Jumamosi, 16 Novemba 2013

KINANA AENDELEA NA ZIARA WILAYA YA TUNDURU

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi wa kata ya Mbesa ,kijiji cha Mbesa wilayani Tunduru ,Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya mkoa wa Ruvuma ambayo ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.
Katibu wa NEC Itikadi na Unezi Nape Nnauye akitoa ufafanuzi kwa wananchi wa kata ya Mbesa, kijiji cha Mbesa juu ya mpango wa serikali katika kuhakikisha wananchi hao wanapata maji,Kushoto Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akisoma kitabu kinachoonyesha Mbesa ipo kwenye mpango wa kupata maji.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akishirikiana na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk Asha-Rose Migiro  kujenga daraja la mto Munjapu wilayani Tunduru.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyeshwa jinsi barabara itakavyokuwa baada ya kukamilika kwa daraja la mto Munjapu,lililopo kijiji cha Mnemasi, Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya kuimarisha chama,kusimamia ilani ya uchaguzi ya CCM 2010 katika mkoa wa Ruvuma akiwa ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa kwenye kijiji cha Mchoteka kwa staili ya aina yake ya kukimbia mchaka mchaka mapaka kwenye miradi ya ujenzi wa madarasa,maabara na nyumba za walimu katika shule ya Sekondari ya Mchoteka wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa moja ya nyumba za walimu wa shule ya Sekondari Mchoteka,wilayani Tunduru.
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akishiriki uchimbaji wa msingi wa vyumba vya maabara ya shule ya sekondari Mchoteka wilayani Tunduru.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na umati wa wananchi wa kijiji cha Mchoteka wilayani Tunduru mkoani Ruvuma.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kijiji cha Mchoteka waliofurika kutaka kumsikiliza, Katibu Mkuu alikuwa na ratiba ya kuonana na kumsalimia balozi wa nyumba kumi lakini kwa namna wananchi walivyojaa ilibidi ahutubie wananchi kwanza kabla ya kuonana na Balozi wa nyumba kumi.
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa KImataifa Dk.Asha-Rose Migiro akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Mchoteka wilayani Tunduru.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Mchoteka waliojitokeza kwa wingi kuja kuwapokea viongozi wao wa kitaifa.
Babu Akuilaya (Babu Mkuu) kama heshima aliyopewa na Machifu wa Mchoteka,Ndugu Abdulrahman Kinana akiongea na wananchi wa kijiji cha Mchoteka na kuwashukuru kwa heshima waliyompa.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi kadi kwa wanachama wapya wa CCM ambapo zaidi ya wanachama 100 wamejiunga na CCM katika kata ya Mchoteka.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata mapokezi mazuri wakati akiwasili katika kata ya Nalasi,kijiji cha Nalasi wilaya ya Tunduru.
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akiimba na akina mama wakazi wa kata ya Nalasi waliojitokeza kwa wingi kuupokea ugeni .
Umati wa wakazi wa Kijiji cha Nalasi ukiwa umejaa kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye yupo kwenye ziara katika mkoa wa Ruvuma.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kataNalasi ,wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma ambao walijitokeza kwa wingi kumsikiliza .
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya Mkina kijiji cha Mkina ,wilya ya Tunduru mkoa wa Ruvuma.
 Baadhi ya wananchi wakisikiliza hotuba za viongozi wao wa CCM Taifa wakiwa juu ya miti.
Sehemu ya wakazi wa kata ya Mkina wakisikiliza hotuba ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya mikoa ya Ruvuma na Mbeya.Wananchi hao wamemueleza Katibu Mkuu wa CCM kuwa hawapo tayari kuuza korosho kwa mkopo,pia hawapo tayari kupangiwa bei na wanunuzi, wananchi hao waliitupia lawama bodi ya korosho pamoja na vyama vya ushirikia kwani vimeonekana havina msaada kwa wakulima.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Mkina wilayani Tunduru mkoani Ruvuma ,Katibu Mkuu aliahidi kushirikiana nao katika kuhakikisha tatizo la zao la Korosho linapatiwa ufumbuzi kwani ni zao pekee linaloweza kuinua uchumi wa eneo hilo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha moja ya leseni za dereva wa Boda Boda ambazo zilitolewa baada ya madereva hao kupata mafunzo ya kuendesha na ya usalama barabarani yaliosimamiwa na mbunge wa Tunduru Kusini Mtutura Abdallah Mtutura.
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu