Unordered List


MAANDALIZI SHEREHE ZA MIAKA 37 YA CCM YAIVA MBNEYA


 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kupalilia katika shamba la Mage Kolimwa (wapili kulia), katika Kijiji cha Mlimanyoka, Kata ya Nsalanga, wilala ya Mbeya mjini. Kinana alifika kumsaidia mkulima huyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 37 ya CCM, inayofanyika Kitaifa Jumapili hii mjini Mbeya.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akisaidiana na vijana kuweka jukwaa kwenye Bustani ya Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, ambako yaitaishia matembelezi ya sherehe za miaka 37 ya CCM, yatakayofanyika Jumapili hii ikiwa ni sehemu ya Kileleha cha maadhimisho ya sherehe hizo.
Vijana wa CCM wakiwa katika mazoezi kwa ajili ya halaiki watakayoinyesha kwenye Uwanja wa Sokoine Mjini Mbeya wakati wa kilele cha sherehe za miaka 37 ya CCM zitakazoongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete.
Vijana wakiwa katika mazoezi hayo. Picha na Bashir bNkoromo.

Chapisha Maoni

0 Maoni