Alhamisi, 20 Machi 2014

CHALINZE YATEMA MKUTANO WA UZINDUZI WA KAMPENI ZA UBUNGE CCM
 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Chalinze kwenye mkutano mkubwa wa uzinduzi wa kampeni za ubunge kupitia CCM jimbo la Chalinze ambapo Kinana aliwaeleza wananchi walifuruka kwenye uwanja wa Miembe Saba kuwa "Hatupo hapa kushindana na wapinzani tupo hapa kutatua kero za wananchi wa Chalinze"

 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akimnadi mgombea wa nafasi ya ubunge jimbo la Chalinze kupitia CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete wakati wa mkutano wa uzinduzi  rasmi wa kampeni za ubunge jimbo la Chalinze.
 Mgombea Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia CCM akihutubia wananchi wa jimbo hilo wakati wa mkutano wa hadhara wa uzinduzi wa kampeni ambapo mgombea huyo aligusia masuala ya afya,barabara,elimu na kilimo cha kisasa na kuwaambia wananchi hao na anatambua changamoto zilizokuwepo hasa migogoro ya wakulima na wafugaji ambapo alisema unahitajika kutengenezwa mpango mzuri wa matumizi bora ya ardhi.Mama Salma Kikwete akiwa mstari wa mbele kumpigia kampeni mwanae Ridhiwani Kikwete kwenye mkutano wa uzinduzi rasmi wa kampeni uliofanyika Miembe Saba Chalinze.

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye ambaye pia ndio Mratibu wa Kampeni za Ubunge CCM Jimbo la Chalinze akihutubia Umati wa wakazi wa Chalinze na kuwaambia CCM itafanya kampeni za kistaarabu sana.
 Mbunge wa Simanjiro Ndugu Christopher Ole Sendeka akihutubia wakazi wa Chalinze wakati wa mkutano wa uzinduzi wa kampeni za Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia CCM.
 Viongozi na Wananchi wa Chalinze wakicheza kwa furaha wakati wa uzinduzi wa kampeni za Ubunge CCM Jimbo la Chalinze
 Kila mtu Ridhiwani Chalinze
 Sam wa Ukweli akitumbuiza wakati wa uzinduzi wa kampeni za CCM jimbo la Chalinze
Msanii wa TOT Band akinengua mbele ya meza kuu wakati wa uzinduzi wa kampeni za Ubunge CCM Jimbo la Chalinze.
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu