Ijumaa, 14 Machi 2014

CCM YAZIDI KUCHANJA MBUGA KAMPENI ZAKE ZA KALENGAMgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika jimbo la Kalenga, Godfrey Mgimwa akisalimiana na vijana na wananchi kwa jumla baada ya kuwasili leo katika kijiji cha Elandutwa, katika jimbo hilo, Iringa Vijijini kwa ajili ya mkutano wake wa kampeni
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu akimnadi Mgimwa katika Kijiji cha Elandutwa, Iringa Vijijini, leo
Wananchi wa Kijiji cha Elandutwa, Iringa Vijijini wakionyoosha mikono kuahidi kumpa kura zote Mgomwa katika uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, wakati wa mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika leo
Mgimwa akiwahutubia wananchi katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika kijiji cha wafugaji cha Elandutwa, Iringa Vijijini leo
Kinamama wa Elandutwa wakimshangilia mgombea wa CCM katika mkutano wa kampeni
Mtoto aliyebebwa mabegani (kushoto) akishangilia CCM, katika mkutano wa kampeni uliofanyika Kijiji cha Itwaga, leo
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Irimga, Jesca Msambatavangu (wanne kushoto) akiongoza warm-up ya aina yake kabla ya kuanza mkutano wa kampeni katika kijiji cha Elandutwa leo
Kada wa CCM kutoka Makao Makuu ya UVCCM, Mtela Mwamopamba,akihutubia mkutano wa kampeni uliofanyika Itwaga
"Jamani nchi yetu ya Tanzania ilipata Uhuru kwa kumwaga damu? Sasa tazama rangi za bendera ya chama hiki cha wenzetu. Rangi hii nyekundu inaashiria nini kwenye bendera yao?" Mwenyekiti wa CCm mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu, alisema hayo wakati akionyesha kofia yenye mpangilio wa rangi za bendera ya Chadema, kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika  kijiji cha Udumka, leo
"Nitatumia ilani hii ya CCM kuhakikisha kero zinazowakabili wananchi katika jimbo la Kalenga zinapata ufumbuzi", anasema Mgombea wa CCM katika uchaguzi mdogo wa jimbo hilo, Godfrey Mgimwa wakati akiomba kura kwenye mkutano wake wa kampeni kijiji cha Itwaga.
Katibu wa CCM mkoa wa Mtwara, Shaibu Akwilombe akihutubia mkutano wa kampeni za CCM katika kijiji cha Elandutwa
Makamanda wa ukweli wa CCM, wakiwa wamepozi kiambazani mwa nyumba ya mwanakijiji katika kijiji cha Elandutwa, wakati wakisubiri kupanda jukwaani mmoja baada ya mwingine, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji hicho. Baadhi yao kutoka kushoto ni Mtela Mwampamba, Katibu wa CCM mkoa wa Iringa Salum Mtenga na Akwilombe
"Huyu si Kijana Mwenzenu, tena Msomi? sasa wakati wenu ni huu kumchagua", Katibu wa Jumuia ya Wazazi ya CCM  akiwaambia Vijana wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika Kijiji cha Udumka
Mashabiki mbalimbali wa CCM wakiagana na mgombea wa chama hicho, Mgimwa baada ya mkutano wa kampeni wa Udumka.
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu