• UVCCM TAIFA

  SAUTI YA VIJANA,SAUTI YA UMMA.CCM MPYA,TANZANIA MPYA.

 • UVCCM TAIFA

  MWAKA MMOJA WA SERIKALI YA AWAMU YA TANO.

 • This is default featured slide 3 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

 • This is default featured slide 4 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

 • This is default featured slide 5 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

Ijumaa, 31 Januari 2014

MAKAMU MWENYEKITI CCM (BARA) NA KATIBU MKUU WAWASILI MBEYA TAYARI KWA SHEREHE ZA MIAKA 37 YA KUZALIWA KWA CCM


 Makamu Mwenyekiti CCM(Bara) Ndugu Phillip Mangula akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya Ndugu Godfrey Zambi wakati wa mapokezi kwenye ofisi za CCM Mkoa,Makamu Mwenyekiti amewasili mkoani Mbeya tayari kwa maadhimisho ya sherehe za miaka 37 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi .
 Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Phillip Mangula akisalimiana na Kanali Mstaafu Limbo Masanja mara baada ya kuwasili kwenye ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya.
 Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndugu Phillip Mangula akijibu baadhi ya maswali ya waandishi wa habari baada ya kuwasili kwenye ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya tayari kwa sherehe za miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM zitakazofanyika tarehe 2 Februari kwenye uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoka nje ya uwanja wa ndege wa Songwe mkoani Mbeya akiongozana na Mwenyekiti wa wilaya ya Momba Ndugu Juma Yusufu Rashid na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya Godfrey Zambi.
 Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Mbeya Dk. Mary Mwanjelwa akibadilishana mawazo na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Dogo Idd Mabrouk nje ya ofisi za CCM Mkoa wa Mbeya.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye akizungumzwa na baadhi ya waandishi wa habari waliofika mkoani Mbeya kwa ajili ya kuapata habari na matukio mbali mbali yatakayojiri wakati wa sherehe za miaka 37 ya CCM.
Bidhaa za CCM zikiwa kwenye soko sambamba na maandalizi ya sherehe za miaka 37 ya kuzzaliwa kwa CCM zinazofanyika kitaifa mkoani Mbeya.
Share:

RAIS JAKAYA KIKWETE AWAAPISHA MAWAZIRI NA MANAIBU WAZIRI IKULU DAR


 Makamu Wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri na Manaibu Waziri waliokuwa wakiapisha Ikulu Dar es Salaam, leo Jan 30, 2014 wakati alipokuwa akiwasili katika hafla hiyo. Picha na OMR
 Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Ummy Mwalimu, kuwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Waziri na Manaibu Waziri iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Jan 30, 2014. Picha na OMR
 Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha George Boniface Tuguluvala Simbachawene, kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,  wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Waziri na Manaibu Waziri iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Jan 30, 2014. Picha na OMR
 Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Kaika Saning’o Telele, kuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Waziri na Manaibu Waziri iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Jan 30, 2014. Picha na OMR
 Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Eng. Dr. Binilith Satano Mahenge, kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Waziri na Manaibu Waziri iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Jan 30, 2014. Picha na OMR
 Rais Jakaya Kikwete, Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakia katika picha ya pamoja na Waziri na Manaibu Waziri walioapishwa katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Dar es Salaam, leo Jan 30, 2014. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri wapya na wa zamani wa Ofisi yake, baada ya kuapishwa wapya katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo. Kutoka (kulia) ni aliyekuwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Charles Muhangwa Kitwanga, ambaye kwa sasa ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano)Samia Suluhu Hassan, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Eng. Dr. Binilith Satano Mahenge, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Ummy Mwalimu na aliyekuwa Waziri wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Terezya Huvisa, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha Waziri na Manaibu Waziri, iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Jan 30, 2014. Picha na OMR

Share:

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKUTANA NA MAWAZIRI WA KATIBA NA SHERIA, SAYANSI NA ELIMU, IKULU DAR

 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Asha-Rose Migiro, wakati alipofika Ofisini kwake kwa Makamu Ikulu Dar es Salaam, leo Jan 30, 2014 kwa mazungumzo. Picha na OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwakaribisha Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof Makame Mbarawa (katikati) wakati walipofika Ofisini kwake kwa Makamu Ikulu Dar es Salaam, leo Jan 30, 2014 kwa mazungumzo. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof Makame Mbarawa (katikati) wakati walipofika Ofisini kwake kwa Makamu Ikulu Dar es Salaam, leo Jan 30, 2014 kwa mazungumzo. Picha na OMR
Share:

Jumatano, 29 Januari 2014

WAZIRI MKUCHIKA AENDELEZA SABABU ZA TANZANIA KUSHUKA VUWABNGO VYA UTAWALA BORA DUNIANI


MOSHI, Tanzania
WAZIRI wa Nchi ofisi ya Rais anayeshuhulikia Utawala Bora, Kaptein mstaafu, George Mkuchika amesema migogoro ya ardhi, mauaji ya maalbino na vikongwe, wanachi kujichukulia sheria mikononi, rushwa pamoja na ujangili zinadaiwa kuwa moja ya sababu zinazochangia kuporomoka kwa Tanzania katika viwango vya utawala bora duniani.

Mkuchika aliyasema hayo alipokuwa akizungumza katika kikao cha 30 cha kamati ya ushauri wa mkoa wa Kilimanjaro (RCC) kikao ambacho ni cha kwanza kwa mwaka 2014 na maalum kwa ajili ya kujadili vipauumbele vya Bajeti ya Mkoa huo kwa mwaka 2014/2015.

Kaptein Mkuchika alisema kutokana na taarifa zilizotolewa hivi karibuni, Tanzania inashika nafasi ya pili kwa utawala bora nyuma ya Rwanda kwa nchi za ukanda wa Afrika mashariki nyuma ya Rwanda, 17 katika ukanda wa Afrika na 102  kati ya nchi 176  duniani ambapo kwa mujibu wa taarifa hizo Tanzania imeshuka kiwango katika ukanda wa Afrika katika kipindi cha miaka miwili.

Alisema katika taarifa hizo, Tanzania ilikuwa ikishika nafasi ya 10 miaka miwili iliyopita na kuongeza kuwa kuporomoka huko kunatokana na kukithiri kwa ukiukwaji wa haki za binadamu, mauaji ya albino na vikongwe, mapigano ya wakulima na wafugaji, Ujangili, ambapo zaidi ya watu kumi walikufa mkoani Manyara.

 “tukiangalia kiundani Matukio haya yamesababisha kwa kiasi kikubwa Tanzania kuporomoka katika viwango vya utawala bora, miaka miwili iliyopita, tulikuwa wa 10 katika bara la Afrika, Afrika mashariki tunashika nafasi ya 2, duniani tuko nafasi ya 102 kati ya nchi 176, kukithiri kwa matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu, mauaji ya albino na vikongwe, mapigano ya wakulima na wafugaji, Ujangili, zaidi ya watu kumi walikufa mkoani Manyara,” alisema Mkuchika.

Kuhusu swala la Rushwa, Mkuchika alisema tatizo hilo haliwezi kumalizwa endapo wananchi wenyewe hawatabadili tabia yao kwani uzoefu unaonesha kuwa asilimia kubwa ya Rushwa ndogo hutokana na Wananchi wenyewe.

Alisema katika swala la Rushwa, kamati za ushauri za mikoa na mabaraza ya Halmashauri zina nafasi kubwa kufanikisha vita na mapambano dhidi ya vitendo hivyo kutokana na kuhusika kwao katika maamuzi mengi yanayohusu maendeleo ya mikoa na Halmashauri zao.

“kweli kwa kiasi kikubwa kamati ya ushauri ya mkoa, mabaraza ya madiwani zina nafasi kubwa ya kupunguza tatizo la rushwa katika Halmashauri na mikoa yao, endapo watu hawa watabadilika hasa katika maamuzi wanayoyachukua katika shughuli na vikao vyao,” alisema

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama aliwataka watendaji katika halmashauri zote za wilaya hiyo kutekeleza agizo la kutenga mgao wa asilimia 15 kwa ajili ya makundi maalum ambayo ni asilimia 5 kwa ajili ya vijana asilimia 5 ya wanawake na asilimia5 kwa ajili ya vita dhidi ya mapambano ya  Ukimwi ambapo alisema mkoa haitasita kuichukulia hatua Halmashauri itakayoshindwa kutekjeleza agizo hilo.

“kila halmashauri inatakiwa kutenga fedha kwa ajili ya makundi maalumu ambapo , asilimia 5 kwa vijana, tano kwa wanawake na asilimia 5 kwa ajili ya mapambano dhidi ya vita ya Ukimwi, na halmashauri itakayoshindwa kutekeleza itachukuliwa hatua kali,” alisema.
Share:

Jumanne, 28 Januari 2014

TAMKO LA JUMUIYA YA VIJANA KUUNGA MKONO KAZI YA SEKRETARIETI YA CHAMA CHA MAPINDUZI CHINI YA KATIBU MKUU NDUGU ABDULRAHAMAN KINANA.

TAMKO LA JUMUIYA YA VIJANA KUUNGA MKONO KAZI YA SEKRETARIETI YA CHAMA CHA MAPINDUZI CHINI YA KATIBU MKUU NDUGU ABDULRAHAMAN KINANA.

“..Chama Cha Siasa chochote duniani hubomoka kutokana na migongano iliyokithiri ya muda mrefu. Uzoefu wa vyama vikubwa vilivyoporomoka umeonyesha hivyo! Chama lazima kidhibiti uchu wa madaraka wa baadhi ya viongozi wake na ndani ya serikali yake...” – Dr Eginald P. Mihanjo

“..Chama cha siasa ni itikadi. Chama cha siasa ni siasa kwa maana halisi ya neno lenyewe siasa –“siasa”. Ni mahali ambapo watu wenye madhumuni mamoja yaliyoainishwa waziwazi hukutana na kuwa kitu kimoja. Chama cha siasa sio mkusanyiko wa “majini dume yenye tamaa”, - majini ambayo yametanguliza mbele tamaa kufa na kupona-tamaa ya kutengeneza pesa au kupata vyeo kwa gharama yoyote! – Dr Bashir Ally

UTANGULIZI:

Hili ni tamko la vijana makini wa jumuiya ya umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) kuunga mkono juhudi na utendaji wa sekretarieti ya halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi ikiongozwa na Katibu Mkuu Komredi Abdulrahaman Kinana.

Maneno ya utangulizi yamebeba dhima ya tamko hili, kufuatia taarifa zilizoripotiwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari vikiwanukuu baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi, wakiwatuhumu Viongozi wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM, Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahaman Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Moses Nnauye.

Sisi Vijana tunatambua kuwa tuhuma hizo na maneno hayo ya hovyo yametolewa kwa nia ovu yenye kulenga kuwakatisha tamaa Viongozi hao wa Chama. Tunafahamu kuwa upo mkakati wa kiuhaini ulioandaliwa na kuratibiwa na “mtandao” ndani ya Chama ambao umejipanga kuendesha uhaini huo.

Sisi vijana wa UVCCM tunatambua na kuthamini juhudi za Katibu Mkuu na Sekretarieti yake katika kukijenga na kukiimarisha Chama kwa kuisimamia barabara misingi na shabaha ya kuundwa kwake, katika umri wetu hatukuwahi kuona Chama kikiwa karibu na wananchi kwa kufuatilia, kusikiliza na kushiriki katika utatuzi wa kero, shida na changamoto zao kama ilivyo katika kipindi hiki chini ya Comrade Kinana na timu yake. Juhudi hizi ni za kuungwa mkono na kamwe si za kubezwa na mwanaCCM muadilifu, muaminifu na mwenye mapenzi ya kweli kwa Chama.

Juhudi za kukiimarisha Chama kutoka ngazi za chini, kwa mabalozi ni mkakati bora kuwahi kutekelezwa na Chama, kukirudisha Chama kwa wanachama ni kutimiza lengo la kuundwa kwa Chama hiki, Chama hiki ni cha wanyonge, masikini wa Taifa hili, HAIWEZEKANI matajiri watake kukihodhi na waratibu mikakati ya kukihujumu kwa pesa zao hali sisi vijana tukitazama, tunasema tutakilinda Chama chetu na tutawalinda viongozi wetu waadilifu.

Ni hawa ambao wanabezwa leo ndio wameweza kurudisha Imani ya wananchi kwa Chama, Imani na matumaini ambayo tayari yalishaanza kupotea na Chama kuonekana si tena cha wanyonge, wakulima na wafanyakazi wan chi hii.

Ni Comrade Kinana na timu yake ndio waliozunguka kwenda kukutana na wakulima wa Pamba kule mikoa ya Kanda ya ziwa na kumpeleka balozi wa China na kumshawishi kujenga viwanda ili kuboresha manufaa kwa wakulima.

Ni Comrade Kinana na timu yake ndio waliokwenda Kusini kukutana na wakulima wa Korosho na kushirikiana nao pamoja na bodi kutatua tatizo la Korosho.

Ni Comrade Kinana na timu yake ndio walioibua hoja na kero za wafugaji, walimu na wananchi kwa ujumla, na kuwataka viongozi wa Serikali kuhakikisha wanawajibika kwa wananchi walipa kodi wa Taifa hili.

Kupinga mafanikio ya Ziara hizo ni kupinga utetezi wa wanyonge.

Mtu anayebeza ziara hizo na kuwaita Viongozi waliozifanya waropokaji na wahuni wahuni ni mtu mjinga, mtu wa hovyo,hana maadili, asiyekipenda Chama, mhaini na mzandiki anayepaswa kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu ili iwe fundisho kwa wengine.

TAMKO hili limezingatia wosia wa Baba wa Taifa, muasisi wa Chama Cha Mapinduzi Mwl Julius Kambarage Nyerere katika kitabu Chake TUJISAHIHISHE.

“Inapofikia wasimamizi wa Kanuni za Chama wanapigwa vita ya wazi kwa uamuzi wao wa kukisimamia Chama, tafsir yake ni moja tu watu wanaowapiga vita hawakitakii mema chama chetu.”

Imetolewa na Paul Christian Makonda.

Katibu wa Hamasa na Chipukizi.
Share:

RAIS KIKWETE AKAGUA DARAJA LILILOVUNJIKA MOROGORO

Helkopta iliyokuja na Rais Kikwete ikitua eneo la daraja la Dumila mkoani Morogoro leo.
Rais Kikwete akishuka katika helkopta aliyokuja nayo.
Rais JK akielekea kukagua daraja la Dumila lililokatika kutokana na mvua kubwa iliyonyesha eneo hilo.
Rais Kikwete akikagua daraja hilo.
Rais Kikwete akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Magole mkoani Morogoro waliokumbwa na mafuriko ambao kwa sasa wanaishi katika mahema yaliyopo Shule ya Sekondari Magole.
Rais Kikwete akisalimiana na bibi mmoja wa kijiji cha Magole.
Rais Kikwete akiingia katika mojawapo ya hema.
...Akitafakari jambo.
Wananchi wa Magole waliokumbwa na mafuriko.
Rais Kikwete (kushoto) akijadiliana jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge William Lukuvi.
Rais Kikwete akiongea na wakazi wa Magole leo.
Wananchi wa Magole wakiwa nje ya mahema yao.
RAIS Dk. Jakaya Kikwete leo ametua kwa helikopta kijijini Magole, Dumila ili kukagua daraja lililoharibiwa na mvua pamoja na kuongea na wananchi wa eneo hilo waliokumbwa na mafuriko yaliyotokea Januari 22, mwaka huu wilayani Mvomero, Morogoro.
Share:

Jumatatu, 27 Januari 2014

DR. SHEIN AMNADI RASMI MGOMBEA WA CCM JIMBO LA KIEMBESAMAKI, MAHMOUD LOMBO


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Katibu Mkuu wa CCM Taifa Abdulrahman Kinana,wakati alipowasili katika viwanja vya Mpira Kiembesamaki katika Mkutano wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM,sambamba na kumnadi Mgombea wa CCM wa uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo leo
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na vijana Chipukizi wakati mapokezi alipowasili viwanja vya Mpira Kiembesamaki katika Mkutano wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM,sambamba na kumnadi Mgombea wa CCM wa Uwakilishi  Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo leo
R ais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akivalishwa Skafu  na vijana Chipukizi wakati mapokezi alipowasili viwanja vya Mpira Kiembesamaki katika Mkutano wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM,sambamba na kumnadi Mgombea wa CCM wa uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo leo
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na  Katibu Mkuu wa CCM Taifa Abdulrahman Kinana,wakati alipowasili katika viwanja vya Mpira Kiembesamaki katika Mkutano wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM,sambamba na kumnadi Mgombea wa CCM wa uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo leo. Katibu Mkuu wa CCM Taifa Abdulrahman Kinana,alipkuwa akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein kuzungumza na wananchi na wanachama wa CCM  katika Mkutano wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM,sambamba na kumnadi Mgombea wa uwakilishi wa  CCM Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo leo,  katika uwanja mpira  Kiembesamaki palipofanyika mkutano huo. 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akimnadi na kumuombea kura kwa wanaCCM na Wananchi, Mgombea wa  CCM wa uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo leo,katika Mkutano wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM katika viwanja vya mpira Kiembesamaki
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akizungumza na wananchi na wanachama wa CCM  katika Mkutano wa maadhimisho ya miaka 37 ya kuzaliwa kwa CCM,sambamba na kumnadi Mgombea wa CCM Jimbo la Kiembesamaki Mahmoud Thabit Kombo leo, katika uwanja mpira  Kiembesamaki palipofanyika mkutano huo.Picha na Ramadhan Othman,IKULU-Zanzibar
Share:

MWANDISHI WA HABARI LEO KILIMANJARO, ARNOLD SWAI, MWENYEKITI MPYA UVCCM WILAYA YA HAI


Arnold Swai (wa kwanza kushoto)wakati wa upigaji kura, zoezi lilofanyika juzi, wilayani Hai kuziba pengo la nafasi ya Mwenyekiti
Mjumbe wa Halmshauri kuu CCM wilaya ya Hai, Fuya Kimbita, akizungumza katika zoezi la kupiga kura lililoshuhudia Mwandishi wa Habari Leo, Arnold Swai akiibuka kidedea.
Arnold Swai akihutubia baada ya kutangazwa Mwenyekiti Mpya kwa kushinda uchaguzi uliofanyika juzi. Swai alipata kura 151 kati ya kura 222 zilizopigwa
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Kilimanjaro, Fredy Mushi, akizungumza na wanajumuiya hiyo muda mfupi kabala ya uchaguzi ulioshuhudia ushindi wa kishindo wa Mwandishi wa Habari Leo, Arnold Swai kuwa Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Hai.
Share:

SERIKALI YATOA TAMKO KUHUSU KUSITISHA UTARATIBU WA KUKODISHA WAFANYAKAZI UNAOFANYWA NA BAADHI YA WAKALA BINAFSI WA HUDUMA ZA AJIRA


Waziri wa Kazi na Ajira Bi.Gaudentia Kabaka akitoa tamko la Serikali kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya usitishwaji wa utaratibu wa kukodisha wafanyakazi unaofanywa na baadhi ya mawakala binafsi wa huduma za ajira wakati wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa idara ya habari (MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam.
*****************************
TAMKO LENYEWE HILI HAPA
1. Wizara ya Kazi na Ajira imekua ikipokea malalamiko  toka kwa wadau mbalimbali kuhusu taratibu wa udalali wa kukodisha wafanyakazi katika makampuni unaofanywa na baadhi ya Wakala Binafsi wa Huduma za Ajira nchini.

2. Wizara imefanya uchunguzi wa kina kuhusu suala hili na kubaini kuwa utaratibu wa kukodisha wafanyakazi unaofanywa na baadhi ya Wakala Binafsi wa Huduma za Ajira ni kinyume cha Sheria ya Huduma za Ajira Na. 9 ya Mwaka 1999  (Sura 243 kama ilivyorejewa Mwaka 2002). Kwa mujibu wa Kifungu 4 cha Sheria hii, majukumu ya msingi ya Wakala wa Huduma za Ajira ni kuwaandaa na kuwaunganisha Watafuta Kazi na Waajiri kwa kutoa mafunzo na  ushauri elekezi kwa watafuta kazi,  kutafuta fursa za ajira na kutoa taarifa za soko la ajira.  Hivyo, Mawakala hawapaswi kuwa waajiri wa wafanyakazi waliowatafutia kazi kwa niaba ya Waajiri wengine.

3. Aidha, uchunguzi umebaini kwamba  utaratibu huu ni ujanja unaotumiwa na baadhi ya Waajiri na Mawakala kwa lengo la kukwepa kodi na kujipatia faida kwa kukwepa kutoa haki za msingi za wafanyakazi kwa mujibu wa Sheria za Kazi. Baadhi ya makampuni yanayokodisha wafanyakazi yamefanyiwa uhakiki na TRA na kubainika kukwepa kodi ya mapato ya ajira (PAYE) na  na kodi ya mapato ya kampuni kinyume na Kifungu cha 7 cha Sheria ya Kodi ya Mapato ya Mwaka 2004 (Sura 332 kama ilivyorejewa Mwaka 2008).

4. Uchunguzi huu umebaini  athari mbalimbali kwa wafanyakazi wanaoajiriwa kwa utaratibu huu. Athari hizo ni pamoja na:
· Wafanyakazi kukosa haki ya hifadhi ya jamii kama vile likizo ya uzazi na matibabu kinyume na Sheria mbalimbali za Mifuko ya Hifadhi ya Jamii;
· Uwepo wa ubaguzi katika malipo ya mishahara kwa kazi ya aina moja kinyume  na  kifungu cha 7(10) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini Na.6 ya mwaka 2004 ambacho kinamtaka mwajiri kuchukua hatua stahiki kwa kuhakikisha kuwa wafanyakazi bila kujali jinsia zao wanalipwa mishahara linganifu na ya haki kwa kazi yenye uzito na thamani sawa;
· Kukosa fursa za kujiendeleza kielimu na mafunzo;
· Kukosekana kwa usalama na uhakika wa ajira ;
· Wafanyakazi kulipwa mishahara ya kima cha chini kinyume na sekta wanayofanyia kazi.

5. Kwa taarifa hii, Wizara ya Kazi na Ajira imeamua kusitisha mara moja utaratibu wa Mawakala kuwaajiri  wafanyakazi wanaowatafutia kazi.  Aidha, Mawakala na Kampuni husika waliopo katika utaratibu huu kwa sasa wanapaswa kuwahamisha  wafanyakazi waliokodishwa kutoka kwa Wakala kwenda  kwa Kampuni husika. Waajiri na Wakala wanatakiwa kukamilisha zoezi hili ndani ya kipindi cha mwezi mmoja na kuwasilisha taarifa za utekelezaji kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Kazi na Ajira kabla au ifikapo tarehe 28/02/2014.

6. Uchunguzi zaidi unaendelea kubaini kama kuna wafanyakazi wa Kigeni wanaohusishwa katika utaratibu wa kukodishwa ili hatua zinazotahili ziweze kuchukuliwa ikiwa ni pamoja na kuwataka waombe vibali vya ajira kwa mujibu wa Sheria ya Uhamiaji Na.7 ya mwaka 1995 na Sheria ya Huduma za Ajira Na.9 ya mwaka 1999. Wageni watakao kidhi vigezo wataajiriwa na kampuni walipokodishwa; ambazo kwa wakati huo zitakua ndiyo mwajiri wao.

7. Wizara ya Kazi na Ajira inawaelekeza Wakala wa Huduma za Ajira nchini kwamba, kwa utaratibu wa sasa watapaswa kuwasilisha barua za maombi ya  usajili wa Uwakala kwa KAMISHNA WA KAZI  kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Ajira Na. 9 ya mwaka 1999 [Sura 243 kama ilivyorejewa Mwaka 2002] ili waweze kufanya shughuli za Uwakala wa Huduma za Ajira kisheria. Maombi haya yawasilishwe ndani ya kipindi cha mwezi mmoja tangu kutolewa kwa tangazo hili. Baada ya muda huo Wakala asiye na kibali cha Kamishna wa Kazi hatoruhusiwa kuendesha shuguli za huduma za ajira nchini. Aidha, Mawakala watakaopata leseni ya Kamishna wa Kazi yatakua yakitangazwa ili yatambuliwe na Umma.

8. Nasisitiza, maelekezo haya yatatolewa kwa Makampuni na Wakala  waliohusishwa katika uchunguzi kwa ajili ya utekelezaji.

IMETOLEWA NA
GAUDENTIA MUGOSI KABAKA (MB)
WAZIRI WA KAZI NA AJIRA
27/01/2014se
Share:

Jumamosi, 25 Januari 2014

VIKUNDI VYA VICOBA VILIYOPO CHINI YA POVERTY FIGHTING TANZANIA(PFT) INAYOSIMAMIWA NA MBUNGE WA TEMEKE ABBAS MTEMVU VYAKABODHIWA VIFAA VYA MILLIONI 192.3


*NI GARI SITA AINA YA SUZUKI CARRY,  *BAJAJ KUMI, *PIKIPIKI 19 AINA YA BOXER, *PIKIPIKI YA MZIGO AINA YA TOYO, *VIFAA VYA UMEME VYA USEREMALA, *MBAO, *VIFAA VYA STATIORIES NA VIFAA VYA SHOOTING CAMERA
Vifaa vikiwa tayari kukabidhiwa kwa vikundi hivyo vya Vicoba chini ya PFT
 Baadhi ya sare zilizovaliwa na wadau zilikuwa na ujumbe huu
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwezeshaji na Uwekezaji. Dk. Mary Nagu (kushoto) akiwasili ukumbini huku akiwa na Mwenyekiti wa PFT, Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu, kwa ajili ya kuvigawia vifaa mbalimbali  vikundi 130 vya Vikoba vilivyo chini ya Taasisi ya PFT katika hafla iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa PTA, Sabasaba, Dar es Salaam
 Mwenyekiti wa PFT, Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu akimtambulisha kwa waziri Nangu, Mwezeshaji wa VICOBA walioko chini ya PFTJohannes Linde wakati waziri Nagu alipowasili ukumbini.
 Wanavikundi wakilipuka kwa shamrashamra wakati wa mapokezi ya waziri Nagu ukumbini
 Cherekochereko na mabango
 Kina mama wa Vicoba wakifurahi
 Mama Mtemvu na Mwanae wakiwa kwenye hafla hiyo
 Wanachama wa Vicoba wakiwa wamekaa baada ya mapokezi
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Juma Kassim 'Juma Nature' akitumbuiza wakati wa hafla hiyo.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Juma Kassim 'Juma Nature' akitumbuiza kwenye hafla hiyo
 Msanii Snura Mushi maarufu kwa jila na Majanga, akikonga nyoyo za wanavicoba wakati wa hafla hiyo
 Snura Majanga akionyesha umahiri wake mbele ya wana-Vicoba
 Mwenyekiti wa PFT, Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu akimkabidhi Waziri Nagu hati maalum ya shukrani kwenda kwa Rais Jakaya Kikwete kutokana na mchango alioutoa wa sh. milioni 50 kwa PFT. Kushoto ni Naibu Waziri wa Maendeleo na Jamii Jinsia na Watoto Pindi Chana.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezaji). Dk. Mary Nagu (katikati) akikabidhi pikipiki kwa moja ya vikundi 130 vya Vikoba vilivyo chini ya Taasisi ya PFT katika hafla ya kuviongezea uwezo kwenye Ukumbi wa PTA, Sabasaba, Dar es Salaam leo. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Temeke, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Abbas Mtemvu.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezaji). Dk. Mary Nagu (katikati) akikabidhi gari kwa moja wa viongozi wa PFT.
Masiriamali ambaye ni mwanachama wa moja ya vikundi cya Vicoba vilivyopo chini ya PFT akiwa kazini wakati wa hafla hiyo
 Wanachama wa Vicoba wakichangamkia fomu za NSSF za Matibabu
 Wanakikundi cha Vicoba wakiwa kwenye gari lao baada ya kukabidhiwa
 Mweneyekiti wa PFT, Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu akizungumza na waandishi wakati wa hafla hiyo
Mtembu akiwa na Kina Juma Nature na Snura Majanga ambao walitumbuiza kwenye hafla hiyo. KUPATA MAELEZO KAMILI KUHUSU HAFLA HIYO NA PFT>

 

Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Gadget

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu