• UVCCM TAIFA

  SAUTI YA VIJANA,SAUTI YA UMMA.CCM MPYA,TANZANIA MPYA.

 • UVCCM TAIFA

  MWAKA MMOJA WA SERIKALI YA AWAMU YA TANO.

 • This is default featured slide 3 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

 • This is default featured slide 4 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

 • This is default featured slide 5 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

Ijumaa, 28 Februari 2014

MWIGULU NCHEMBA ALIVYOZINDUA KWA KISHINDO KAMPENI ZA CCM KALENGA


 Abdul Adam, Mtoto wa Spika wa Bunge wa zamani Chifu Adamu Sapi Mkwawa, akimpongeza mgombea wa CCM katika Uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, Iringa Vijijini, Godfrey Mgimwa, wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa kampeni za CCM uliofanyika Viwanja vya Ifunda, Februari 27, 2014.

 Wananchi wakinyoosha mikono kuunga mkono kuwa mgombea wa CCM anafaa, wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa kampeni za CCM uliofanyika Viwanja vya Ifunda, Februari 27, 2014.

 Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Mwigulu Nchemba akionyesha makada wa CCM,  Alphonce John (kushoto) na Musa Tesha, walionusurika kuuawa na watu wanaodaiwa kutumwa na Chadema kwa mmoja kumwagiwa tindikali na mwingine kutobolewa jicho kwenye kampeni zinazohusu udiwani na Ubunge, katika maeneo ya Igunga na Kahama, alipokuwa akieleza fuji za Chadema, wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa kampeni za CCM uliofanyika Viwanja vya Ifunda, Februari 27, 2014.

  Alfonce aliyetobolewa jicho Kahama akizungumza jukwaani.

  Mwigulu akihutubia, wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa kampeni za CCM uliofanyika Viwanja vya Ifunda, Februari 27, 2014.


 Mwigulu (4th) na mgombea wakitroti na Green Guard, wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa kampeni za CCM uliofanyika Viwanja vya Ifunda, Februari 27, 2014.

 Katibu wa CCM, wilaya ya Mufindi, Miraji Mtaturu, alionyesha mbao zenye misumari inayodaiwa kutegwa njiani na Chadema, kwa nia ya kudhuru msafara wa mgombea wa CCM katika jimbo la Kalenga.

 Katibu wa CCM  mkoa wa Iringa, akishauriana jambo na Mwenyekiti wake Joyce Msavatavangu

 Mjumbe Kamati Kuu ya CCM, Pindi Chana,  akitema cheche jukwaani, wakati wa mkutano wa uzinduzi rasmi wa kampeni za CCM uliofanyika Viwanja vya Ifunda, Februari 27, 2014.

Godfrey Mgimwa-Mgombea wa CCM uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, Iringa.
Imetayarishwa na theNkoromo Blog
Share:

Jumanne, 25 Februari 2014

TANZANIA YASITIZA NYONGEZA YA POSHO KWA WALINZI WA AMANI WA UMOJA WA MATAIFA


Na Mwandishi Maalum, New York
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  imesema, posho ya dola 1.28  kwa siku wanayolipwa walinzi wa amani wanaohudumu katika Misheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa,  hailingani na  mazingira magumu  na hatari ya utekelezaji wa mamlaka wanayokabidhiwa na Umoja wa Mataifa. 
        Na kwa sababu hiyo ,na kwa zingatia hali halisi,  Tanzania  imesisiza kwamba,  wakati umefika sasa wa kuangalia upya posho hiyo ambayo imedumu kwa zaidi ya miaka 20.
       Balozi Tuvako Manongi, Muwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania katika Umoja wa mataifa,  ametoa rai hiyo  mwanzo mwa  mkutano wa Kamati   Maalum  ya      Usimamizi wa  Operesheni za Ulinzi wa    Amani maarufu kama C-34.
       Kamati hii ambayo wajumbe wake ni kutoka nchi zinazochangia walinzi wa Amani katika misheni mbalimbali za kulinda  amani,  imeanza mkutano wake wa  mwezi mmoja hapa  Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa ambapo  wajumbe watajadili  mambo yote yanayohusu sera za ulinzi wa Amani  chini ya Umoja wa Mataifa.
       Balozi Manongi amewaeleza wajumbe wa mkutano huo  kwamba   Kamati   ilikuwa inaanza mkutano wake,  wakati ambapo ,  operesheni za ulinzi wa amani  zinakabiliwa na  changamoto mbalimbali zikiwamo za malipo duni.
      “ Tunaposhindwa kukubaliana kujadili hoja ya  kuongeza kiwango cha posho ya kila siku kwa walinzi wa amani,  posho  ambayo  imebaki  dola 1.28 kwa zaidi ya miaka 20, siyo tu kwamba tumewaangusha walinzi wa amani,  bali pia tunawavunja moyo na kuwakatisha tamaa katika utekelezaji wa majukumu yao”. akasisitiza Balozi  Manongi.
       Akasema waeleza wajumbe    licha ya  malipo duni na mazingira magumu, walinzi hao wanajitolea uhai wao kwaajili  ya watu wengine na kwamba,kutokana  umuhimu wao , Umoja wa Mataifa  umejikuta  ukilazimika kuwapeleka katika Misheni ambazo ama hakuna amani ya kulinda au  mahali ambako kuna  vikundi vingi vyenye silaha vinavyokinzana.
      “Hii ndiyo hali halisi inayozikabili Misheni zetu zote  katika  utekelezi wa mamlaka  tunazokabidhiwa na Umoja wa Mataifa. Inasikitisha  na kukatisha tamaa pale baadhi yetu tunaposisitiza kwamba Misheni mpya inayoundwa au kuongezewa mamlaka itekeleze mamlaka hayo kwa kuzingatia rasilimali zilizopo, ili hali tunafahamu wazi kwamba rasilimali zinazozungumzwa  ama hazipo au hazikidhi hali halisi ya  Misheni hizo”. Akabainisha Balozi Manongi.
      Na kuongeza. “Ni vema tukaunganisha nguvu zetu kukabiliana na  changamoto hizi na nyingine nyingi ili  walinzi wa amani  ambao wanategemewa  sana waweze kusaidia katika ulinzi wa amani kwa raia wasiokuwa na hatia, lakini pia  kujihakikishia usalama wao wenyewe.

       Akaeleza kwamba  ni matumaini ya Tanzania kuwa  hoja ya  kuongezwa kwa posho  hiyo   pamoja na nyongeza ya  malipo ya vifaa itapewa umuhimu na kujadiliwa ipasavyo katika mkutano ujao wa Kamati ya Tano ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa inayohusika na masuala ya   Utawala na Bajeti ya Umoja wa Mataifa.
       Pamoja na  changamoto hizo,  Muwakilishi  huyo wa Tanzania, ameuhakikishia  Umoja wa Mataifa  kwamba,  Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kuwajibika kwa kushiriki katika operesheni za ulinzi wa Amani  kwa  mujibu wa Mamlaka inayokabidhiwa na  Umoja wa Mataifa.
       “ Tumedhamiria na tunajivunia ushiriki wetu wa ulinzi wa Amani katika  maeneo mbalimbali ikiwamo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambako  tunashiriki  kupitia Misheni ya Kulinda Amani katika DRC ( MONUSCO). Misheni ambayo ndani yake  kuna  Force  Intervention Brigade ( FIB)”.
      Vile vile  akabainisha kwamba  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  itaendelea  kushiriki kikamilifu katika  utekelezaji wa  Mpango  Mpana wa Kisiasa wa Umoja wa Mataifa, kuhusu Ulinzi, Usalama na   Ushirikiano wa  Ki- maendeleo katika DRC na  eneo la  Maziwa Makuu.

        Akizungumzia  zaidi kuhusu Misheni  ya MONUSCO na mchango wake katika  usimamizi wa amani  katika DRC.
        Balozi Tuvako Manongi amesema, Tanzania inaamini   kwamba utendaji kazi wa Misheni hiyo  unasimama katika  misingi ya  Misheni Moja,  Jeshi Moja,  Nguvu  Moja ya Mamlaka,  kuwa  ndiyo  mweleko sahihi na wenye tija  katika ngazi zote  kiutendaji.
        Misheni ya MONUSCO  inaundwa na walinzi wa Amani  kwa upande mmoja kutoka Pakistani, India na  Bangladeshi pamoja na  Tanzania,  Afrika ya Kusini na Malawi kupitia FIB.

        Aidha,   Muwakilishi wa  Tanzania katika Umoja wa Mataifa,  amezitaka Mamlaka za Jamhuri ya  Kidemokrasia ya Kongo,  kutumia  mafanikio yaliyopatikana hivi karibuni, kuimarisha  taasisi zake za  kisiasa, kiulinzi , kiuchumi   pamoja na kuongeza kasi ya  majadiliano na  maridhiano. Baadhi ya  Waambata wa Kijeshi wanaoziwakilisha nchi zao Katika Umoja wa Mataifa, wakiwa  katika  picha ya pamoja muda mfupi kabla ya  ufunguzi wa Mkutano wa Mwezi mmoja wa Kamati Maalum ya Usimamizi wa Operesheni za Kulinda  Amani.    Katika Mkutano huu wajumbe ambazo ni kutoka  nchi ambazo zinachangia walinzi wa amani watajadili sera zote zinazohusu ulinzi wa amani chini  ya  Umoja wa Mataifa.
Share:

Monday, February 24, 2014

Dar es Salaam, Tanzania
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu leo ametangaza kuwang'oa viongogo wa ngazi ya juu katika Idara ya wanyamapori akieleza kuwa ni kutokana na kutoridhishwa na utendaji wao.
Ifuatayo ni Taarifa rasmi ya tamko la Waziri Nyalndu,  kama alivyolisoma leo na CCM Blog kupata nakala ya tamko hilo

Leo, TAREHE 24 Februari, 2014 Natangaza kuubadili uongozi wa Idara ya Wanyamapori ya Wizara ya Maliasili na Utalii kama ifuatavyo:

Ninamuondoa Profesa Alexander Songorwa katika nafasi ya Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori ya Wizara ya Maliasili na Utalii.  Nachukua hatua hii kutokana na kutokuridhishwa kwangu na utendaji wa kazi wa idara hiyo katika mapambano dhidi ya ujangili yanayoendelea nchini.  Aidha, hatua hii ni utekelezaji wa Azimio la Bunge lililotolewa tarehe 22 Disemba, 2013, lililotaka Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori kuwajibishwa kutokana na tuhuma za uzembe na ukiukwaji wa haki za binadamu katika Operesheni Tokomeza.

Utekelezaji wa agizo hili unaanza mara moja, nami namteua Bwana Paul Sarakilya kukaimu nafasi hiyo ya Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori ya Wziara ya Maliasili na Utalii kuanzia sasa.

Aidha, ninamuondoka Profesa Jafari Kidegesho katika nafasi ya Mkurugenzi Msaidizi wa Matumizi Endelevu ya Wanyamapori na kumteua Dr. Charles Mulokozi kuchukua nafasi hiyo.

Hali kadhalika, ninamteua Bwana Julius Kibebe kuwa Mkurugenzi Msaidizi Uzuiaji – Ujangili na anachukua nafasi ya anayeenda kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Wanyamapori.

Vilevile, Bibi Nebbo Mwina anaendelea kuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Mafunzo, Utafiti na Takwimu, na Bwana Herman Keiraryo anaendelea kuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Uendelezaji wa Wanyamapori. Pamoja na Kitengo cha Uzuiaji – Ujangili nilichokitaja awali, hivi ni vitengo vya Idara ya Wanyamapori katika Wizara ya Maliasili na Utafiti.

Nawaagiza kwamba Wakurugenzi na Wakuu wote wa kila Idara, kila Shirika, na Taasisi zote ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii kutengeneza viashiria muhimu vya utendaji kazi (Key Performance Indicators) nakukabidhi kwangu ndani ya siku 30 zijazo.  Viashiria hivi ni hatua ya kufanikisha yafuatavyo, 1)  Malengo ya wizara, 2)  Uwajibikaji, 3) Uwazina 4) Ufanisi katika utendaji wa kazi za kila siku.  Ni sharti tutekeleze mikakati ya wizara katika mifumo inayopimika, tuweze kujipima natuweze kupimwa, natutumikie Taifa kwa uadilifu.

Kwa mtumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii ikiwemo mimi mwenyewe, Lazaro Nyalandu, atapaswa kuzingatia na kutekeleza majukumu ya kazi kwa kuzingatia Kanuni za Mwenendo (Code of Conduct) ambazo zitapendekezwa na kupitishwa na Baraza la Wafanyakazi wa Wizara.  Baraza hili liwe limeitishwa na Katibu Mkuu wa Wizara kabla ya mwisho ya mwezi ujao.  Azma ya kanuni hizi ni kuwa na misingi bora ya utumishi, uwajibikaji, utu, usawa na haki katika utekelezaji wa majukumu yetu ya kila siku.

 
Mungu ibariki Tanzania.

Asante.
 
Lazaro S. Nyalandu (MB)
Wizara ya Maliasili na Utalii
24/02/2014
Share:

Jumamosi, 22 Februari 2014

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE HAYA HAPA

Share:

Ijumaa, 21 Februari 2014

Paul Makonda mjumbe wa Bunge la Katiba afunguka kuhusu tuhuma za kudai Posho.

MJUMBE WA BUNGE LA KATIBA PAUL
MAKONDA, AFUNGUKA KUHUSU TUHUMA ZA
KUDAI POSHO.

"Huko nyuma niliwahi kutoa maelezo kuwa kazi
tuliyopewa ni ya watanzania na inahitaji
muafaka wa kitaifa ili tupate Katiba itakayokidhi
mahitaji na matarajio ya watanzania,Katiba
bora itakayojali haki na usawa kwa ustawi wa
Taifa letu kwa zaidi ya miaka 50 ijayo.

Kuna baadhi ya watu wameanza kujivika
uwakala wa kuwa wasemaji wangu, tena kwa
nia ya kutaka kuniondoa katika ajenda hii ya
msingi kwa maslahi ya watanzania. Nimekuwa
nikipigiwa simu na kupokea meseji kuhoji juu ya
taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao
kuwa ninadai ongezeko la POSHO. Naomba
ieleweke kwamba sijazungumza na chombo
chochote cha habari wala kuandika kwenye
mitandao ya kijamii kuhusu suala la posho.
Taarifa zilizosambazwa kuhusu mimi sio sahihi.

Najitambua na natambua wajibu wangu kwa
taifa na kwa watanzania wote katika mchakato
huu. Natambua hali ya maisha ya watanzania
na natambua matarajio yao kwetu, sijateuliwa
kuwa mjumbe ili nipate maslahi binafsi ya
kiuchumi bali kushiriki katika kuamua
mustakabali wa Tanzania tunayotaka kuijenga.
Hatuwezi kuwa na azma ya kupunguza pengo
kati ya walionacho na wasionacho, huku
tukiendelea kudai maslahi makubwa zaidi kwa
WABUNGE na wawakilishi na kusahau maslahi
ya wanyonge walio wengi.

Nawaomba vijana wenzangu na wale wote
wanaosambaza taarifa hizo, badala ya kutumia
muda mwingi kuandaa majungu na fitina,
tumieni muda vizuri kutushauri mambo ambayo
sote kwa pamoja tunadhani yatasaidia
kuliendeleza Taifa letu kiuchumi, kisiasa na
kijamii".

By

@paulmakonda
Share:

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHUDHURIA MKUTANO WA NNE WA NCHI WASHIRIKA WA KANDA YA KASKAZINI, JIJINI KAMPALA UGANDA


 Viongozi Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki wakiimba wimbo maalumu wa Afrika Mashariki, kabla ya kuanza rasmi Mkutano wa Nne wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Ushirikiano wa Kanda ya Kaskazini, uliofanyika jana kwenye Hoteli ya Speke Resort Munyonyo jijini Kampala Uganda, ambapo Tanzania imeshiriki Mkutano huo kama Mwalikwa. Picha na OMR

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kushoto) akizungumza katika mkutano huo. Picha na OMR
 Rais wa Uganda Yoweri Museven, akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Nne wa wakuu wa Nchi wanachama wa Ushirikiano wa Kanda ya Kaskazini. Umoja huo unaundwa na nchi za Uganda, Kenya, Rwanda na Sudan Kusini,Tanzania na Burundi zimeshiriki mkutano huo kama nchi waalikwa ambao pamoja na mambo megine waliyojadili ni kukamilisha miradi mbalimbali inayofanywa kwa pamoja na ushirikiano huo. Picha na OMR
 Baadhi ya washiriki wa mkutano huo Ujumbe wa Tanzania
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kushoto) na Rais wa Burundi Gervas Rufykiri, wakitia saini kushiriki katika mkutano huo. Picha na OMR
 Makamu wa Rais Dkt Bilal (katikati) akizungumza na Rais wa Uganda Yower Museven (kulia) baada ya Mkutano huo. Picha na OMR
Share:

ZIARA YA MZEE MANGULA CHINA

 Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula akisalimiana na Kada wa CCM, Suleiman Serera ambaye ni miongoni mwa makada walimlaki Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Beijing, China, juzi
 Msafara wa Mzee Mangula kutoka Uwanja wa Ndege wa Beijing
 Mzee Mangula akiwa na Balozi wa Tanzania Nchini China Abdulrahman Shimbo
Makamu Mangula akizungumza na Mwenyeji wake aliyempokea baada ya kuwasili nchini China, Ndg. Wang Heming ambaye ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa kitengo cha Mambo ya Afrika katika Idara ya Kimataifa ya Kamati Kuu ya CPC.
 Makamu Mangula akizungumza na baadhi ya makada wa CCM wa Tawi la China waliomtembelea katika hoteli ya Diaoyutai alipofikia na Ujumbe wake.
 Makamu Mangula akizungumza na baadhi ya makada wa CCM wa Tawi la China waliomtembelea katika hoteli ya Diaoyutai alipofikia na Ujumbe wake.
 Makamu Mangula akizungumza na baadhi ya makada wa CCM wa Tawi la China waliomtembelea katika hoteli ya Diaoyutai alipofikia na Ujumbe wake.
 Makamu Mangula akizungumza na baadhi ya makada wa CCM wa Tawi la China waliomtembelea katika hoteli ya Diaoyutai alipofikia na Ujumbe wake.
Makamu Mangula na Ujumbe wake wakiwa ktk picha ya pamoja na Makada waliopo mjini Beijing waliomtembelea ktk hoteli aliyofikia. 
Share:

MEMBE; SERIKALI KUENDELEA KUSAIDIA KUSIMAMIA MASUALA YA AMANI BARANI AFRIKA


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu masulala mbalimbali ya uhusiano wa kimataifa ikiwamo hatua zinazochukuliwa na Tanzania katika kusuluhisha Migogoro inayotokea ndani na nje ya mataifa mbalimbali na kusisitiza kuwa Tanzania haiwezi kuingia katika mgogoro na majirani zake, Wakati wa Mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe akifanya mahojiano na Mwandishi wa shirika la utangazaji la Uingereza (BBC) Erick David Nampesya leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa Habari waliohudhuria mkutano wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam. 

(Picha na Hassan Silayo)

Frank Mvungi
Serikali ya Tanzania imesema  haina ugomvi na nchi jirani kwa kuwa ni wadau  wa maendeleo katika  kujenga uchumi imara kwa kutumia fursa  zilizopo.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Bernard Membe wakati akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es salaam kuhusu taarifa mbalimbali zinazoripotiwa na vyombo vya habari kuhusu uhusiano wa Tanzania na Rwanda.

Akieleza zaidi Mh.Membe alisema vyombo vya habari  vinalojukumu kubwa la kuielimisha jamii na kuimarisha uhusiano kati Tanzania na nchi jirani na si kufanya jambo lolote linaloweza kuleta tofauti kati ya Taifa moja na jingine.
Mh. Membe amesema kuwa Tanzania ni nchi inayotumia njia za Kidiplomasia kuondoa tofauti zozote zitakazojitokeza  kati yake na nchi yoyote na haina mpango wa kuingia kwenye mgogoro na nchi yoyote ile.

Aliongeza kuwa Tanzania kwa miaka mingi imekuwa kisiwa cha amani na mfano bora katika bara la Afrika ndio maana imekuwa mstari wa mbele katika kutatua migogoro ndani ya bara la Afrika.

Akifafanua zaidi Mh. Membe amesema Tanzania imepeleka vikosi vyake  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,Lebanon,Sudan ya Kusini, katika kutimiza jukumu la kulinda amani Duniani.

“Tunafikri ni vyema Jukumu la ulinzi  wa Bara la Afrika likawa mikononi mwa Afrika yenyewe” alisisitiza Mh.Membe alipokuwa akifafanua kuhusu nafasi ya Tanzania katika kuleta amani katika mataifa mbalimbali ndani na nje ya Bara la Afrika.

Pia alieleza kuwa tangu harakati za ukombozi wa bara la Afrika Tanzania imekuwa  makao makuu ya vyama vyote vya ukombozi barani Afrika na kusaidia katika harakati za kuleta ukombozi .

Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa mwaka huu imepanga kufanya maandalizi mazuri yatakayoiwezesha timu ya Taifa kushiriki na kupata medani katika michezo ya jumuiya ya madola.
Share:

NAPE: NDOTO ZANGU KABLA YA KUWA MWANASIASA NILITAMANI KUWA ASKARI WA KURUSHA NDEGE ZA KIJESHI

Wednesday, February 19, 2014

*Azungumzia tofauti yake na wanasiasa waliopo upinzani
*Asema CCM haijatelekeza wasanii
*Asema nyimbo za Bongo Fleva hazidumu kwa sababu ya mashairi ya kulipua
*Ni kwa sababu ya wasanii kutaka 'watoke' haraka
*Akunwa na Kina Mwana FA, Lina na Lady Jay Dee

NAPE NNAUYE
NA BASHIR NKOROMO, DSM, Tanzania
KATIBU wa NEC Itikadi na Uenezi-CCM Nape Nnauye amesema, ndoto aliyokuwa nayo ya kazi ambayo angependa kufanya alipokuwa hajawa mwanasiasa ni kuwa askari ambaye rubani wa ndege za kijeshi.

Amesema maandalizi ya kutimiza ndoto hiyo alikuwa ameianza kwa kuweka kipaumbele kwenye masomo ya fani hiyo ikiwemo fizikia na jiografia wakati anamaliza kidato cha nne.

Nape mwenye umri wa miaka 37, sawa na umri wa CCM, amesema hayo leo alasiri  alipododoswa na watangazaji kwenye kipindi cha 'Power Jam' katika Kituo cha Radio cha East Africa, kilichopo Mikocheni jijini Dar es Salaam, ambao walitaka awaambie wasikilizaji ni kazi ya fani ipi aliyokuwa akiipenda kuifanya asingekuwa mwanasiasa.

"Kazi niliyopienda zaidi ni kuwa Mwanajeshi, tena Mwanajeshi mwenyewe ambaye ni rubani wa kurusha ndege za kijeshi...Na hata nilipokuwa namaliza kidacho cha nne, nilikuwa nimejiandaa zaidi katika masomo ya fani hiyo ikiwemo fizikia na jiografia", alisema, Nape.

ANAVYOJITOFAUTISHA NA WANASIASA WALIOPO VYAMA VYA UPINZANI
Akizungumzia tofauti iliyopo kati yake na wanasiasa walipo kwenye vyama vya upinzani kama walivyotaka kujua watangazaji hao, Nape alisema, tofauti kubwa iliyopo ni kwamba yeye ni mwanasiasa ndiyo sababu yupo kwenye chama cha CCM ambacho ni cha siasa lakini wapinzani siyo wanasiasa bali ni wana harakati kwa sababu wapo kwenye vyama vya harakati siyo vya siasa.

"Unajua mimi ni mwanasiasa ndiyo sababu nipo kwenye Chama Cha Mapinduzi ambacho ni chama cha siasa, lakini hao wengine ni wana harakati ndiyo sababu wapo kwenye vyama vya harakati. Na hii ndiyo tofauti kubwa ya mimi na wao", alisema Nape.

JE CCM IMEWATELEKEZA WASANII AMBAO HUWATUMIA KWENYE SHUGHULI ZAKE WA KAMPENI?
Akijibu swali la watangazaji hao ambao kwa bahati mbaya mtandao huu haukuweza kuyashika majina yao, ambao walitaka kujua Nape alikuwa anasemaje kuhusu tetesi za mitaani kwamba wasanii CCM imewatelekeza wasanii ambao wamekuwa wakitumia kwenye kampeni zake, Nape alisema si kweli kwamba CCM imewatelekeza.

"Wanaosema kwamba wasanii hao CCM imewatelekeza wanakosea, nadhani kwa kutojua hasa kuwa Chama kinawatumiaje.. Ni kwamba wakati wa shughukli zetu kama za kampeni huwa tunaingia nao mkataba wa kutufanyia kazi na tukisha walipa kwa makubaliano ya kazi husika, kazi ikimalizika hatuwezi kuendelea nao, matarajio yetu ni kwamba wataendelea na shughuli zao kama kawaida", alisema Nape na kuongeza;

"Mikataba ambayo CCM huingia na wasanii ni sawa na ile ambayo tunaingia na Media (vyombo vya habari) kutufanyia shughuli zetu, tukisha walipa huwa ndiyo basi mpaka tunapowahitaji tena.. Lakini Wasanii wanakuwa kwenye shughuli zetu moja ya faida wanazopata ni kupata fursa ya kueleza changamoto zinazowakabili katika kazi zao".

Nape alisema, moja ya matokeo ya wasanii hao kuambatana na Mgombea Urais wa CCM ambaye sasa ni Rais Jakaya Kikwete, kwenye kampeni za uchaguzi mkuu uliopita, ni kupiganiwa kwa hakimiliki za kazi zao hali ambayo alisema, ni utekelezaji wa agizo la Rais Kikwete ingawa utekelezaji wake bado haujakidhi kiwango.

Nape aliitaka serikali kuweka taratibu endelevu za kuhakikisha utekelezaji wa kupambana na wezi wa kazi za wasanii unakuwa wenye kuonyesha matunda ya uhakika kuliko ilivyo sasa, ambapo licha ya mapambano kuwepo lakini bado wizi nao wa kazi za wasanii upo.

"Moja ya njia ambayo ingewakomboa wasanii, na wakati huo huo ikasaidia kukuza pato la taifa kutokana na kazi zao ni kuhakikisha kila mmoja anapata haki yake kulingana na kazi aliyofanya. Ikumbukwe kwamba ukimwezesha msanii kuwekeza katika kazi zake kama muziki naye atachangia kuinua uchumi wa taifa kwa kulipa kodi", alisema Nape.

Nape aliwapongeza wasanii hasa wa muziki wa Bongofleva, kwa kuisaidia CCM katika kampeni zake za kuska kuongoza nchi na hatimaye kushinda, na kuongeza kuwa kwa kufanya hivyo hawakukosea kwa sababu CCM ndicho chama makini chenye mwelekeo wa uhakika na wa kueleweka katika kuwatumikia Watanzania.

KWA NINI NYIMBO NYINGI ZA BONGOFLEVA HAZIWI ENDELEVU?
Akizungumzia hali ya muziki wa wasanii wa Bongofleva, Nape alisema, tatizo kubwa linalosababisha muziki wao kuchuja haraka ni kutokana na kutokuwa na mashairi yenye mashiko na uhalisia hasa katika masuala ya mapenzi ambako wengi wamejikita.

Nape alisema, wakati wanamuziki wa zamani kama kina Mbaraka Mwinshehe waliimba mashairi yenye uhalisia hata katika mapenzi, mashairi ya wanamuziki hawa wa Bongo Fleva hayana uzito huo sababu kubwa inayowapeleka kwenye tungo za mashairi ya kulipua ikiwa ni tamaa ya kutaka mafanikio ya haraka.

"Msanii anakuwa na tamaa ya kutaka atoke haraka, akitoa  singo yake moja tu anataka apate kila tu, nyumba nzuri, gari la kifahari na pesa za kujirusha kwenye klabu za starehe, basi", alisema Nape.

WANA-BONGOFLEVA WANAOMKUNA
Akijibu kuhusu wanamuziki gani za muziki wa kizazi kipya anaowaona kuwa ni magwiji katika fani, Nape alisema, ni wengi lakini Kina Mwana FA, Lina na Lady Jay Dee ni miongoni mwa wanamuziki wa muziki wa fani hiyo ambao wanamkuna.

Nape alimaliza kuhojiwa katika kipindi hicho kwa kuimba wimbo wa  'zilipendwa' ambao baadhi ya mashairi yake ni; "Napenda nipate lau nafasi, nipate kusema na we kidogo aa mama aa, mwenzio naumia....

Nape alisema, ni mpenzi wa muziki kiasi kwamba nyumbani kwake na seti za vyombo vya muziki mithili ya Studio na karibu vyombo vyote vya muziki ikiwemo gita, drums, tumba na kinanda anajua kuvicharaza na kwamba kupiga vyombo vya muziki ndiyo ulevi wake mkubwa

MSAADA TOKA UINGEREZA KWA MAMA WA MAPACHA WANNE WA MBEYA

Misaada ya hali na mali imeanza kumiminika kwa ajili ya Aida Nakawala (25) mkaazi wa kijiji cha Chiwanda, Wilaya ya Momba, Mkoa wa Mbeya, ambaye alijifungua watoto wanne kwa mkupuo (Quadruplets) usiku wa kuamkia Mwaka mpya wa 2014 katika Hospitali ya Wazazi ya META jijini Mbeya.
 Msamaria mwema wa Uingereza, Bi Gladness Sariah, ametuma maboksi mawili yenye nguo na vitu kadhaa vya watoto, ambavyo vimewasili salama katika ofisi za Michuzi Media Group (MMG) inayoendesha Globu ya Jamii jijini Dar es salaam baada ya kusafirishwa bure na Wazee wa Kazi, Serengeti Freight Forwarders ya huko Uingereza.
 Hivi sasa MMG ikishirikiana na waratibu wa misaada kwa mama huyo, Mbeya Yetu Blog, wanaandaa utaratibu wa kumfikishia Mama Aida mizigo yake haraka iwezekanavyo.
 Kwa niaba ya mzazi wa mapacha hao, Michuzi Blog na Mbeya Blog zinatoa shukrani za dhati kwa msamaria mwema Gladness Sariah kwa wema na upendo aliouelekeza kwa mzazi huyo. Huo ni mfano wa kuigwa, na tunatarajia misaada zaidi itatolewa na wasamaria wema ambao tunajua mko wengi kila kona ya dunia.
 Kama umeguswa na hili na unataka kutoa msaada tafadhali wasiliana na: issamichuzi@gmail.com ama jmwaisango@yahoo.com 
nasi tutafikisha ubani wako. 
Serengeti Freight wametoa ofa ya 
kusafirisha bure misaada ya aina hii 
ASANTENI SANA
Michuzi Blog/Mbeya Yetu Blog

Aida Nakawala 25 mkazi wa kijiji cha Chiwanda Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya, hivi karibuni alijifungua watoto wanne  mapacha kwa mkupuo(Quadliplets) katika usiku wa kuamkia Mwaka mpya anaendelea vizuri.
Mwanamke huyo ambaye kwa hivi sasa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Wazazi ya Meta akiwa na watoto wake wote wanne alijifungua majira ya saa 10 alfajiri usiku wa kuamkia Januari Mosi Mwaka huu katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi na watoto wakiwa na uzito wa kawaida tofauti na matarajio ya Wengi.
 Misaada kwaajili ya Aida Nakawala (25) mkaazi wa kijiji cha Chiwanda, Wilaya ya Momba, Mkoa wa Mbeya mara baada ya kufikishwa katika makao makuu ya Globu ya Jamii jijini Dar es salaam baada ya kusafirishwa bure toka Uingereza na Wazee wa Kazi Serengeti Freight.

Share:

Jumatano, 19 Februari 2014

WADAU WAOMBA KUDHAMINI MAONESHO YA KAZI ZA VIJANA WAJASILIAMALI YATAKAYOFANYIKA DODOMA


Mkurugenzi wa Mtendaji wa Kampuni ya Aj It Development  Bw Jackson Audiface akizungumzia  kuhusu Maonyesho ya Tatu ya Kazi za Vijana wajasiriamali Yatakayofanyika Mkoani Dododma Mwezi Aprili mwaka huu.Maonyesho hayo ya kazi za Vijana wajasiriamali Hususani Vijana wanaosoma Vyuo Vikuu vya Dodoma. Lengo la Manonyesho hayo ni Kuzitangaza Kazi za Vijana wajasiriamali Wa Tanzania.Pili kuwapa Muda wadau Mbalimbali Kukutana na Vijana Wajasiriamali Ili kutatua Kero zote zinazowakabili vijana Katika Shuguli zao za Ujasiriamalia .
 Baadhi ya Bidhaa Ambazo zinazozalishwa na Vijana wajasiriamali Waliohitimu Vyuo vikuu Mbalimbali hapa Nchini Na Ambao Bado wako Vyuoni kuendelea na Masomo yaoamabzo zitaonyeshwa katika Maonyesho hayo Yatakayofanyika Mkoani Dodoma Yakiwa Ni ya Tatu kuafanyika hapa Nchini kwa Lengo la Kukuza soko la Kazi za Vijana wajasirimali pia Kuzitangaza na Kuatatua Ngangamoto Mbalimbali Zinazowakabili Vijana wa Kitanzania Kama Vile Vibali vya Kufanya Biashara Kutoka Mamlaka Mbalimbali hapa Nchi.Wadau Mbalimbali wa Vijana Mnaombwa Kujitokeza Kudhamini Maonyesho hayo.Bidhaa Mbalimbali za Kilimo Zinazozalishwa na Vijana wa Mkoani Dodoma Ambao watazionyesha kwa Wakazi wa Mkoa wa Dodoma na Mikoa ya Jirani.Bw Jackson Audiface Akielezea Zaidi Kuhusu Maonyesho hayo Yatakayofanyika Mkoani Dodoma.Hapa Akiwa Ameshika Mafuta yanayozalishwa na Vijana wajasirimali wa Mkoani Dodoma jana Wakati wajasiriamali hao walipotembelea Ofisi za Kampuni ya Aj It Development Kwajili ya Kujisajili ili kushiriki Katika Maonyesho ya Kazi za Vijana wajasiriamali Yatakayofanyika Mkoani Dodoma


Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Akikagua Moja ya Shuguli za Kikundi cha Vijana kijulikanacho Kama Mae Ambao watashiriki Katika Maonyesho hayo.
Kampuni ya AJ IT DEVELOPMENT  inatarajia kufanya Maonyesho ya Tatu ya Kazi za  vijana Wajasiriamali Yanayofahamika kama Tanzania Youth Enterprenuership Program (TAYEP) Yanayotarajiwa Kufanyika April 3 - 5 April, 2014 Mkoani Dodoma.

Kwa mujibu  Mkurugenzi wa Kampuni ya AAj It Development  Bw Jackson Audiface, Maonyesho hayo ya  aina yake kufanyika nchini Tanzania yenye lengo la Kuzitangaza Kazi za Vijana Wajasiriamali .
“Maonyesho haya Yalianzishwa Kwa Lengo la Kutatua changamoto zote zinazowakabili Vijana wajasiriamali Pindi wanapojishugulisha Katika Shuguli zao za Ujasiriamalia.
Aliongeza kuwa washiriki watapata Ya Kuzitangaza Kazi zao,Kujua Taratibu Mbalimbali na Namna Ya Kuingiza bidhaa zao Kwenye Masoko Mbalimbali kwa Wingi zaidi.Namna ya Kupata vibali Mbalimbali vya Kufanyia Biashara Kutoka Mamlaka Mbalimbali za serikali.Kupata elimu namna ya Kuziboresha Bidhaa zao ziendane na soko pia Kukidhi viwango na Matakwa ya Wateja.Kuwakutanisha na wadau Mbalimabali wa Vijana na Kujua taratibu  namna ya Kushirikiana na Wadau hao katika Kuboresha Bidhaa zao.
Akizungumza mfumo utakaotumika kuendesha Maonyesho hayo Bw Jackson Audiface Alisema Kila Mshiriki Atapata Fursa ya Kuonyesha Kazi yake na Kuilezea Kwa Kina pia na Changamoto Anazokabiliana nazo kazi kazi zao za Ujasiriamali.
Walengwa wakuu wa Maonyesho hayo ni Vijana Kutoka Mkoani Dododma Hususani Vijana Kutoka Vyuo Vilivyoko Mkoani Dodoma.        
Washiriki wa Maonyesho hayo wanatarajiwa kuwa 3,000 Ambapo Vijana 250 Wataonyesha Kazi zao Zikiwemo Bidhaa za Kilimo ,Teknolojia ya Habari,Sayansi ya Kompyuta,Utalii wa Ndani na Ufugaji.
“Tunaomba makampuni na mashirika  Ambao ni Wadau wakubwa wa Maendeleo ya vijana kutumia fursa hii Kufadhili Maonyesho Hayo ili waweze Kujione Fursa Mbalimbali Wanazofanya Vijana. Pili  kujitangaza, na kutangaza bidhaa na huduma zao, kwa lengo la kuongeza ufahamu wa bidhaa zao 
Mgeni rasmi wa Maonyesho Hayo anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Mizengo Pinda.
Share:

Jumanne, 18 Februari 2014

TAARIFA RASMI YA CCM
Kati ya tarehe 13/02/2014  na tarehe 18/02/2014 kumekuwa na mfululizo wa vikao kadhaa vya Chama kitaifa vilivyoshughulikia suala la maadili ndani ya Chama.

Vikao hivyo ni pamoja na Kamati Ndogo ya Udhibiti tarehe 13-14/02/2014, Tume ya Udhibiti na Nidhamu 18/02/2014 na Kamati Kuu tarehe 18/02/2013.

Waliohojiwa katika mfululizo wa vikao hivi ni wafuatao:-

     1.    Ndgugu Frederick Sumaye
2.    Ndugu Edward Lowasa
 3.    Ndugu Bernard Membe 
4.    Ndugu Stephen Wassira
      5.    Ndugu January Makamba  
6.    Ndugu William Ngeleja

Baada ya kuwahoji ilithibitika kuwa baadhi ya tuhuma dhidi yao ni za kweli na hivyo kupendekeza adhabu.  Mapendekezo hayo yalipelekwa kwenye Tume ya Udhibiti na Nidhamu na hatimaye Kamati Kuu ya CCM ambayo ilitoa adhabu kwa wahusika.

Kwa ujumla waliohojiwa wamethibitika kuwa na makosa yafuatayo:-

1.    Walithibitika kuanza kampeni za kutafuta kuteuliwa kugombea Urais kabla ya wakati kinyume na Kanuni za Uongozi na Maadili za CCM Toleo la Februari 2010, Ibara 6(7)(i).

2.    Wamethibitika kufanya vitendo vinavyokiuka maadili ndani ya Chama na baadhi yao kufanya vitendo vinavyokiuka maadili ndani ya jamii.  Kosa hili nalo ni kwa mujibu wa Kanuni za Uongozi na Maadili za CCM Toleo la Februari 2010, Ibara kadhaa za kanuni hizo.

Kamati Kuu baada ya kuthibitisha makosa hayo imewapa watu wote sita waliohojiwa adhabu ya ONYO KALI na kuwataka wajiepushe na vitendo vinavyokiuka maadili na iwapo wataendelea na vitendo hivyo Chama kitawachukulia hatua kali zaidi.

Tafsiri ya adhabu ya ONYO KALI kwa mujibu wa Kanuni za Uongozi na Maadili za CCM Toleo la Februari 2010, Ibara ya 8(ii) (b) ni:-

“Mwanachama aliyepewa adhabu ya ONYO KALI atakuwa katika hali ya kuchunguzwa kwa muda usiopungua miezi 12, ili kumsaidia katika jitihada zake za kujirekebisha.”

Kamati Kuu imeitaka pia Kamati Ndogo ya Udhibiti kuwachunguza na kuchukua hatua kwa wote waliohusika kwa namna moja au nyingine (mawakala na wapambe) kufanyika kwa vitendo hivyo vilivyovunja Kanuni za Chama.

Aidha, Kamati Kuu imewaonya vikali Viongozi na Watendaji wa Chama na kuwataka kujiepusha kujihusisha na matendo ya wanawania Urais yanayovunja na kukiuka maadili ya Chama, wametakiwa kuzingatia Kanuni na taratibu za Chama.

Imetolewa na:- 
Nape Moses Nnauye,
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
ITIKADI NA UENEZI,
18/02/2014
Share:

Jumatatu, 3 Februari 2014

RAIS JAKAYA KIKWETE AGUSWA NA UTENDAJI WA KINANA, ATAKA AWE MFANO WA KUIGWA

Kikwete akihutubia leo mjini Mbeya. Kushoto ni Kinana na Mzee Mangula
NA BASHIR NKOROMO, MBEYA
MWENYEKITI wa CCM, Rais Jakaya Kikwete leo amevunja ukimya na kuzungumzia suala la mawaziri waliotuhumiwa na wananchi kuwa mizigo wakati wa ziara za Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na baadhi ya wajumbe wa sekretarieti katika mikoa kadhaa nchini mwishoni mwa mwaka jana.
 
"Najua wapo baadhi ya watanzania, walitaka Mawaziri waliotajwa kuwa ni mizigo wafukuzwe kazi, na kwa vile halikufanyika basi suala hilo limegeuzwa kuwa la malumbano,  ni vyema ieleweke kuwa kuitwa kwa Mawaziri hao na Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), hakuna maana ya kuishia kufukuzwa", alisema, Kikwete leo akihutubia maelfu ya watu katika sherehe za kilele cha miaka 37 ya CCM, kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya. 

Alisema Mawaziri hao waliitwa kwa sababu ya kuwepo matatizo yaliyoonekana yanatakiwa yapatiwe ufumbuzi, matatizo hayo yamezungumzwa na maelekezo kutolewa kuhusu cha kufanya.

"Kamati Kuu ya CCM imetimiza wajibu wake uliobaki ni wa serikali.Kamati Kuu itaendelea kufuatilia na kama hakuna maendeleo ndipo inapoweza kuamua kuomba mamlaka ya uteuzi ichukue hatua zipasazo dhidi ya mhusika.Huko hatujafika" alisema Rais Kikwete.

Rais Kikwete alimpongeza Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akisema, ziara ambazo amekuwa akifanya ni mfano unaopaswa kuigwa na viongozi wengine hasa wa CCM kwa sababu ndio hasa unaotakiwa.

Alisema ziara za Kinana zinakijenga Chama na kutoa taswira nzuri ya CCM katika jamii kwani zinahuisha uhai wa CCM kwa kuwa Katibu Mkuu huyo katika ziara hizo huenda hadi kwa wanachama waliopo ngazi za chini.

"Katibu Mkuu Kinana amekuwa anafanya mambo ambayo baadhi ya watu wanadhani kuwa ni mageni, lakini katika kufanya hayo amekuwa pia akionyesha umahiri na ujasiri mkubwa kwa kwenda  maeneo ambayo ni magumu kufikika" alisema Rais Kikwete na kuongeza;

"Katika ziara hizo  wakati mwingine amekuwa anatumia njia za usafiri zinazoogopesha, amewahi kutumia meli  ya MV Songea kutoka mkoani Ruvuma hadi Mbeya, amepanda milima na mabonde kwa magari katika maeneo ambayo ni hatari, lakini lengo likiwa ni kuhakikisha anawafikia wanachama wa ngazi za chini kabisa".

Rais Kikwete alisema mambo mengine yalivyomvutia katika ziara za Kinana, ni hatua ya Katibu mkuu huyo kwenda kukaa na  kula na wananchi katika ngazi za chini na kisha kufanya nao kazi za maendeleo  na zaidi kutoa fursa kwa wananchi kueleza matatizo na manung'uniko yanayowasibu.

Mwenyekiti huyo wa CCM Taifa alisema Katibu mkuu wa Chama amekuwa anashiriki katika kutafuta majawabu na matatizo anayoambiwa hali ambayo imesaidia sana kumaliza baadhi ya matatizo kulekule mikoani.

"Pale ambapo pamekuwa panahitaji hatua zaidi za serikali hakusita kutoa taarifa kwa Waziri Mkuu, vile vile amekuwa anatoa taarifa ya ziara zake kwenye Kamati Kuu ya CCM" alisema Rais Kikwete.
Share:

Jumapili, 2 Februari 2014

MATEMBEZI YA MSHIKAMANO KUADHIMISHA MIAKA 37 YA CCM YAFANA JIJINI MBEYA


 Mweneyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwasili eneo la Soweto kuongoza  matembezi ya mshikamano ya miaka 37 ya CCM, yaliyofanyika leo asubuhi mjini Mbeya.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akitangaza kuwasili kwa Mwenyekiti wa CCM Rais Kikwete eneo la Soweto
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akipatiwa maelezo na Nape namna matembezi yatakavyoanza
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwapungiamikono wananchi kabla ya matembezi kuanza
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete akiwapungia mkono wananchi matembezi yalipoanza eneo la Soweto. Wengine kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM, Kinana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya Godfrey Zambi
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza matembezi hayo huku akiwa na watoto ambao aliwateua kutembea nao baada ya kuwaona eneo la Soweto
 "Haya Simameni Hapa tutembee wote" Rais Jakaya Kikwete akiwaambia watoto hao kabla ya kuanza matembezi
 "Vipi Mmechoka", Rais Kikwete akiwauliza watoto, lakini wakasema hawajachoka ambapo walitembe hadi mwisho umbali wa kilometa tano. Picha na Bashir Nkoromo. Kwa picha nyingine 28 za tukio hili> BOFYA HAPA
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Gadget

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu