Unordered List


KINANA: URASIMU UNAUMIZA WANANCHI

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Masoko ,kijiji cha Lupando wilaya ya Rungwe ,Katibu Mkuu waliwaambia wananchi hao kuwa urasimu na umangi meza wa watendaji wa serikali ndio unachangia kwa kiasi kikubwa kurudisha maendeleo yao nyuma na kusema kamwe CCM haitokubali hali hiyo iendelee na kusisitiza CCM itahakikisha wananchi wanapata haki zao za msingi kwanza.
 Mwakilishi wa Wananchi wa Kijiji cha Lupando Ndugu Wema Mwaipopo akiomba sana kwa niaba ya wananchi wake watatuliwe suala la maji,umeme na barabara kwani hizo ndio zilikuwa ahadi kubwa za Mbunge na Rais.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya Masoko kijiji cha Lupando na kuwaambia wananchi kuwa wapinzani ni sawa na Jogoo hata aamke saa ngapi hawezi fungua mlango,na kuwasisitiza wananchi wa kijiji hicho ni CCM pekee inayoweza kuwazungumzia na kero zao zikatatuliwa.
 Asumwisi Asagwile Mwatebela ,Mlezi wa Vijana wa Chadema wilaya ya Rungwe akirudisha kadi yake kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na kujiunga rasmi na CCM.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Kiwira Rungwe na wakati wa ufunguzi wa vikundi viwili vya wajasiriamali ambapo aliwaambia vijana maendeleo yanaletwa kwa kufanya kazi kwa kujituma na waondoe mawazo kuwa Katiba mpya ndio itakuwa mwarobaini wa matatizo yao.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia maabara ya shule ya Sekondari ya Ikuti ikiwa moja ya sehemu ya ahadi ya serikali ya kujenga maabara katika kila shule ya Sekondari ya Kata.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa Nyumba za walimu wa shule ya Sekondari Ikuti wilayani Rungwe.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahmani Kinana akiongozana na Mkuu wa Shule ya Ikuti Ndugu Emmanuel Ngasa pamoja na viongozi wengine wa chama na serikali baada ya kukagua jengo la hosteli la shule ya sekondari ya Ikuti.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wakazi wa shina namba 2,Butonga Tawi la Ikuti kwa Balozi James Mbasi, na kusisitiza viongozi wote wa CCM waige mfano wa Mabalozi kwani wanafanya kazi kwa kujitolea katika kukiimarisha na kukijenga chama.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahama Kinana akikata utepe kama ishara ya kuwasha umeme katika kituo cha Afya cha Ikuti wilayani Rungwe.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongozana na viongozi wa wilaya ya Rungwe pamoja na wananchi kuelekea kwenye uwanja wa mkutano Ikuti.
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Wilaya Ndugu Richard Kasesela akipiga ngoma ya Kitongo kabla ya kuanza kwa mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Ikuti ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Mbunge wa Viti Maalum Wananwake mkoa wa Mbeya Dk.maru Mwanjelwa akicheza ngoma  kabala ya kuanza kwa mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Ikuti ambapo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na viongozi wa kitaifa aliofutana nao Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro na Katiibu wa NEC Itikadi na Uenezi walihutubia.
 Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya Dk.Mary Mwanjelwa akihutubia wakazi wa kata ya Ikuti na kuwaambia wanawake waandae vikundi vyao kwani Benki ya wanawake karibia itafunguliwa hivyo fursa za kupata mikopo zitaongezeka na kusaidia kufanya biashara kwa ufanisi na kuleta maendeleo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Ikuti wilayani Rungwe mkoa wa Mbeya na kusema serikali ipunguze matumizi yasiyo na lazima na badala yake nguvu nyingi iletwe kwa wananchi katika kuwaletea maendeleo.
 Wakazi wa Ikuti wakiwa juu ya mti wakisikiliza kwa makini hotuba za viongozi wao ambazo nyingi zilijibiwa vizuri hasa suala la umeme ambalo wananchi wanaweza kulipa kidogo kidogo.
Dk.Mary mwanjelwa akizungumza na akina Mama wauza ndizi wa kijiji cha Iponjola kata ya Rufingo wilaya ya Rungwe na kuwataka waanzishe vikundi kwani benki ya wanawake ipo karibuni kufunguliwa katika mkoa wa Mbeya hivyo itawasaidia kupata mikopo kwa riba nafuu.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alisimama kuwasalimu wakina mama hao kisha kuutambulisha uongozi wote aliokuwa nao kwenye msafara.

Chapisha Maoni

0 Maoni