti anayemaliza muda wake, Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchini
Rwanda, Sheikh Mussa Fazil Harerimana (wakatikati). Picha na Felix
Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. (hd)
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bw. Clement
Mshana(kushoto) akieleza kwa waandishi wa habari(hawapo Pichani) kuhusu
mkutano Mkuu wa mwaka wa Vyombo vya Utangazaji vya nchi Jumuiya ya
Maendeleo Kusini mwa Afrika(SADC) unaotarajiwa kufunguliwa rasmi tarehe
21 october 2013 Jijini Arusha, ambapo mgeni rasmi atakuwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete.Kulia ni
Mratibu wa Kanda wa Shirika hilo Bw. Joe Rugarabamu.
Picha na Hassan Silayo-MAELEZO (hd)
Picha na Hassan Silayo-MAELEZO (hd)
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na Balozi wa Tanzania, nchini Addis Ababa, Ethiopia, Naimi
Aziz, aliyefika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Okt 3,
2013 kwa ajili ya mazungumzo.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na Balozi wa Oman nchini Tanzania, Yahya Moosa Bakari,
aliyefika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Okt 3, 2013 kwa
ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini (hd)
Afisa
Mawasiliano Mwandamizi toka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF) Bw.
Luhende Singu(kushoto) akieleza kwa waandishi wa habari(hawapo Pichani)
kuhuasu m-pango wa huduma za matibabu kwa mama wajawazito kw a Mikoa ya
Mbeya na Tanga, wakati wa Mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya
Habari(MAELEZO) Leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa habari Idara ya
Habari(MAELEZO) Bw. Frank Mvungi (hd)
Afisa
Habari Mwandamizi toka Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia Bi.
Prisca Ulomi(kushoto) akieleza kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)
kuhusu Uanzishwaji wa Tume ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano,
wakati wa Mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) leo
Jijini Dar Es salaam.Kulia ni Afisa Habari Idara 6ya Habari(MAELEZO)
Hassan Silayo.
Picha na Eliphace Marwa-MAELEZO (hd)
Picha na Eliphace Marwa-MAELEZO (hd)
Mradi wa
ukarabati wa uwanja wa michezo wa namfua uliopo Singida mjini umechelewa
kuanza kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kitendo cha Chama Cha Mapinduzi
Mkoa wa Singida kuchelewa kutoa baraka zake juu ya ukarabati huo,
CHANZO: Zainul Mzige (hd)
0 Maoni