Jumamosi, 15 Machi 2014

KINANA AONGOZA CCM KUFUNGA MKUTANO WA KALENGA


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimnadi mgombea wa ubunge jimbo la Kalenga kupitia CCM Ndugu Godfrey Mgimwa wakati wa mkutano wa mwisho wa kampeni uliofanyika Kidamali leo tarehe 15 Machi 2014.
 Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Kidamali wakati wa kuhitimisha kampeni za ubunge jimbo la Kalenga ambapo aliwaambia wananchi wao CCM inatekeleza ilani yake ya uchaguzi ya mwaka 2010 hivyo kushinda uchaguzi huo kutaharakisha maendeleo ya Kalenga.
 Naibu Katibu Mkuu CCM(Bara) Ndugu Mwigulu Nchemba akihutubia wakazi wa kata ya Nzihi,kijiji cha Kidamali wakati wa kufunga kampeni za ubunge jimbo la Kalenga ambapo CCM imemsimamisha Godfrey Mgimwa.
Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Seif Shaaban Mohamed akihutubia wakazi wa kata ya Nzihi na kuwasihi kushikamana katika zoezi la kupia kura ili kuhakikisha ushindi unabaki CCM.
 Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM Sixtus Mapunda akihutubia wakazi wa kata ya Nzihi kijiji cha Kidamali na kuwaambia Umoja wa Vijana ipo kamili na itahakikisha ulinzi wa kutosha kwa kila mpiga kura.
 Katibu wa CCM mkoa wa Mtwara Ndugu Shaibu Akwilombe akihutubia wakazi wa kata ya Nzihi kijiji cha Kidamali na kuwaambia CCM ipo imara na inatekeleza sera zake zenye misingi bora kwa maendeleo ya Kalenga na Tanzania kwa ujumla.
 Mbunge wa Ludewa ndugu Deo Filikunjombe akihutubia wakazi wa kata ya Nzihi wakati wakufunga kampeni za ubunge ulofanika kjiji cha Kidamali.
  Mbunge wa jimbo la Mwibala Ndugu Kange Lugola  akihutubia wakazi wa kata ya Nzihi wakati wakufunga kampeni za ubunge zilizohitimishwa leo kwenye kijiji cha Kidamali na kuwataka wananchi hao kumpa nafasi Godfrey Mgimwa kwa kumpigia kura za ndio siku ya tarehe 16 Machi 2014.
Mbunge wa Viti Maalumu Pindi Chana akiwasisitiza wakina mama kupiga kura kwa mgombea wa ubunge wa CCM Godfrey Mgimwa.
Katibu Mkuu wa CCm taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akipeana mkono na Chifu Abdul Sapi Mkwawa katika viwanja vya kata ya Nzihi
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akibadilishana mawazo na Naibu Katibu Mkuuwa CCM (Bara) pamoja na mgombea wa ubunge jimbo la Kalenga kupitia CCM Ndugu Godfrey Mgimwa wakati wa mkutano wa mwisho wa kufungia kampeni uliofanyika katika kata ya Nzihi kijiji cha Kidamali.
Msanii Dokii akiongoza wakazi wa kata ya Nzihi kucheza nyimbo za kampeni maalumu kwa ajili ya Godfrey Mgimwa.
Godfrey Mgimwa akishindwa kujizuia na kuamua kudua pamoja na msanii Dokii na wakazi wa kata ya Nzihi wakati wa kuhitimisha mkutano wa kampeni kupitia CCM
Mgombea Ubunge jimbo la Kalenga akiwa amebebwa juu na wananchi wa kata ya Nzihi wakati wa kuhitimisha kampeni za ubunge jimbo la Kalenga.

 Mgombea wa Ubunge jimbo la Kalenga CCM Ndugu Godfrey Mgimwa akimtambulisha mke wake Robby Salehe Mgimwa mbele ya umati wa wakazi wa kata ya Nzihi wakati wa kuhitimisha kampeni za ubunge zilizofanyika leo tarehe 15Machi 2014.
 Kamanda wa Vijana wa mkoa Iringa Salim Faraj Abri  alikuwepo kuhakikisha mkutano unaenda vizuri wakati wa kuhitimisha kampeni za ubunge jimbo la Kalenga katika kata ya Nzihi kijiji cha Kidamali.
Sehemu ya wakazi wa kata ya nzihi wakifuatilia kwa makini mkutano wa mwisho wa kampeni za ubunge CCM
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu