• UVCCM TAIFA

  SAUTI YA VIJANA,SAUTI YA UMMA.CCM MPYA,TANZANIA MPYA.

 • UVCCM TAIFA

  MWAKA MMOJA WA SERIKALI YA AWAMU YA TANO.

 • This is default featured slide 3 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

 • This is default featured slide 4 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

 • This is default featured slide 5 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

Jumamosi, 28 Desemba 2013

RAIS KIKWETE AREJEA NCHINI AKITOKEA MAREKANI KUCHEKIWA AFYA Makamu wa Rais Dk.Mohamed Gharib Bilal akimlaki Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya Kuwasili nchini akitokea jijini New York Marekani ambapo alikwenda kwa ukaguzi wa kawaida wa afya yake.
Share:

JAJI WARIOBA KUKABIDHI RASIMU YA KATIBA MPYA KWA RAIS KIKWETE NA DR. SHEIN JUMATATU

JAJI WARIOBA
DAR ES SALAAM, Tanzania
Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Tume ya Mabadiliuko ya Katiba, Assaa Rashid, imesema, Jumatatu ijayo ya Desemba 30, 2013, Tume hiyo itakabidhi rasimu hiyo kwa Rais Jakaya Kikwete na Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein.
Share:

Alhamisi, 19 Desemba 2013

DR. FENELLA AFUNGUA SEMINA YA WAZAZI WILAYA YA KINONDONI ILIYOFANYIKA MOROGORO

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Waziri wa Habari, VIjana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara, akimkabidhi cheti Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Kata ya Kawe,  Benjamin Joseph,
Share:

Jumatano, 18 Desemba 2013

POSHO KWA WAWAKILISHI WA WANANCHI NI KIKWAZO CHA MAENDELEO YA TAIFA


Picha_no_2
Na. Zainul Mzige
Ingawaje Tanzania inaitwa nchi masikini pamoja na kwamba wahisani na wadau wa maendeleo wanasema ni nchi inayoendelea lakini kwa ujumla na kwa yeyote anayeijua nchi yetu kwa maana ya hali ya maisha ya wananchi wake, ni jambo la hatari kwa kikundi kidogo cha watu waliokalia ofisi za umma na kujipangia utaratibu fulani wa kujinufaisha.
Share:

WAZIRI WA ARTHI, MAKAZI NA NISHATI MHE. RAMADHAN SHAABAN AFUNGUA JENGO LA OFISI(ZANZIBAR)WAZIRI WA ARDHI, MAKAZI NA NISHATI MHE. RAMADHAN SHAABAN AFUNGUA JENGO LA OFISI(ZANZIBAR)

za_9189d.jpg
 Waziri wa Ardhi, Makazi na Nishati Mhe. Ramadhan Shaaban akikata utepe wakati akifungu Jengo la Ofisi ya Kitengo Shirikishi cha Afya ya mama na mtoto kiliopo Kidongo Chekundu nje kidogo ya Mji wa Zanzibar, ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Share:

Jumanne, 17 Desemba 2013

MKE WA RAIS, MAMA SALMA KIKWETE AHUDHURIA MKUTANO WA WANAWAKE AFRIKA MASHARIKI NA KATI NA ASIA

MKE WA RAIS, MAMA SALMA KIKWETE AHUDHURIA MKUTANO WA WANAWAKE AFRIKA MASHARIKI NA KATI NA ASIA

 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokewa na Mwanzilishi na Afisa Mtendaji Mkuu wa CEO Clubs Network, Bwana Tareq Ahmed Nizami,
Share:

Jumatatu, 16 Desemba 2013

MP. Dkt, Hamisi Kigwangalla na PESA ZA USHURU WA HUDUMA kutoka Resolute Tanzania: (Nzega)

PESA ZA USHURU WA HUDUMA kutoka Resolute Tanzania:
Mbunge huyu Kijana wa Jimbo la Nzega na Mwenyekiti wa TAMISEMI  Alianza kwa Kusema hivi

 "Ndg. Gisberth Kabamba na ndugu zangu wengine wote mnaonisoma hapa. Kuna maneno mengi sana yanayosemwa kuhusiana na upatikanaji wa pesa za ushuru wa huduma kutokana na uwepo wa mgodi wa uchimbaji dhahabu Lusu Nzega. Kuwa ni nani haswa aliyezileta pesa hizo? Japokuwa si muhimu sana kumjua aliyezileta bali kushukuru kwamba tu kuwa zimekuja. Kwa faida ya historia na kuweka sawa kumbukumbu ni vizuri hili jambo likaelezwa.
Acha leo niseme na mimi mnisikie. Siku zote niliona si muhimu sana kuzungumzia hilo maana niliamini ukweli unajulikana. Na kwa tabia ya ukweli, kuwa haubadilishwi na uongo, niliamini ukweli utabaki kuwa ukweli na hivyo sikuona haja ya kueleza. Pia niliamini kuwa wananzega wenzangu wanajua ni nini kilifanyika mpaka pesa zile zikapatikana. Na nilijua watu makini wakifanya tafakuri tunduizi hawatopata tabu kujua kuwa mgodi huu ulikuwepo Nzega kwa zaidi ya miaka 14, na kulipita wabunge na madiwani wengi na walijua kuna sheria ya kudai ushuru wa huduma, sasa nini kiliwafanya wao hawakufanikiwa kuzidai pesa hizi na leo zimefanikiwa kudaiwa. Kuna kitu gani tofauti hapo kimetokea?
Hadithi ya kufikia pesa hizi kupatikana ni ndefu na mimi binafsi sikupenda kuyasema mengine ambayo hayakupaswa kusemwa kwenye umma.
Kwanza, historia ya jambo hili ikoje? Wakati nagombea na hata baada ya kuchaguliwa kuwa MB wa Nzega, nimejikuta na tabia ya kutembelea sehemu mbalimbali za kijamii ambazo zinanipa heshima ya kuhojiwa maswali na kuyajibu. Utamaduni huu niliukuta kwa mara ya kwanza sana sana pale kwenye kijiwe maarufu cha BBC, ambacho wengi husema kina wapinzani wengi wanaofika pale kujadili siasa za Nzega, Kitaifa na Kimataifa. Pale nilikutana na wazee ambao walinifikishia malalamiko yao ya madai kule Lusu na malalamiko yanayohusiana na mgodi wa Golden Pride. Nikiwa kwenye kampeni kama mgombea wa CCM, kuna watu wa maeneo ya mgodi walikataa kupigia kura CCM kwa kuwa waliahidiwa na mgombea wa CHADEMA kuwa akishinda atahakikisha wanalipwa stahiki zao. Nikaenda binafsi kuongea nao, bahati nzuri nikakuta wakiwemo watu wangu kama akina Mzee Jailos, Mzee Sudi (Mungu amrehemu) na akina Bilantanye, nikawasihi wasinisuse wanisaidie tuchukue Ubunge nami nitawapigania kufa na kupona.
Niliposhinda Ubunge niliamua kuanza na jambo hili. Nikifanya mikutano ya kushukuru wananchi kwa kunichagua nilifanya mkutano viwanja vya parking na watu wale walinisomea risala huku wakitoa machozi, niliumia sana, nikasema nitapigana pembeni yao. Nikaanza utafiti wa namna gani nifanye ili niweze kuwasaidia. Niliandika barua nyingi ambazo hazikuzaa matunda. Nilipigana mpaka kuhakikisha hili jambo limemfikia Mhe. Waziri Mkuu na mwishowe kwa Mhe. Rais, kwa namna na sura tofauti tofauti. Nimewasilisha hoja binafsi kuhusu jambo hili zaidi ya mara 10 bila mafanikio. Nimechangia Bungeni zaidi ya mara 5, maswali zaidi ya mara 3 bila mafanikio. Nimefanya mikutano na mawaziri kuanzia Ngeleja mpaka Prof. Muhongo bila mafanikio. Kutokufanikiwa kwangu hakukunifanya nichoke ama niache kufuatilia. Nilikomaa zaidi na kubuni mbinu mpya kila siku. Sikukata tamaa. Niliendelea kupigana. Wasionipenda walinipa majina mengi, wengine wakithubutu hata kupeleka fitna na majungu kwa wakubwa kwenye chama change eti mimi ni mpinzania!
Mara kwa mara nilikutana na wale wachimbaji nikiwapa mrejesho wa ninachokifanya. Na wao walinipa moyo kwa kuendelea kuniamini na kuvumilia bila kuchoka.
Nikaamua kutumia hatua kali zaidi za nguvu ya umma - tukaomba kibali cha kuandamana, tukanyimwa, tukafanya mikutano haramu tukapata matatizo. Mwishowe Mkuu wa Mkoa akaamua kutupa kibali tuandamane kuonesha hasira zetu. Nikatoa hotuba kali sana pale Mwabangu huku nikijiapiza kwenda kuvamia mgodi kama wazungu hawatokubali kulipa pesa zote tunazodai. Maafisa uhusiano wa mgodi walikuwepo.
Niliendelea kupigana kutokea kila kona. Katika Baraza la madiwani, niliamua kuliingiza jambo hili kama hoja yangu binafsi nikimtaka DED wa Nzega, enzi hizo Ndg. Kyuza Kitundu, awaandikie ‘demand note’ watu wa mgodi ili wasipolipa twende tukakamate mali zao zenye thamani ya deni hili, kwa mujibu wa sheria na sheria ndogo (by-laws) zetu, akabisha sana kwa woga wa kuanzisha mapambano na shirika hili kubwa la kimataifa, niliendelea kumbana kwenye vikao mpaka kufikia kutishia kumwajibisha kwa mujibu wa kanuni kwa kutotekeleza maamuzi ya vikao – akaamua kuandika! Nao wakaanza vita ya kisheria kwa kutujibu kisheria kupitia mawakili wao, REX Attorneys. Vita hii haikuzaa matunda baada ya kukwamishwa na mazungumzo yaliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa. Sikuchoka. Niliendelea kufuatilia.
Ni siku tulipoandamana, wakaona umati ulioshiriki na ukali wa hotuba na michango yetu kwenye mkutano ule wa Mwabangu na wakizingatia tishio la kuvamia mgodi ndani ya siku tisini ndipo nikapigiwa simu na Waziri Muhongo akinitaka tuonane Dodoma tuzungumze kuhusu jambo hili wakiwepo wawakilishi wa mgodi na wawakilishi wa Halmashauri ya Nzega. Na kwenye mazungumzo yangu na Muhongo ambaye alimuita Naibu Waziri Madini Massele ndipo wakaniambia tuzungumze kwanza kabla ya kuchukua hatua hizo kali, nilimuelewa na nikakubali. Katika mkutano huu nilioneshwa email zilizotoka kwa watu wa Resolute wakilia lia kuwa MB wa Nzega Dkt. Hamisi Kigwangalla ni mkali sana na ana nia ya kuchafua hali ya hewa pale mgodini na kwamba wanahofia usalama wao na ule wa mali zao.
Baada ya miadi hii ya kukutana tulifunga safari ya madiwani na watumishi wa Halmashauri kuambatana nasi Wabunge wawili Dodoma kuhudhuria kikao hiki. Kikao hiki na hoja zote za madai haya zilitolewa na mimi maana nilikuwa na uelewa mpana zaidi wa suala hili kutokana na ufuatiliaji wangu wa kina na wa muda mrefu. Baadhi ya madiwani waliokuwepo ni mashahidi kwenye hili. Wahe. Patrick Gululi Mbozu, Pele Izengo Anthony, Bazilio Furaha Lazaro, Sawaka Paraxedes Shita na Kalori Ng’hwagi Masanja walikuwepo, waulizeni watawaambia ukweli kama mkitaka kuthibitisha hili. Mhe. Selemani Zedi (MB) alikuwa na dharura ya kikazi na hivyo alikaa mwanzoni tu wakati wa utambulisho kisha akaomba udhuru akatoka. Kuna saa niligonga hadi meza kwa hasira mpaka wakawa wananituliza. Kwa hoja niliwasambaratisha wazungu na kuhakikisha Naibu Waziri Massele na wataalamu wake wanakaa upande wa kuamua kwa faida ya Nzega.
Mhe. Selemani Zedi alinisaidia sana kuhakikisha tunapata mkataba kamili baina ya Resolute na Serikali ya Tanzania, kipindi hicho akiwa mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini. Kabla sijaupata mkataba huu, nilipewa kurasa zote nyeti za mkataba na rafiki zangu watumishi wa umma na ndizo zilizonitia nguvu ya kuendeleza mapambano tangu awali bila wasiwasi wa ‘kuchemka’ ama kushindwa.
Mkuu wa Wilaya ya Nzega, aliyeondoka, Mama Florence Horombe, mumkumbuke wana Nzega zaidi kwa kuniweka ‘lupango’ bila sababu za msingi, na kwa kunizuia nisiingie kwenye geti la mgodi kwenye kikao cha kujadiliana kuhusu madai haya. Kama si Mhe. Zedi naye kukataa kuingia na madiwani, watumishi wote wa ofisi ya DED na ya Mkuu wa wilaya kumfuata, mimi nikiwa kimya tu, wakisema 'kama aliyeanzisha hoja hii hatakiwi humo ndani, naye ndiye analijua jambo hili, sisi sasa tutaingia kusema nini?’ ‘…basi nasi hatuingii, tugeuze magari turudi Nzega mjini'. Msimamo huu ulikuwa muhimu kwa ‘movement’ nzima maana ilionesha kuwa si ‘wehu’ wangu tu unaosababisha mvutano huu na kwamba ni mtazamo wa watu wengi ‘wazima’ na kwamba tuna msimamo wa pamoja kwenye jambo hili kama wilaya.
Mumkumbuke pia Katibu wa CCM wilaya Nzega wakati huo Ndg. Kajoro Vyohoroka kwa kuandika barua kwa viongozi na wanachama wenzangu wote wa CCM akiwaamrisha wasishiriki maandamano ya Mbunge kudai haki za Nzega; na pia kwa kuandika barua kwa OCD Nzega kumtaka asitishe maandamano hayo kwa kuwa CCM haijabariki (kumbe ni yeye binafsi tu hajabariki maana hata mimi ni CCM na hakukuwa na kikao kilichotoa msimamo huo).
Pia mnapofuatilia jambo hili, msimsahau Katibu wa CCM Mkoa wa Tabora Ndg. Iddi Ali Ame kwa kuamua KUYARUHUSU maandamano hayo kwa kuwa aliona yana maslahi ya umma ninaouwakilisha.
Pia msiusahau mchango wa Mwenyekiti wa Halmashauri na Mkurugenzi wake na zaidi mwana Sheria (mke wa Ndg. Mwaluko) aliyetushauri vizuri kwenye vikao na kusema Mbunge Dkt. Hamisi Kigwangalla ana hoja nzito iliyosimama kisheria. Na kwa kuendelea kunishauri mara kwa mara na kunipa taarifa za namna alivyoendelea kujibishana nao kwa barua.
Huu ndiyo mchango wa kila mtu (kwa ufupi tu). Sitaki kuwa mtoa hukumu kuwa ni nani alizileta pesa zile. Niwaache mtoe hukumu wenyewe. Kuna watu walinikejeli kwa kuandika waraka wa kunikashifu kwenye mitandao wakidai kuwa sintofanikiwa kwenye madai hayo lakini pesa zilipotoka walikuwa wa kwanza kudai zimeletwa na watu wanaowajua wao na wakitoa maelekezo ya namna ya kuzitumia pesa hizo. Mpaka leo pesa hizi hazijatumika kwa sababu ya mivutano na chokochoko inayofanywa na wanasiasa uchwara (ambao mwanzoni walidharau harakati hizi). Nimeyazoea haya kwa kuwa ni siasa ndogo ndogo, na kwa mwanamabadiliko na mwanamapinguzi kama mimi sipati tabu hata kidogo, ila najituma kufanya kazi zangu kwa bidii na weledi wa hali ya juu nikijua ipo siku wananzega watanikumbuka. Kama siyo mnaoishi leo, basi watakaokuja kuishi baadaye."

Alimaliza hivo alipokuwa akiongea na wana Nzega 
Share:

KATIBU WA ITIKADI NA UENEZI, Ndugu Nape Nnauye
Share:

KAMATI KUU YA CCM YAWAHOJI MAWAZIRI SABA

  Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika kikao chake kilichofanyika jana mjini Dodoma chini ya Mwenyekiti wake Rais Jakaya Kikwete imeibuka na masuala mazito kadhaa, ambayo leo, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (pichani) ameyaeleza wakati akizungumza na waandishi wa Habari, Katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Lumumba jijini Dar es Salaam.


Moja ya mambo ambayo Nape amezungumzia, ni kuhusu Kamati Kuu hiyo kuwahoji Mawaziri saba, kujibu kero au mambo kadhaa ambayo yaliibuliwa wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana iliyomalizika hivi karibuni katika mikoa ya Mtwara, Ruvuma, Mbeya na Njombe.

Nape  alisema, Kamati Kuu iliwahoji mmoja baada ya mwingine, kuanzia saa tano asubuhi hadi jioni, baada ya kila mmoja kufika akiwa ameandaa majibu ya tuhuma au hoja alizokuwa ametakiwa kujibu mbele ya Kamati Kuu hiyo.

"Kwa kuwa mawaziri hao tulikuwa tumeshawapelekea hoja zinazowahusu ambazo tulizipisha kwa kiranja wao Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wengi wao walifika wakiwa na mafaili yenye majibu, ambapo waliingia na kujieleza mmoja baada ya mwingine, na baada ya maelezo ya kila mmoja wajumbe walitoa mapendekezo kwa Mwenyekiti, Rais Jakaya Kikwete", alisema Nape.

Hata hivyo Nape alisema, si vema kueleza kwenye vyombo vya habari kuhusu mapendekezo ambayo Kamati Kuu ilimshauri Mwenyekiti kuchukua, akisema kufanya hivyo itakuwa sawa na kumshinikiza kiongozi huyo kutekeleza mapendekezo yao kwa lazima na hivyo kuharibu maana nzima ya ushauri.

"Sisi tulichofanya ni kumpa mapendekezo, naye kwa mujibu na namna atakavyoona inafaa, atachukua hatua, ambavyo si lazima kumfukuza Waziri Kama wengi wanavyotaka iwe, bali anaweza kuchukua hatua yoyote ili mradi yeye mwenyewe kwa mamlaka aliyo nayo ataona ina manufaa yatakayotoa majibu ya kero zilizosaababisha kila mmoja wa mawaziri hao kuitwa mbele ya Kamati Kuu", alisema Nape.

IFUATAYO NI TAARIFA YOTE KAMA ALIVYOITOA NAPE LEO.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imekutana mjini Dodoma kwa kikao chake cha kawaida tarehe 13/12/2013. Kikao hicho kiliongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Ndg. Jakaya Mrisho Kikwete.

Pamoja na mambo mengine Kamati Kuu ilipokea taarifa ya ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana na baadhi ya wajumbe wa Sekretarieti kwenye baadhi ya mikoa nchini.
Kamati Kuu imepongeza ziara hizo kwa kuwa na mafanikio makubwa na kwa jinsi zilivyoongeza uhai wa Chama na zilivyojishughulisha na mambo na mahitaji ya wanachi.

Aidha Kamati Kuu imeipongeza sana Serikali kwa utekelezaji mzuri wa Ilani ya uchaguzi ya CCM kwenye maeneo yote ambayo Katibu Mkuu ametembea. Maeneo yaliyopongezwa ni pamoja na Miundombinu hasa barabara, hatua kubwa kwenye fursa na ubora wa elimu, maeneo ya afya na umeme vijijini.

Kamati Kuu iliwaita mawaziri saba kuja kutoa maelezo ya mambo mbalimbali yaliyoibuliwa kwenye ziara hizo za Katibu Mkuu wa CCM. Mawaziri hao ni;-

i). Ndg. Christopher Chiza- Waziri wa Kilimo,Chakula na Ushirika
ii). Ndg. Shukuru Kawambwa- Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
iii). Ndg. Celina Kombani - Waziri wa Utumishi
iv). Ndg. Hawa Ghasia -Waziri wa TAMISEMI
v). Ndg. Abdallah Kigoda- Waziri wa Viwanda na Biashara
vi). Ndg. Mathayo David Mathayo- Waziri wa Mifugo na Uvuvi
vii). Ndg. Saada Mkuya- Naibu Waziri wa Fedha( kwa niaba ya Waziri wa Fedha).
Baada ya maelezo ya kutosha kutoka kwa mawaziri husika, Kamati Kuu iliagiza yafuatayo kwa Serikali;-

1.Kuhusu wakulima wa Pamba
(i). Serikali iangalie upya upatikanaji wa pembejeo za ruzuku kwa wakulima wa Pamba nchini.
(ii). Uwepo wa mbegu bora ni muhimu lakini ni vizuri pakawa na ushindani unaozingatia ubora ili kuondoa ukiritimba wa mtengenezaji mmoja, hivyo kusaidia bei kuwa nzuri kwa wakulima. Hata hivyo Chama kimeiagiza serikali kutowalazimisha wakulima kutumia mbegu ya Quiton badala yake elimu itumike zaidi badala ya nguvu. Serikali imetakiwa kuangalia upya utaratibu wa kutoza bei ya mbegu ya Quiton kwa dola za kimarekani badala ya pesa ya kitanzania,wakizingatia mbegu hiyo inazalishwa nchini.
(iii).Kamati Kuu imepongeza juhudi za Serikali kuvutia wawekezaji kwenye viwanda vya pamba mjini Shinyanga, hata hivyo imeitaka Serikali kuangalia upya urasimu katika uwekezaji wa viwanda nchini hasa vinavyoongeza thamani ya mazao na kutoa ajira nyingi nchini.

(iv). Kuhusu kilimo cha mkataba kwa wakulima wa Pamba, Serikali imetakiwa kuratibu utaratibu wa kilimo hicho cha mkataba ili kuhakikisha kunakuwa na sheria na kanuni zinazosimamia mfumo huo, ili kuwe na haki kwa pande zote mbili. Aidha wakulima wasilazimishwe kufanya kilimo cha mkataba bali waingie kwa hiari yao wenyewe.

2. Kuhusu wakulima wa Korosho.
(i). Pamoja na kuridhishwa na hatua za muda mfupi kwa msimu wa korosho kwa mwaka 2013/2014 ambazo zimesaidia bei na soko kuwa afadhali, bado Kamati Kuu imesisitiza Serikali kujipanga kutatua tatizo la korosho kwa suluhisho la kudumu kwa kuhakikisha korosho ina banguliwa nchini.

(ii). Serikali imetakiwa kuangalia upya orodha ndefu ya makato wanayokatwa wakulima hasa wa korosho na vyama vya msingi au mamlaka zinginezo ili kuondoa makato yasiyo ya lazima ili kuongeza kipato cha mkulima.

(iii). Serikali pia imetakiwa kuangalia upya mfumo wa uendeshaji wa vyama vya ushirika nchini ili uwe ni ule wenye tija kwa wakulima na nchi kwa ujumla badala ya huu wa sasa unaotoa mwanya kwa walaji kujipenyeza.

3. Kuhusu pembejeo za ruzuku
(i). Kamati Kuu imepokea taarifa ya malalamiko ya wakulima juu ya ufanyaji kazi wa mbolea ya Minjingu na kuagiza kuwa pamoja na kuendelea na utafiti wa nini kinachotokea kwenye mbolea hiyo ya Minjingu kiasi cha kuleta malalamiko yote hayo, wananchi wawe huru kutumia mbolea wanayoitaka badala ya kulazimishwa kutumia mbolea wanayoilalamikia ya Minjingu.

(ii). Serikali iangalie utaratibu bora wa kuratibu swala zima la pembejeo za ruzuku ili lifaidishe zaidi wakulima walio wengi badala ya utaratibu wa sasa ambao licha ya kulalamikiwa na wakulima unaotoa mwanya kwa watu wachache kutumia vibaya utaratibu huo kuiibia serikali na wakulima.

4. Kuhusu wakulima wa mahindi.
(i). Pamoja na Serikali kuanza kulipa madai ya wakulima wa mahindi kwa mikoa ya Ruvuma baada ya ziara ya Katibu Mkuu kwenye maeneo hayo, bado serikali imetakiwa kumalizia malipo yaliyobaki na kuhakikisha wanakomesha utaratibu wa kuwakopa wananchi mazao yao bila kuwalipa.

(ii). Utaratibu uwekwe wa kufanya tathimini mapema ya mahitaji na uwezo wa kununua  mahindi wa Serikali ili kuepusha utaratibu wa kuchukua mahindi ya wakulima bila kuwalipa.

5. Kuhusu madai mbalimbali ya waalimu.
(i). Kamati Kuu imesisitiza kupandishwa vyeo na kulipwa stahiki  zao waalimu ni haki yao ya msingi hivyo lazima itekelezwe bila kuwa na visingizio na ifanyike kwa haki.

(ii). Kamati Kuu imeiagiza Serikali kukamilisha haraka uhakiki wa madai ya waalimu na kuwalipa haki zao zote mapema iwezekanavyo. Lakini Kamati Kuu imeitaka Serikali kuhakikisha madeni haya hayazaliwi tena kwa kuweka mfumo utakao zuia madeni haya kuzaliwa.

(iii). Kuhusu wakuu wa idara mbalimbali wasiotenda haki kwa waalimu, na wale wanaotumia lugha mbaya na za kejeli kwa waalimu wakibainika wachukuliwe hatua mara moja.

(iv). Pamoja na kuwa Serikali inaangalia utaratibu bora wa kuboresha mawasiliano kati ya wizara zinazohusika na kusimamia waalimu, Kamati Kuu imeitaka Serikali jambo hili lifanyike mapema ili kupunguza malalamiko ya waalimu.

6. Kuhusu ubadhirifu kwenye Halmashauri.
(i). Kamati Kuu imekemea watendaji wachache wanaojihusisha na ubadhirifu kwenye Halmashauri mbalimbali nchini. Imewataka madiwani wa CCM kuwa wakali na wasiamamie vizuri halmashauri zao kuhakikisha fedha inatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na kupata thamani ya fedha.
(ii). Aidha Serikali imetakiwa kuchukua hatua kali na kwa haraka kwa wote wanaobainika kufanya ubadhirifu, ili iwe fundisho kwa wengine.

(iii). Serikali imeshauriwa kuangalia upya sheria kama zinakidhi mahitaji ya wakati na mazingira ya sasa ili kuongeza uwezo wa udhibiti na kuokoa pesa za walipakodi zinazopotea kwa walafi wachache kwenye Halmashauri mbalimbali nchini.

7. Kuhusu tatizo la Maji nchini.
Kamati Kuu ilipokea taarifa ya tatizo kubwa la maji nchini, ambalo lilijitokeza kila sehemu aliyotembelea Katibu Mkuu. Chama kimeishauri Serikali kuchukua juhudi na mkakati wa makusudi na dharura kulitafutia ufumbuzi wa haraka na wakudumu tatizo la upatikanaji wa maji nchini.

8. Kuhusu migogoro ya Aridhi, Wafugaji na Wakulima.
Pamoja na kupokea taarifa juu ya migogoro mbalimbali ya wakulima ,wafugaji na wakulima nchini, kamati kuu imepongeza uamuzi wa bunge kuunda Kamati teule ya bunge na uamuzi wa kuiagiza kamati ya kudumu ya bunge ya aridhi, maliasili na mazingira kuchunguza migogoro hii na kutoa mapendekezo juu ya namna bora ya kuimaliza kabisa migogoro hii.

Aidha kamati kuu imeitaka Serikali na wabunge wa CCM kuzijadili kwa makini ripoti hizo na kufikia hitimisho la migogoro hii nchini. Hata hivyo Kamati Kuu imeitaka Serikali kuangalia upya utaratibu uliotumika kuwamilikisha watu wachache maeneo makubwa ya aridhi, ambao wameshindwa kuyaendeleza badala yake wanayatumia kuwakodishia wakulima wadogo.

Aidha maagizo yote haya yatatolewa taarifa kwenye Chama mara kwa mara, ili kuwezesha Chama kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2010/2015.

Imetolewa na;-
Nape Moses Nnauye
Katibu wa Itikadi na Uenezi
14/12/2013

Share:

Jumamosi, 14 Desemba 2013

Baraza la Mawaziri Hali ni Tete


Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM chini ya Mwenyekiti wake Rais Jakaya Kikwete, imeanza kuwahoji mawaziri waliotajwa ni ‘mzigo’ kwa Serikali.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, jana alilithibitishia gazeti dada la Mwananchi, The Citizen juu ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu (CC), lakini hakuwa tayari kuingia kwa undani kuhusu ajenda.
Hata hivyo, habari za ndani zilieleza kwamba miongoni mwa ajenda kuu za CC ni kuwahoji mawaziri wanaolalamikiwa na wananchi, kwamba wameshindwa kutekeleza majukumu yao.
Wakiwa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma, Nape aliwatupia lawama mawaziri wakati akielezea changamoto zinazowakabili wakulima ambao ni asilimia 80 ya Watanzania, huku mawaziri husika wakikaa kimya.
Mawaziri waliotajwa mzigo ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa; Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza na Naibu wake, Adam Malima, kwamba wameshindwa kazi na alipendekeza wang’olewe.
Hata hivyo, gazeti hili jana lilishuhudia mawaziri kadhaa wakifika na kuingia kwenye mkutano wa CC, taarifa zingine zilisema mawaziri waliofika kwenye kikao hicho walihojiwa na wajumbe wa CC.
Kuhojiwa na CC
Mawaziri waliohojiwa na CC hadi kufikia saa 8:00 mchana jana walitajwa kuwa ni Naibu Waziri wa Fedha, Saada Mkuya na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza. Mkuya ndiye ambaye kwa sasa anaisimamia Wizara Fedha kutokana na Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa kulazwa nchini Afrika Kusini akisumbuliwa na maradhi ambayo hayajatajwa.(P.T)
Waandishi wa gazeti hili jana waliwashuhudia takriban mawaziri 10 wakiingia katika ofisi za makao makuu ya CCM, Dodoma, maarufu White House, huku baadhi wakiwa si wajumbe wa CC.
Habari zilizotufikia jioni ziliwataja wengine kuwa ni Dk David Mathayo David (Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi), Hawa Ghasia (Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-Tamisemi), Dk Kawambwa, Celina Kombani (Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma).
Dk Kawambwa wakati akitoka kwenye kikao cha CC aliulizwa na waandishi wa habari kilichotokea na yeye alijibu kwa kifupi; “Mawaziri mizigo ndiyo tunatoka.”
Mawaziri ambao si wajumbe wa CC ni Mkuya, Chiza, Dk Kawambwa, Hawa Ghasia na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais anayeshughulikia Utawala Bora, George Mkuchika ambaye naye taarifa zilidai alihojiwa.
Azimio la Bunge
Tayari Bunge limepitisha azimio la kumtaka Ghasia pamoja na naibu mawaziri wake wawili, Aggrey Mwanry na Majaliwa Kassim Majaliwa, kupima na kutafakari kama bado wanatosha kusimamia wizara hiyo.
Kiini cha Bunge kupitisha azimio hilo ni taarifa ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali kubainisha kuwapo wizi, ubadhirifu na mtandao wa ufisadi ndani ya Tamisemi, Halmashauri na Hazina.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye baadhi ya wabunge wamemtaja kama waziri mzigo namba moja, amesema yuko tayari kuachia ngazi kama Rais ataamua kumwondoa katika wadhifa huo.
Pinda alitoa kauli hiyo juzi bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la papo kwa hapo kutoka kwa Mbunge wa Viti Maalumu, Rukia Ahmed (Cuf) aliyetaka aeleze anajisikiaje kuitwa mzigo namba moja.
Akijibu swali hilo, Pinda alisema yeye anasimamia wizara 20, hivyo kama wapo watakaomhukumu kwa sababu ya wizara moja ama mbili kutofanya vizuri basi watu hao watakuwa hawamtendei haki.
Alisema kama Rais atamwona ameshindwa kuwajibika yuko tayari kuachia ngazi na endapo Rais hatafanya hivyo na wabunge bado wakaona ipo haja hiyo, wampigie kura ya kutokuwa na imani naye.
Kauli ya CCM
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, mbele ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana, alisema kuwa mawaziri hao wameshindwa kutimiza wajibu wao wa kuwatumikia Watanzania.
Alisema kuwa Waziri Chiza na Malima wamebaki wakifunga tai na kuvaa suti mjini wakati wakulima wa Ruvuma na mikoa mingine ya Tanzania wakiteseka.
Nape alisema Waziri Kawambwa naye anatakiwa kuchukuliwa hatua kwa kuingia mkataba na kampuni ya ujenzi ya Progressive iliyopewa zabuni ya kutengeneza barabara ya Namtumbo hadi Tunduru wakati mkandarasi huyo hana uwezo wa kuijenga na matokeo yake amefukuzwa kazi.
Dk Kawambwa ametupiwa lawama hizo kutokana na kuipa kazi kampuni hiyo wakati akiwa Waziri wa Miundombinu pamoja na kushindwa kusimamia elimu.
“Katibu Mkuu (Kinana), nilimuuliza Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Chiza na Malima wamefika lini kusikiliza matatizo ya wakulima wa tumbaku, korosho na mahindi, alinijibu hakumbuki kama wamefika mkoani hapa. Nikafuatilia na kubaini si yeye tu hata Waziri aliyetangulia Profesa Jumanne Maghembe naye hakuwahi kufika. Najiuliza sababu nini, hakuna majibu,” alisema Nape.
Alisema anasikitishwa na kitendo cha mawaziri hao waliopewa dhamana kushindwa kutambua wajibu wao na kwamba umefika wakati wa kuhojiwa na Kamati Kuu (CC) ya CCM, ili wachukuliwe hatua kwani bila kufanya hivyo aibu itarudi kwa chama chake.
Wabunge wajitosa
Kikao hicho cha CC kinafanyika huku kikiwa na taarifa kwamba wabunge wa chama hicho tawala wameanza kukusanya saini za wabunge, ili kushinikiza kuitishwa kwa kikao cha wabunge hao au Party Cocas.
Uchunguzi wa gazeti hili, uliofanywa kwa siku kadhaa mjini hapa, umebaini kuwa wabunge wa CCM zaidi ya 160 wametia saini katika fomu hiyo wakiwamo mawaziri zaidi ya 10.
Chanzo kimoja cha kuaminika kilisema kuwa fomu hiyo iliwasilishwa katika ofisi ya katibu wa wabunge wa CCM, ikiambatana na barua inayotaka kuitishwa kwa kikao kitakachowakutanisha.
“Tuliwaomba waitishe kikao cha wabunge wa CCM ili mawaziri ambao tunawaona hawatimizi majukumu yao kikamilifu waweze kuhojiwa lakini wakawa wanasuasua,”kilisema chanzo hicho.
“Lakini mmoja wetu akasema kwa kuwa wamepiga chenga ya kukiitisha basi kuna nafasi ya kikanuni ya kukusanya saini za wabunge zaidi ya nusu kushinikiza kuitishwa kwa kikao,”alisema mbunge huyo.
Taarifa ya ziada na Habel Chidawali
Mbunge mwingine wa CCM alisema katika kikao hicho wabunge walitaka kukutanishwa kwa pamoja kati yao, mawaziri wanaoonekana kuwa mzigo na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
“Kikao hicho tulitaka kiwe Desemba 12 mwaka huu ili tuanze kuwahoji mawaziri kabla ya CC lakini Mwenyekiti (Mizengo Pinda), amekuwa akipiga danadana hadi leo (jana) inapokutana”alisema.
Habari zaidi zilisema baadhi ya wabunge wa CCM walikutana faragha na Kinana juzi jioni na kumtahadharisha kama mawaziri hao wasipowajibishwa, CCM kitakuwa na wakati mgumu.
Vuguvugu linaloendelea hivi sasa ndani ya wabunge wa CCM, liliwahi kujitokeza Bunge la Aprili mwaka jana na kumlazimisha Rais Kikwete kupangua Baraza lake Mawaziri Mei 4,2012.
Kung’olewa kwa mawaziri sita waliokuwa wakishinikizwa na wabunge wajiuzulu kulitokana na taarifa za kamati za kudumu za bunge na za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Katika baraza lake hilo jipya, Rais aliwatosa mawaziri waliokuwa wakishinikizwa kujiuzulu akiwemo Waziri wa Fedha, Mustafa Mkullo na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Cyril Chami.
Wengine waliotoswa kwa shinikizo hilo lililoungwa mkono na kambi ya upinzani ni wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, wa Nishati na Madini, William Ngeleja na wa Uchukuzi, Omar Nundu.
Pia Naibu Waziri wa Uchukuzi wa wakati huo, Dk Athuman Mfutakamba naye alitoswa sambamba na Waziri wa Afya, Dk Haji Hussein Mponda na Naibu wake, Dk Lucy Nkya.
Chanzo:Mwananchi