• UVCCM TAIFA

  SAUTI YA VIJANA,SAUTI YA UMMA.CCM MPYA,TANZANIA MPYA.

 • UVCCM TAIFA

  MWAKA MMOJA WA SERIKALI YA AWAMU YA TANO.

 • This is default featured slide 3 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

 • This is default featured slide 4 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

 • This is default featured slide 5 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

Jumamosi, 30 Novemba 2013

NAPE AMPA USHAURI WAZIRI WA KILIMO

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akihutubia wakazi wa Vwawa wilayani Mbozi.Nape ampa ushauri wa bure Chiza
 • Amtaka aandae majibu kwa Kamati Kuu sio kumshambulia magazetini
 •  Ahoji busara anayoidai itumike ni ipi?
 •   Asisitiza kutetea wakulima ni msimamo wa Chama
 •   Amkumbusha CCM ni chama cha wakulima
 •   Ahoji busara ya kuachia ushirika kuwadhulumu wakulima.
 •   Ahoji busara ya kulazimisha wakulima kutumia mbolea ya Minjingu inayoharibu mazao yao.
Katibu wa NEC itikadi na uenezi amemtaka
 Waziri wa kilimo, Chakula na Ushirika kuacha kumshambulia kwenye magazeti badala yake atumie muda huu kuandaa majibu ya kuwasilisha Kamati Kuu kwa hoja zilizoibuliwa na wakulima nchini.

Nape akihutubia mamia ya wananchi wa mji wa Vwawa wilayani Mbozi mkoani Mbeya alionyesha kukerwa na tabia ya hivi karibuni ya Waziri huyo kumshambulia Nape kwenye magazeti kwa maneno ya kejeli badala ya kujibu malalamiko ya wakulima.
 " Katibu Mkuu tumezunguka wilaya nyingi sana nchini hakuna mahali hakuna malalamiko ya wakulima ambao ni 80% ya watanzania wote. Sasa tumemtaka waziri aje kwenye kamati kuu kueleza anatatuaje changamoto hizi, yeye amekazana kila kukicha kunishambulia kwenye magazeti. Nataka kumpa ushauri wa bure mheshimiwa sana waziri, anachofanya hanishambulii mimi anawashambulia wakulima kwasababu siongei yangu naongea malalamiko
 ya wakulima" alisisitiza Nape

 "Nimemvumilia sana lakini sasa nimechoka, kila kukicha anatumia maneno ya kejeli na vijembe, kwanini hajifunzi busara ya Naibu wake Adam Malima? aliposikia wito wetu akasema yuko tayari kuja kujieleza kwenye Kamati Kuu kwakuwa chama ndiyo mwajiri wake hivyo atazingatia maamuzi ya chama, yeye waziri kila kukicha Nape Nape Nape, kumshambulia Nape hakuondoi kero za wakulima"! Alisema Nape
 "Nimesikia leo anasema sina busara!!busara ipi anayohoji? Mie ninayewatetea wakulima wanaolalamika kulazimishwa kutumia mbolea ya Minjingu inayounguza mazao yao na yeye anayeleta mbolea hiyo na kulazimisha wakulima watumie nani anatumia busara hapa? Yeye anayepuuza malalamiko ya wakulima kuumizwa na baadhi ya maafisa ushirika na mimi ninayetaka hatua zichukuliwe dhidi ya maafisa wake nani anatumia busara??"
 " mimi ninayemkumbusha kutembelea mkoa alioutangaza kuwa ghala la taifa la chakula ambao hajautembelea kwa miaka sasa licha ya kuwa waziri wa chakula na yeye ambaye hajatembelea nani anatumia busara?"

 " mimi ninayemshauri asikilize kilio cha wakulima wa tumbaku,pamba na korosho badala ya kusikia kilio hicho miaka nenda miaka rudi na
 yeye nani anatumia busara?"

Katika ziara hiyo ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye ameongozana na  Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye imekuwa na mafanikio makubwa  na imeongeza sana imani kwa wananchi wenye mapenzi mema na nchi hii.

Ziara hii imekuwa ya aina yake kwani Katibu Mkuu amepata fursa ya kusikia matatizo ya wananchi kuanzia wakulima ambao ndio asilimia 80%,walimu ambao ni zaidi ya asilimia 60% ya watumishi wa serikali,na kundi kubwa la vijana ambalo pamoja na kuwepo kwa taratibu za kufanya shughuli zao kwa kujiajiri bado wamekutana na vikwazo visivyo vya kawaida.

Uamuzi wa kuwaita Mawaziri kwenye kamati kuu ya chama ili watoe majibu kwa nini matatizo ya wananchi hasa wakulima hayashughulikiwi .

Wakulima wamelalamika sana kuhusu dhuluma  zinazofanywa na vyama vya ushirika na upatikanaji wa pembejeo kuwa wa tabu na cha ajabu Waziri wa Kilimo na watumishi wake wameziba masikio hata kutembelea wakulima kutaka kujua matatizo yao hawataki.
Share:

NAMPA AMPA USHAURI WAZIRI WA KILIMO

Ijumaa, 29 Novemba 2013

KINANA AITEKA TUNDUMA

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Tunduma katika viwanja vya vya shule ya Msingi Mwaka ambapo alizungumzia mambo mbali mbali ukiwemo urasimu uliokuwepo mpakani kati ya Tanzania na Zambia unaosababisha msongamano wa malori na kushauri uweke utaratibu wa kufanya kazi masaa 24 huku kukiwa na zamu za wafanyakazi kuingia kazini kwa muda utakaopangwa,Katibu Mkuu pia aligusia utaratibu wa kulipa kodi kwa wafanyabiashara wadogo uangaliwe upya ili wafanya biashara wadogo wapunguziwe kodi,pia alisema kwa kuwa Serikali haina uwezio wa kuajiri watu wote basi itengeneze mazingira rahisi kwa vijana kujiajiri.
 Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akihutubia wakazi wa kata ya Tunduma kwenye viwanja vya shule ya msingi Mwaka na kushauri wakina mama kujiunga kwenye vikundi ili waweze kupata mikopo kirahisi na pia elimu ya ujasiriamali kwa wanawake bado inahitajika kwa kiasi kikubwa na pia kusisitiza hata kiwango cha wanafunzi wa kike wanaosoma elimu ya sekondari ni ndogo na kusisitiza kila mzazi anatakiwa kutambua kuwa elimu kwa mtoto wa kike ni kitu muhimu sana.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Tunduma na kuwaambia wananchi hao wasihadaike na maneno mengi ya upinzani kuhusu Katiba Mpya, kwani Katiba hiyo haipigi kura wanaopiga kura ni wao wananchi.

 Wanachama na Wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi wakicheza muziki na Dk.Asha-Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa kwenye viwanja vya shule ya Msingi ambapo mkutano mkubwa ulifanyika.
Wanachama na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi wakiwa wamembeba juu juu Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kwenye viwanja vya shule ya msingi Mwaka ambapo mkutano mkubwa ulifanyika na kuhudhuriwa na maelfu ya watu wa mji wa Tunduma.
Share:

Jumatano, 27 Novemba 2013

KINANA: URASIMU UNAUMIZA WANANCHI

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Masoko ,kijiji cha Lupando wilaya ya Rungwe ,Katibu Mkuu waliwaambia wananchi hao kuwa urasimu na umangi meza wa watendaji wa serikali ndio unachangia kwa kiasi kikubwa kurudisha maendeleo yao nyuma na kusema kamwe CCM haitokubali hali hiyo iendelee na kusisitiza CCM itahakikisha wananchi wanapata haki zao za msingi kwanza.
 Mwakilishi wa Wananchi wa Kijiji cha Lupando Ndugu Wema Mwaipopo akiomba sana kwa niaba ya wananchi wake watatuliwe suala la maji,umeme na barabara kwani hizo ndio zilikuwa ahadi kubwa za Mbunge na Rais.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya Masoko kijiji cha Lupando na kuwaambia wananchi kuwa wapinzani ni sawa na Jogoo hata aamke saa ngapi hawezi fungua mlango,na kuwasisitiza wananchi wa kijiji hicho ni CCM pekee inayoweza kuwazungumzia na kero zao zikatatuliwa.
 Asumwisi Asagwile Mwatebela ,Mlezi wa Vijana wa Chadema wilaya ya Rungwe akirudisha kadi yake kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na kujiunga rasmi na CCM.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Kiwira Rungwe na wakati wa ufunguzi wa vikundi viwili vya wajasiriamali ambapo aliwaambia vijana maendeleo yanaletwa kwa kufanya kazi kwa kujituma na waondoe mawazo kuwa Katiba mpya ndio itakuwa mwarobaini wa matatizo yao.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia maabara ya shule ya Sekondari ya Ikuti ikiwa moja ya sehemu ya ahadi ya serikali ya kujenga maabara katika kila shule ya Sekondari ya Kata.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa Nyumba za walimu wa shule ya Sekondari Ikuti wilayani Rungwe.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahmani Kinana akiongozana na Mkuu wa Shule ya Ikuti Ndugu Emmanuel Ngasa pamoja na viongozi wengine wa chama na serikali baada ya kukagua jengo la hosteli la shule ya sekondari ya Ikuti.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wakazi wa shina namba 2,Butonga Tawi la Ikuti kwa Balozi James Mbasi, na kusisitiza viongozi wote wa CCM waige mfano wa Mabalozi kwani wanafanya kazi kwa kujitolea katika kukiimarisha na kukijenga chama.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahama Kinana akikata utepe kama ishara ya kuwasha umeme katika kituo cha Afya cha Ikuti wilayani Rungwe.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na viongozi wa wilaya ya Rungwe pamoja na wananchi kuelekea kwenye uwanja wa mkutano Ikuti.
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya Ndugu Richard Kasesela akipiga ngoma ya Kitongo kabla ya kuanza kwa mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Ikuti ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Mbunge wa Viti Maalum Wananwake mkoa wa Mbeya Dk.maru Mwanjelwa akicheza ngoma  kabala ya kuanza kwa mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Ikuti ambapo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na viongozi wa kitaifa aliofutana nao Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro na Katiibu wa NEC Itikadi na Uenezi walihutubia.
 Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya Dk.Mary Mwanjelwa akihutubia wakazi wa kata ya Ikuti na kuwaambia wanawake waandae vikundi vyao kwani Benki ya wanawake karibia itafunguliwa hivyo fursa za kupata mikopo zitaongezeka na kusaidia kufanya biashara kwa ufanisi na kuleta maendeleo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Ikuti wilayani Rungwe mkoa wa Mbeya na kusema serikali ipunguze matumizi yasiyo na lazima na badala yake nguvu nyingi iletwe kwa wananchi katika kuwaletea maendeleo.
 Wakazi wa Ikuti wakiwa juu ya mti wakisikiliza kwa makini hotuba za viongozi wao ambazo nyingi zilijibiwa vizuri hasa suala la umeme ambalo wananchi wanaweza kulipa kidogo kidogo.
Dk.Mary mwanjelwa akizungumza na akina Mama wauza ndizi wa kijiji cha Iponjola kata ya Rufingo wilaya ya Rungwe na kuwataka waanzishe vikundi kwani benki ya wanawake ipo karibuni kufunguliwa katika mkoa wa Mbeya hivyo itawasaidia kupata mikopo kwa riba nafuu.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alisimama kuwasalimu wakina mama hao kisha kuutambulisha uongozi wote aliokuwa nao kwenye msafara.

Jumanne, 26 Novemba 2013

KINANA ASEMA KILA MTENDAJI ATAMBUE WAJIBU WAKE

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa nyumba za Walimu wa Shule ya Sekondari ya Mwakaleli.
 Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akikata ubao akiwa pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakikata mbao kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya maabara na madarasa ya shule ya Sekondari ya Mwakaleli.
 Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akiongea na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Mwakaleli na kuwataka wanafunzi waongeze bidii kwenye masomo kwani elimu haina mwisho.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimu wanafunzi wa  shule ya sekondari ya Mwakaleli baada ya kumaliza kushiriki shughuli za kimaendeleo ya ujenzi wa madarasa ,maabara na nyumbza za walimu.
 Mbunge wa Jimbo la Rungwe Magharibi Profesa David Mwakyusa akiwasalimu wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mwakaleli na kuwataka wajitahidikusona na kuepukana na vitendo vitakavyo waharibia maisha yao.
 Wanafunzi wa Kidato cha Sita wa shule ya Sekondari ya Mwakaleli wakiwa kwenye picha ya pamoja na Katibu wa NEC Siasa na Mahusiano ya Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro na Mbunge wa Viti maalum wanawake mkoa wa Mbeya Dk.Mary Mwanjelwa.
 Mzee Issa Simion akitoa salaam kwa niaba ya wazee wa Kijiji cha Katende na pia kushukuru kwa Serikali na Chama Cha mapinduzi na pia kuelezea kero zinazohusu wakazi wa kata ya Katende.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kijiji cha Katende ambapo alihimiza sana kuwa makini na vyama vinavyojita vya siasa  kwani sasa vimeanza kupoteza muelekeo.
Mbunge wa Wanawake Mkoa wa Mbeya  Dk.Mary Mwanjelwa akiwasalimia wakazi Katende
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye picha ya pamoja na wazee wa kijiji ambao leo walimpa heshima ya kuwa Mzee wa Katende na kumvisha mgolole kama heshima ya mtu mzima.
 Katibu wa NEC Siasa na Mahusiano ya Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akiwa ameketi kwenye mkeka unaojulikana kama Kalili aliopewa zawadi na wakina mama wa Katende.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Katende na kuwaahidi CCM inatekeleza ilani yake ya uchaguzi na kusema ahadi zilizoahidiwa zitatimizwa.
Katibu Mkuu wa CCM aliwaambia wananchi hao kuwa lazima tuhoji serikali  pesa za maendeleo kwa nini haziji kwa wakati.
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Gadget

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu