Alhamisi, 7 Novemba 2013

Hotuba ya Mh, Rais Jakaya Kikwete kwa Bunge leo Tarehe 7 /November/2013

 Mh.Rais aliingia kwa maandamano na Mh. Spika wa Bunge
 Mh, Spika alimkaribisha Raisi ili kuanza Kulihutubia Bunge.
Alizanza kwa kuzungumzia kuwa watu wengi wamesema mengi sana kuwa Leo hii anakuja kuzungumza maswala ya, Migogoro mbali mbali lakini Kilichomleta Bungeni ni kuzungumza maswala ya EAC kwani hapapendezi hata kidogo.
Lakini alizungumzia Operesheni Tokomeza Majangili kuwa imesitishwa kwa muda na itaendelea kwani sasaivi unnatengenezwa mpango mzuri wakufanya kazi hiyo na pia kuwawajibisha wale wote walokiuka utaratibu na kufanya mambo ya ajabu ktk Oparesheni hiyo.
 kisha akasisitizia kufanya kazi kwa uadilifu, Uaminifu na kwa moyo wa dhati.  nk,,,,
Alianza kwa kutaja mambo yanayofanya EAC ifanyike na waliyajadili.

 Kuijenga Reli ya kisasa Mombasa, Kigali, Bunjumbula, Sudani
 Mafuta . Kenya , Uganda Sudani kusini.
 KUJENGA KIWANDA CHA MAFUTA UGANDA.

 KUHARAKISHA SHIRIKISHO LA AFRICA MASHARIKI KUARAKISHA VISA YA PAMOJA EAC
 UTARATIBU WA UTAMBULISHO WA KUSAFIRIA.
USAMBAZAJI WAUMEME


Yako manne hayahusiki.
1.Uzalishaji na usambazaji wa Umeme. kutafuta sehemu moja yakutunza umeme afu tuutumie. jukumu limeachiwa nchi wanacha jukumu la kuutekeleza.
2. Ujenzi wa kiwanda cha mafuta Uganda, M
3. Bomba la mafuta.
4.Ujenzi wa Reli ya Kisasa, Kigali, Bunjumbula mpaka Sudani Kusini. ( esten african railway plan, aest africa road network, Usafiri wamaji, Lake Victoria network program,

Lazima nikiri hili ni tatizo,
 Tulikaa tarehe April 28 2013, arusha, June 24 na 25 kikao cha kimya kimya. miezi miwili baadaye wakatugeuka inashangaza sana.

Haya
1.Kitambulisho cha Taifa kama hati ya Kusafiria..  Tuliwaruhusu waanze wale walokuwa navyo tayali lakini kwetu waje na Passport.

2.Mkutano mkuu 28 April wa Kamati ya jumuiya ya mashariki tulikubaliana Kila mwananchi mwanachama itasimamia Maswala yao binafsi ya kibiashara,Lakini tulikubaliana Kila bidhaa zinazovuka kwenda nchi tofauti zitakaguliwa ktk mawakala wa Forodha wa nchi husika

Paia tulikubalia kuundwa kwa Task force kwa baraza la mawaziri waunde, na watoe taarifa na utekelezaji uanze, Cha kushangaza wenzetu wanaanza moja kwa moja wakati Task force haijaleta riport kitu ambacho si sawa.
Inashangza ...!! Wenzetu wamekosa imani na jumuiya, wanachuki na tz, hawatupendi? hawatuamini au laa?
lakini nawahakikishia tuko ktk Jumuiya na hatutotoka hata kidogo, kwani sisi ni wanachama wavumilivu, watiifu na wavumilivu, 

3. Jambo la tatu si hatuelewi ila tunasikia eti kuwa.
Wao wametangulia tu na sisi tukiwa tayali tutajiunga nao.
sasa tunajiuliza nani ambae hayuko tayali?
hamjatushirikisha na hamjatualika alafu mseme eti hatuko tayali kwani, Mimi kama Rais sijapata mwaliko hata mmoja, naskia wakisema eti tanzania haina Moyo na Haina mshawasha, Tanzania inawachelewesha kufikisha mafanikio ya EAC,Jamani madai hayo hayana  ukweli wowote sababu hizo hazina Mashiko. kwani Tanzania inamoyo wa Dhati sana. kwa Vitendo kwani Tanzania imeunganisha muungano wa Nchi mbili na mpaka leoo tuko pamoja na hakuna Nchi imeweza kwa Africa nzima. (Tanganyika na Zanzibar)
Tanzania ni mwanachama wa Africa mashariki, kwani imehudhulia kila vikao na kila kitu kimefanyika kwa utaratibu hakuna hata moja tumefanya kinyume ingawa kuna mambo yanatukwaza, na kama kuna jambo halikufanyika basi limefanyika kwa maksudi kabisa.

Tumetumia Muda, Garama na nguvu zetu, Sisi tumekuwa wakwanza kuianzisha na hatuwezi kuiacha na tunatumia zaidi ya Milioni Kumi na Mbili kwa mwaka hatuwezi kuicha tu.

Najua na naskia Kinachotupa Taabu ni Misimamo yetu, Kama  Maswala ya Ardhi , ajira, Uhamiaji nadhani haya ndo yanatupa taabu huko ktk EAC.

Napata taabu sana kuamini kwamba kutofautiana kwa mawazo ndo ipelekee kutofautiana hata kwa Mambo ya muhimu haya ya EAC.
Hatuna tatizo na ualakishaji wa EAC lakini mikataba au mkataba huu unaelekeza nini cha kuanzia na kumalizia sasa sisi tunafata utaratibu na katiba husika ya EAC
Nikweli hatukuunga mkono ualakishwaji wa shirikisho kwani tunaitaji shirikisho lijengwe kwa Msingi imara, Forodha , Soko na kuimarisha na kunufaisha wananchi wote kwa usawa kwani kama ngazi hizi hazitasimamiwa ipasavyo lazima shirikisho litayumba na litavunjika kwani tunasema haya kwa uzoefu.
Tunawashauri kwa Uzoefu mkiyapuuza haya ya Uchumi itawasumbua kwani haya ya siasa hayana Taabu sana.
Msimamo huu sio wangu ila mawazo haya niyawatanzania wote, kwani tunataka kufuata msimamo wa katiba ya EAC.
Maswala ya Ardhi, Ajira na Uhamiaji .... yabaki kwa Nchi husika.
Na tulisema kuwa Wananchi wa nchi husika waweka maoni kuwa wakubali kuwa shirikisho liwepo au laa.
Inatia mashaka baada ya wanachi kuangaika kuweka EAC na baadae baadhi ya viongozi kuamua maamuzi yao na kuanza kutekeleza kitu ambacho si kizuri, kwani haijawai tokea hii.
Nchi yetu inataka kuona kuna EAC komavu, Nzuri, na Yenye mshikamano,Tanzania iko na inataka kuwepo lakini haitaki kuruka kipengere hata kimoja. kwani hii itasumbua baadae.
Napenda kuwahakikishia kuwa nitaendelea kuhudhulia na kufanya hili, na nitahakikisha kuwa haivunjiki na kama ikitokea ikafa Tafadhali Tanzania isinyooshewe Mkono kwa Kuvunjika kwake,
Tutaendelea kukumbushana, Majukumu, Mashalti na Mipango ya EAC, kwani tukifanya ivo itanufaisha wanachi jumuiya na wengine wote.

Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki EAC Asanteni kwa kunisikiliza.
...................................................................................................................................................................
Mizengo.
Namshukuru sana nkwa hotuba yake hasa pale ktk sehemu ya 3 kwani umetufanya tuwe na nguvu na Moyo.
umenifurahisha sana pale uliposema Tupo, Tunaendelea kuwepo na hatutotoka kamwe.
zile ulizo chomekea pia zile kwetu ni elimu tosha.
Ukifanya fanya hivi mala mbili mala tatu katika kipindi kijacho si Haba.

 Baada ya hotuba kulikuwa na Upigaji picha ya Kumbukumbu kwa Viongozi wote wa Nchi na Bunge hapa ni picha ya pamoja kati ya Mh, Rais, Spika wa Bunge, Jaji Mkuu, Rais wa Zanzibar Makamo wa Raisi na Viongozi wakuu na Wabunge Wote Hawa niwafanyakazi wa Bunge
 Hawa nimakatibu wa Bunge

 Baadhi ya wafanyakazi wa Bungeni
 Upigaji picha ukaisha na Rais akawa anasalimiana na Jaji Mkuu na Baadhi ya wabunge, Mawaziri na Wabunge.
 Rais aliingia ktk Gari yake na kuondoka viwanja vya Bunge.Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu