Unordered List


KINANA AITEKA TUNDUMA

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Tunduma katika viwanja vya vya shule ya Msingi Mwaka ambapo alizungumzia mambo mbali mbali ukiwemo urasimu uliokuwepo mpakani kati ya Tanzania na Zambia unaosababisha msongamano wa malori na kushauri uweke utaratibu wa kufanya kazi masaa 24 huku kukiwa na zamu za wafanyakazi kuingia kazini kwa muda utakaopangwa,Katibu Mkuu pia aligusia utaratibu wa kulipa kodi kwa wafanyabiashara wadogo uangaliwe upya ili wafanya biashara wadogo wapunguziwe kodi,pia alisema kwa kuwa Serikali haina uwezio wa kuajiri watu wote basi itengeneze mazingira rahisi kwa vijana kujiajiri.
 Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akihutubia wakazi wa kata ya Tunduma kwenye viwanja vya shule ya msingi Mwaka na kushauri wakina mama kujiunga kwenye vikundi ili waweze kupata mikopo kirahisi na pia elimu ya ujasiriamali kwa wanawake bado inahitajika kwa kiasi kikubwa na pia kusisitiza hata kiwango cha wanafunzi wa kike wanaosoma elimu ya sekondari ni ndogo na kusisitiza kila mzazi anatakiwa kutambua kuwa elimu kwa mtoto wa kike ni kitu muhimu sana.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Tunduma na kuwaambia wananchi hao wasihadaike na maneno mengi ya upinzani kuhusu Katiba Mpya, kwani Katiba hiyo haipigi kura wanaopiga kura ni wao wananchi.

 Wanachama na Wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi wakicheza muziki na Dk.Asha-Rose Migiro Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa kwenye viwanja vya shule ya Msingi ambapo mkutano mkubwa ulifanyika.
Wanachama na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi wakiwa wamembeba juu juu Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kwenye viwanja vya shule ya msingi Mwaka ambapo mkutano mkubwa ulifanyika na kuhudhuriwa na maelfu ya watu wa mji wa Tunduma.

Chapisha Maoni

0 Maoni