• UVCCM TAIFA

  SAUTI YA VIJANA,SAUTI YA UMMA.CCM MPYA,TANZANIA MPYA.

 • UVCCM TAIFA

  MWAKA MMOJA WA SERIKALI YA AWAMU YA TANO.

 • This is default featured slide 3 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

 • This is default featured slide 4 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

 • This is default featured slide 5 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

Jumatano, 30 Aprili 2014

NCHI ZIMILIKI MAGEUZI YA SEKTA ZA USALAMA: TANZANIA


Na Mwandishi Maalum
Tanzania,  imeungana na mataifa mengine katika kusisitiza umuhimu wa nchi kumiliki mchakato wa Mageuz iya Sekta za Usalama ( Security Sector Reform).
Akichangia majadiliano ya Baraza Kuu la Usalama  la Umoja wa Mataifa ambalo lilikutana kwa siku nzima ya Jumatatu  wiki hii, kujadili taarifa ya Katibu Mkuu kuhusu SSR,  Naibu Mwakilishiwa Kudumu wa Tanzania katika  UN, Balozi Ramadhan Mwinyi amesema, Tanzania kama ilivyo kwa nchi nyingine nyingi inapenda kuona kwamba mageuzi ya sekta za usalama yanamilikiwa na nchi zenyewe zikiwamo nchi zinazotoka katika machafuko.
Katika Mkutano huo, Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, lilipitisha kwa kauli moja na kwa mara ya kwanza Azimio linalojitegemea kuhusu mchakato wa Mageuzi ya Sektaza Usalama,kupitia azimio hilo namba 2151 (2014)  pamoja na kusisitiza umuhimu wa dha nazima ya mageuzi ya sekta za usalama na umuhimu wake kwa usalama, amani na ustawi wa mwanadamu.
 Azimio linasisitiza kwamba umiliki wa nchi katika mageuzi hayo ni jambo la muhimu.
Akaongeza kuwa makundi ya wapiganaji na ambao wameka silaha zao chini na kuingia katika mchakato wa majadiliano wanapaswa pia kuwa sehemu ya mageuzi ya sekta za usalama.
Akasema kwa kuyashirikisha makundi hayo ya wapiganaji na mengine kutasaidia ujenzi wa Amani na usalama na pia kuepusha kujirudia kwa mapigano.
Aidha Balozi Mwinyi, ameleza kwamba, nchi zinazopakana na nchi zinazotoka kwenye machafuko pia zinayo nafasi na wajibu wa kutoa ushirikiano na uzoefu wao katika ujenzi wa sekta za usalama.
Vile vile Balozi amebainisha kwamba katika miongo ya miaka mitano iliyopita imedhihirisha wazi umuhimu wa jumuia za kikanda katika uzuiaji wa mapigano, ulinziwa Amani naujenziwa Amani.
Majadiliano hayo yalifunguliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na yaliitishwana Nigeria ambayo ni Rais wa Baraza hilo kwa Mwezi huu wa April. Waziri wa Mambo ya Nje wa Nigeria  Bw. Aminu Wali aliongoza majadiliano.
Wawakilishi kutoka nchi 42 wanachama waUmojawa Mataifa, zilizungumza wakati wa majadiliano kuhusu dhana hiyo ya mageuzi ya sektaza usalama, na bila ya kujali tofauti zao,  kila moja ilisisitiza hoja ya nchi kumiliki mchakato huo hata kwa zile ambazo zimetoka katika machafuko au mapigano.
Aidha pamoja na kusisitiza haja na umuhimu wa nchi kumiliki mchakatohuo, zimeongeza kuwa bado kuna haja ya Jumuiya ya Kimataifa,  kuziwezesha nchi hasa zile zinazotoka katika machafuko kuweza si kujenga upya sekta hizo za usalama bali pia kuzifanyia mageuzi.
Vile vile ilisisitizwa pia kuwa mageuzi hayo ya sekta za usalama ni muhimu katika kuziimarisha nchi ambazo ndiyo kwanza zimetoka kwenye machafuko. Na kwamba mageuzi hayo yatapewa kipaumbele katika utekelezaji mamlaka za ulinzi wa Amani  na misheni maalum za Kisiasa.
Wajumbe wengine walikwenda mbalizaidi, kwa kueleza kwamba mageuzi hayo ya sektza za usalama yanapashwa kuwajumuishi kwa maana ya kushirikisha makundi mengine ya kijamii. Lakini kwa msisitizo kwamba serikali ndiyo iwe na mamlaka ya kuamua mfumo wa sekta zake za usalama.
Katika salamu zake za ufunguzi Ban ki Moon,  alisema,  lengo la kutekeleza mageuzi ya sekta za usalama ambazo ni pamoja na jeshi, polisi na vyombo vya usalama ni kuwawezesha wananchi ambao ndiyo walengwa kuishi maisha yenye usalama.

“Sektaza Usalama ndiyo muhimili mkuu wa makubaliano kati ya serikali na wananchi wake. Mamlaka ya kutumia nguvu nilazima yaendane na wajibu wa kulinda raia na kuheshimu haki za binadamu” akasemaKatibuMkuu.
Kwa mujibu wa Ban Ki Moon,  sekta za usalama zinazotekeleza majukumu yake chini ya misigi ya utawala wa sheria zina uwezo wa kuimarisha imani ya wananchi kwa serikali yao na hivyo kuchangia katika uimara wa ujenzi wa Amani namaendeleo.
Share:

Jumatatu, 28 Aprili 2014

ZIARA YA MWENYEKITI WA UVCCM TAIFA YATIKISA KATA YA KAWE


 Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM, Taifa, Sadifa Juma (wapili kushoto) akiwasili kwenye Uwanja wa Mkutano eneo la Tanganyika Packers, Kawe Dar es Salaam, Jumapili, Aprili 27, 2014 ambako mbali na kuhutubia mkutano wa hadhara, alikabidhi vifaa vya michezo kwa timu mbalimbali za soka katika kata ya Kawe. Kulia ni Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Kawe, Lilian Rwebangila na Katibu wa UVCCM wa kata hiyo, Aisha Katundu na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Kata hiyo Said Herry.
 Vijana wa CCM na wananchi kwa jumla wakimsindikiza Sadifa, kwa hamasa kuingia uwanjani
 Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM (Bara) Mfaume Ali Kizigo akihutubia kwenye mkutano wa hadhara wa UVCCM uliofanyika viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe Dar es Salaam, Jumapili ya Aprili 27, 2014, kumkaribisha Sadifa kuhutubia.
 Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Kawe Lilian Rwebangila akimkaribisha Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Hamis Juma, kuhutubia mkutano huo wa hadhara kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe.
 Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Hamis Juma, akihutubia mkutano wa hadhara huku shamrashamra zikitawala, kwenye Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe, Dar es Salaam, Jumapili Aprili 27, 2014.
 Sadifa akigawa vifaa vya michezo kwa kiongozi wa timu ya soka ya Ukwamani Shooting, wakati wa mkutano huo
 Mlezi wa UVCCM Kata ya Kawe, Coolman Massawe, akikabidhi vifaa vya michezo kwa kiongozi wa timu ya Ukwamani, Ali Kidogodogo, wakati wa mkutano huo
 Sadifa (kushoto) akishuhudia wakati Katibu wa CCM wilaya ya Kinondoni, Athuman Shemsha, akimtawaza Kada wa CCM, Vincet Massawe, wakati wa mkutano wa hadhara wa UVCCM  uliofanyika Viwanja vya Tanganyika Packers, Kawe, Dar es Salaam, Jumapili, Aprili 27, 2014

 Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Juma Hamis akimwelekeza jambo, Kamanda wa UVCCM Kata ya Kawe, Vincent Masawe wakati wa mkutano huo
 Kamanda wa UVCCM Kata ya Kawe, Masawe akishukuru kwa kupewa ukamanda huo. Kushoto ni Sadifa akimsikiliza
 Katibu wa UVCCM Kata ya Kawe, Dar es Salaam, Aisha Kitundu (katikati) akiwa na Wasanii wa Kikundi cha TOT, Malkia wa Mipasho Nchini, Khadija Kopana na Jane Komba wakati wa mkutano huo
 Viajana wa Kikosi kazi cha UVCCM Kata ya Kawe wakipozi kwa picha maalum ya kumbukumbu wakati wa mkutano huo.
 Baadhi ya viongozi wa CCM na UVCCM Kawe waliohudhuria kwenye mkutano huo. Kushoto ni Kamanda wa UVCCM Kawe,Aisha Voniatis na Mlezi wa Wazazi Muta Rwakatare
 Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM (Bara) Mfaume Ali Kizigo akiwa na viongozi wa Chipukizi, Nimka Lameck (Mwenyekiti wa Chipukizi Taifa) na Maleo Motelo (Mwenyekiti wa UVCCM Kinondoni) baada ya uzinduzi wa Tawi UVCCM la Kawe, Mnarani, Dar es Salaam, Jumapili, Aprili 27, 2014.
 Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Hamis Juma akizindua Tawi la UVCCM, Kawe Mnarani, DSar es Salaam, Jumapili, Aprili 27, 2014.
Kamanda wa UVCCM Kawe, akitoa mchango wa sh.  200,000 kwa Ktb wa tawi la UVCCM Mnarani, Mlangala Zacharia kwa ajili mradi wa maendeleo ya tawi hilo. Picha zote na Bashir Nkoromo wa CCM BLOG
Share:

Jumamosi, 26 Aprili 2014

VIJANA WAFANYA MATEMBEZI YA UZALENDO


 Vijana wakiwa kwenye matembezi ya Uzalendo yalioratibiwa na Umoja wa Vijana wa CCM katika kuadhimisha miaka 50 ya Muungano ambapo vijana hao walianzia matembezi kutoka ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Temeke mpaka kwenye viwanja vya sabasaba na kulakiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete.
 Vijana wakionyesha uzalendo kwa kuonyesha skafu zao zenye  jina la Tanzania
 Ujumbe maridhawa ambao ndio gumzo la mjni kwa sasa.
 Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam Ndugu Ramadhani Madabida muda mchache kabla ya kupokea matembezi ya Uzalendo yaliofanywa na vijana mbali mbali .

 Mwenyekiti wa UVCCM Ndugu Sadifa Juma Khamis akienda kukabidhi bendera ya Taifa kwa Dk Jakaya Mrisho Kikwete .
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ameshikilia picha ya  Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage huku Rais wa Mapinduzi ya Zanzibar  Dk.Ali Mohamed Shein akiwa ameshikilia picha ya  Rais wa kwanza wa Zanzibar Sheikh Abeid Amani Karume baada ya kuzipokea kutoka kwa vijana waliofanya matembezi ya Uzalendo.
Share:

SHEREHE ZA MIAKA 50 YA MUUNGANO ZAFANA


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akiwapungia mkono wananchi waliohudhuria sherehe za miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na Viongozi mbali mbali wa ndani na nje ya nchi.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la Jeshi la wananchi kwenye sherehe za miaka 50 ya Muungano wa Tanzania.
 Kikosi cha Makomandoo kikipita kwa mwendo wa aina yake wakati wa sherehe za miaka 50 ya Muungano.
 Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria sherehe za miaka 50 ya Muungano ambazo zimefanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
 Kikosi cha Makomandoo kikitoa salaam kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya Muungano.
 Makomandoo wakionyesha namna ya kupambana bila kutumia nyenzo hapa wakivunja matofali kwa kutumia kichwa na mikono.
 Baadhi ya silaha zakijeshi zikipitishwa mbele ya umati kuonyesha uwezo mkubwa wa jeshi letu.
 Kikosi cha Wanamaji
 Ndege za kivita zikilinda Ndege ya Rais katika maonyesho ya Ndege yaliofanyika kwenye Kilele cha  Maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano.
 Askari wa kikosi cha Mwamvuli akishuka kutoka futi 4500 kwenye uwanja wa Uhuru kwenye kilele cha miaka 50.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpa mkono wa pongezi mmoja wa wanajeshi wa kikosi cha mwamvuli .
 Maandamano ya Pikipiki.
 Matembezi maalum ya kusheherekea miaka 50 ya Muungano .
Njiwa wakirushwa juu kama ishara ya miaka 50 ya Muungano ambapo watu waliorusha njiwa hao nao wametimiza miaka 50.
Share:

Ijumaa, 25 Aprili 2014

KINANA AKUTANA NA WAZIRI MKUU WA MSUMBIJI JIJINI DAR ES SALAAM LEO

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkaribisha Waziri Mkuu wa Msumbiji, Dk. Alberto Vaquina, kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo April 25, 2014. Baadaye Waziri Mkuu huyo alifanya mazungumzo na Kinana kuhusu masuala mbalimbali hususan ya kisiasa.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkaribisha Waziri Mkuu wa Msumbiji, Dk. Alberto Vaquina, kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, Baadaye Waziri Mkuu huyo alifanya mazungumzo na Kinana kuhusu masuala mbalimbali hususan ya kisiasa.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkaribisha kwa ajili ya mazungumzo, Waziri Mkuu wa Msumbiji, Dk. Alberto Vaquina, kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam,
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa na mgeni wake, Waziri Mkuu wa Msumbiji, Dk. Alberto Vaquina, kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na Waziri Mkuu wa Msumbiji, Dk. Alberto Vaquina (kulia), kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, leo Aprili 25, 2014. Picha zote na Bashir Nkoromo-CCM Blog
Share:

Alhamisi, 24 Aprili 2014

KATIBU MWENEZI WA CHADEMA WILAYA MEATU AHAMIA RASMI CCM

 Aliyekuwa Katibu Mwenezi wa Chadema wilaya ya Meatu Kimwaga Jackson Ndibo akirudisha vitu vya Chadema zikiwemo kadi, bendera na katiba kwa viongozi wa CCM baada ya kurudi rasmi.
 Mwenyekiti wa Vijana  mkoa wa Simiyu na MNEC wa Itilima Ndugu Njalu Silanga akikabdihi kadi ya CCM kwa  moja ya viongozi wa Chadema Meatu waliorudi CCM.
 Mwenyekiti wa Vijana  mkoa wa Simiyu na MNEC wa Itilima Ndugu Njalu Silanga akihutubia wakazi wa wilaya ya Meatu na kuwahakikishia wananchi hao CCM imejipanga kuendelea kuleta maendeleo ya nchini.
Mwenyekiti wa Vijana Mkoa wa Simiyu na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa wilaya ya Itilima Ndugu Njalu Silanga (wa katikati) akiwa pamoja na viongozi wa Chama wilaya ya Meatu.
Share:

MZEE CLEOPA MSUYA ANGA'TUKA RASMI KATIKA UONGOZI WA UMMA

Rais Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza na kuzungumza na Waziri mkuu Mstaafu mzee Cleopa David Msuya aliyetangaza rasmi kung’atuka nafasi zote za uongozi baada ya kuitumikia serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa zaidi ya miaka 33. Mzee Msuya alitangaza hayo katika hafla maalumu iliyofanyika katika Ofisi kuu ya Chama Cha Mapinduzi wilayani Mwanga, jana.
 Mzee Msuya akiteta jambo na Rais Kikwete wakati wa hafla hiyo.
 Mzee Msuya akizungumza na kutangaza kung'atuka rasmi shughuli za uongozi katika Chama na serikali, wakati wa hafla hiyo
 Wazee wa wilaya ya Mwanga wakimkabidhi Mzee Cleopa David Msuya zawadi mbalimbali na kumkaribisha kijijini wakati wa hafla ya kumuaga kama kiongozi iliyofanyika katika ofisi kuu ya CCM Wilayani Mwanga jana
 Mzee Msuya akifurahia jambo
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri Mkuu mstaafu  Mzee Cleopa David Msuya wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine wa Chama na Serikali wakati wa hafla ya kumuaga iliyofanyika katika ofisi kuu ya CCM mjini Mwanga,Mkoani Kilimanjaro jana  ambapo Mzee Msuya alitangaza kung’atuka rasmi kutoka nafasi zake zote za uongozi wa umma.Wengine katika picha walioketi mbele kutoka kushoto ni Mkuu wa mkoa wa KilimanjaroBwana Leonidas Gama,Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana, na kulia ni Wziri wa maji mbaue pia ni mbunge wa Mwanga Profesa Jumanne Maghembe.Picha zote na Ikulu.
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu