Jumatano, 5 Machi 2014

MBUNGE WA KIBAHA VIJIJINI AMWAGA PIKIPIKI NA BAISKELI KWA VIONGOZI WA KATA NA MASHINA


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Kibaha Kijijini kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Mtongani ambapo aliwaambia moja ya kazi kubwa ya viongozi wa CCM ni kutekeleza yale walioahidi kwa wananchi.
 Mbunge wa Kibaha Kijijini Ndugu Hamoud A. Jumaa akihutubia wakazi wa Kibaha Kijijini na kuwaambia mafanikio waliyoyapata ikiwa pamoja na kufungua ofisi ya kisasa ya Mbunge kugawa pikipiki tisa na baiskeli themanini na sita kwa makatibu kata na mabalozi wa shina.
 Isha Mashauzi akitumbuiza wakazi wa Kibaha Kijijini  wakati wa mkutano wa hadhara ambao Katibu Mkuu wa CCM alikuwa mgeni wa Heshima.
 Viongozi wa CCM wilaya ya Kibaha wakicheza rusha roho wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Mtongani.

 Suleiman Jabir maarufu kama Msagasumu akiburudisha umati uliofurika kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Mtongani Kibaha Kijijini.
 Hamis Rashidi akirudisha kadi na makabrasha ya CUF kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na kujiunga na CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya Msingi Mtongani Kibaha Kijijini.
 Wanachama wapya wakila kiapo baada ya kukabidhiwa kadi za uanachama wa CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Mtongani ambapo mgeni wa Heshima alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Pikipiki tisa na Baiskeli themanini na sita zilizotolewa na Mbunge wa Kibaha Kijijini Ndugu Hamoud A. Jumaa kwa Makatibu kata na viongozi wa mashina wa Kibaha Kijijini.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani Ndugu Mwishehe Shaban Mlawa akimuambia Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana waanze safari kwa pikipiki mpya zilizotolewa na Mbunge wa Kibaha Kijijini Ndugu Hamoud A.Jumaa kwa Makatibu kata na wajumbe wa mashina 86 kwenye viwanja vya shule ya msingi Mtongani.
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu