Unordered List


Paul Makonda mjumbe wa Bunge la Katiba afunguka kuhusu tuhuma za kudai Posho.

MJUMBE WA BUNGE LA KATIBA PAUL
MAKONDA, AFUNGUKA KUHUSU TUHUMA ZA
KUDAI POSHO.

"Huko nyuma niliwahi kutoa maelezo kuwa kazi
tuliyopewa ni ya watanzania na inahitaji
muafaka wa kitaifa ili tupate Katiba itakayokidhi
mahitaji na matarajio ya watanzania,Katiba
bora itakayojali haki na usawa kwa ustawi wa
Taifa letu kwa zaidi ya miaka 50 ijayo.

Kuna baadhi ya watu wameanza kujivika
uwakala wa kuwa wasemaji wangu, tena kwa
nia ya kutaka kuniondoa katika ajenda hii ya
msingi kwa maslahi ya watanzania. Nimekuwa
nikipigiwa simu na kupokea meseji kuhoji juu ya
taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao
kuwa ninadai ongezeko la POSHO. Naomba
ieleweke kwamba sijazungumza na chombo
chochote cha habari wala kuandika kwenye
mitandao ya kijamii kuhusu suala la posho.
Taarifa zilizosambazwa kuhusu mimi sio sahihi.

Najitambua na natambua wajibu wangu kwa
taifa na kwa watanzania wote katika mchakato
huu. Natambua hali ya maisha ya watanzania
na natambua matarajio yao kwetu, sijateuliwa
kuwa mjumbe ili nipate maslahi binafsi ya
kiuchumi bali kushiriki katika kuamua
mustakabali wa Tanzania tunayotaka kuijenga.
Hatuwezi kuwa na azma ya kupunguza pengo
kati ya walionacho na wasionacho, huku
tukiendelea kudai maslahi makubwa zaidi kwa
WABUNGE na wawakilishi na kusahau maslahi
ya wanyonge walio wengi.

Nawaomba vijana wenzangu na wale wote
wanaosambaza taarifa hizo, badala ya kutumia
muda mwingi kuandaa majungu na fitina,
tumieni muda vizuri kutushauri mambo ambayo
sote kwa pamoja tunadhani yatasaidia
kuliendeleza Taifa letu kiuchumi, kisiasa na
kijamii".

By

@paulmakonda

Chapisha Maoni

0 Maoni