Unordered List


WANANCHI WA KALENGA WAPIGA KURA LEO


 Wananchi wakiwa kwenye kituo cha kupiga kura cha Kalenga A leo wakati wa upigaji kura, katika uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, Iringa Vijijini.
 Yosefa Cosmas akitumbukiza kura yake kwenye kisanduku kwenye kituo cha kupigia kura cha Mangalale B, wakati wa uchaguzi huo
Josephine Myagile akitafakari kidogo baada ya kutumbukiza kura yake kwenye kisanduku katika kituo cha Kalenga B
 Msimamizi wa kituo cha kupigia kura cha Kalenga B, akimtafutia jina, Joseph Mdibule kwa ajili ya kupiga kura kwenye kituo hicho
 Zaveri Alphonce (70) akijikongoja kwenda kupiga kura kwenye kituo cha  Kalenga A katika uchaguzi huo
Polisi akilinda moja vituo vya kupigia kura wakati wa uchaguzi
 Wazee wenye matatizo maalum wakisubiri kuitwa kupiga kura kwenye kituo cha Mangalale A, jimbo la Kalenga, wakati wa uchaguzi huo
 Watu kwenye kituo cha kupigia kura cha Mangalale A, wakati wa uchaguzi huo
Mgombea wa CCM  Godfrey Mgimwa akizungumza na waandishi baada ya kukagua vituo kadhaa  vya kupigia kura, wakati wa uchaguzi huo. Picha zote Bashir Nkoromo wa theNkoromo Blog

Chapisha Maoni

0 Maoni