Ijumaa, 14 Machi 2014

RAIS KUMWAPISHA YAHYA KHAMIS HAMAD KUWA KATIBU WA BUNGE MAALUM LA KATIBA, DR KASHILILAH KUWA NAIBU KATIBU


DODOMA, Tanzania
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo asubuhi, Ijumaa, Machi 14, atamwapisha Katibu wa Baraza la Wawakilishi Bwana Yahya Khamis Hamad kuwa Katibu wa Bunge Maalum la Katiba.

Aidha, katika sherehe fupi itakayofanyika Ikulu Ndogo, Dodoma, Rais Kikwete atamwapisha Katibu  wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Thomas Didimu Kashililah kuwa Naibu Katibu wa Bunge Maalum la Katiba.

Taarifa iliyotolewa jioni ya jana jioni, Machi 13, mwaka huu wa 2014 mjini Dodoma na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue inasema kuwa Rais Kikwete atawaapisha Katibu na Naibu Katibu wa Bunge Maalum la Katiba kwa mujibu wa kifungu cha 24(7) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83, toleo la mwaka 2014.

Bwana Hamad na Dkt. Kashilillah wanashika  nafasi hizo kwa mujibu wa Kifungu cha 24(1) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83, toleo la mwaka 2014, ambacho kinasema kuwa nafasi za Katibu na Naibu katibu wa Bunge Maalum la Katiba zitajazwa na Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katibu wa Baraza la Wawakilishi, Zanzibar.

Kwa mujibu wa kifungu cha 24(3) cha sheria hiyo, Sura ya 83, toleo la mwaka 2014, Katibu wa Bunge Maalum atatoka upande tofauti na ule anakotoka Mwenyekiti wa Bunge Maalum.

Kwa vile aliyechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum, Mheshimiwa Samuel John Sita anatoka Tanzania Bara, basi Katibu wa Bunge anakuwa Bwana Yahya Khamis Hamad ambaye ni Katibu wa Baraza la Wawakilishi, Zanzibar na Naibu Katibu wa Bunge Maalum la Katiba anakuwa Dkt. Kashililah  ambaye ni Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu