Unordered List


Watu 29 wafariki kwenye ajali A. Kusini



Waziri wa usafiri ameagiza uchunguzi kufanywa kubaini kiini cha ajali

Watu 29 wamefariki na wengine wengi kujeruhiwa kwenye ajali ya basi iliyotokea nchini Afrika Kusini.
Ajali hiyo ilitokea, wakati basi lilipogongana ana kwa ana na lori Jumatatu jioni katika mkoa wa Mpumalanga Mashariki mwa nchi.
Basi hiyo inasemekana ilianguka baada ya kwenda mrama wakati mvua kubwa ilipokuwa inanyesha katika barabara ya Moloto inayosifika kwa ajali za mara kwa mara.
Afrika Kusini ni moja ya nchi zenye idadi kubwa ya ajali za barabarani duniani, huku watu elfu kumi wakifariki kila mwaka.
Rais Jacob Zuma alielezea kushtushwa sana na idadi ya watu waliofariki. '' ajali hizi za barabarani lazima zikome. Haikubaliki kabisa,'' alisema Zuma
Mwandishi wa BBC, Milton Nkosi mjini Johannesburg anasema kuwa ajali hiyo ilitokea baada ya dereva kukosa uwezo mzuri wa kuona barabara kutokana na mvua kubwa.
Kwa mujibu wa walioshuhudia ajali hiyo, magari mengine mawili yalianguka juu ya basi hiyo.
Waziri wa usafiri Dipou Peters, ameamuru uchunguzi kufanyika ili kubaini kiini cha ajali hiyo.
Takriban watu 50,000 hutumia usafiri wa umma kwenda kazini kila siku

Chanzo:- BBC

Chapisha Maoni

0 Maoni