Unordered List


DR.SLAA HATA HAYA MADOGO UNAWEZA?

Wednesday, April 2, 2014
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kufyatua matofali kwa ajili ya ujenzi Ofisi ya CCM, wilaya mpya ya Kalambo, Aprili 2, 2014, Ofisi hiyo ipo mji mdogo wa Matai mkoani Rukwa jana. Kinana yupo katika mkoa wa Rukwa kwa ajili ya kukagua uhai wa Chama, Utekelezaji wa ilani ya chama na kusikiliza kero za wananchi na kujadili nao njia ya kuzipatia ufumbuzi.
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipanga matofali baada ya kushshiriki kufyatua matofali kwa ajili ya ujenzi Ofisi ya CCM, wilaya mpya ya Kalambo,  Ofisi hiyo ipo mji mdogo wa Matai mkoani Rukwa Aprili 2, 2014.
 Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akiondoka kwenye Ofisi ya CCM wilaya mpya ya Mkalamo baada ya kushiriki ufyatuaji matofali kwa ajili ya kuboresha jengo la ofisi hiyo. Watatu kulia ni Mjumbe wa NEC, Balozi Ali Karume ambaye amefuatana na Kinana katika ziara ya mkoa wa Rukwa.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumza na Mjumbe wa shina namba moja, Apolinary Kibiko, alipofika kwenye shina hilo, katika kijiji cha Matai, wilaya mpya ya Kalambo mkoani Rukwa, Aprili 2, 2014.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi katika mkutano uliofanyika kwenye shina namba mbili la mjumbe, Daudi Nkaisi (kushoto), katika mji mdogo wa Matai, wilaya mpya ya Kalambo mkoani Rukwa, Aprili 2, 2014.
 Mbunge wa Kalambo Josephat Kandege akisalimia wananchi, Kinana alipowasili katika shina namba mbili, katika Kijiji cha Matai, wilaya mpya ya Kalambo, Aprili 2, 2014,
 Wananchi wakishangilia Kinana alipozungumza nao kwenye shina namba moja, katika Kijiji cha Matai wilaya ya Kalambo, Aprili 2, 2014,
 Wananchi wakimshangilia Kinana alipozungumza nao kwenye shina namba mbili katika kijiji cha Matai
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiingia ukumbini kuzungumza na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, Aprili 2, 2014
 Msafara wa Kinana ukienda Kijiji cha Kasanga kilichopo mwambao wa ziwa Tanganyika katika wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, Aprili 2,2014
 Wananchi wakijimwayamwaya kwenye mkutano wa Kinana uliofanyika kijiji cha Kasanga, wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, Aprili 2, 2014.
 Kinana akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kasanga kilichopo mwambao wa ziwa Tanganyika katika wilaya mpya ya Kalambo mkoani Rukwa, Aprili 2, 2014
 Mabinti wa kijiji cha Kalambo kilichopo mwambao wa ziwa Tanganyika, wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa akifurahia kurekodi matukio ya mkutano wa Kinana kwa kutumia simu zao, alipohutubia katika kijiji hicho, Aprili 2, 2014. Licha ya kuwa pembezoni Kijiji cha Kalambo ni miongoni mwa vijiji vinavyopata mtandao wa mawasiliano ya uhakika ya simu za mkononi.
 Mama akimyanyua mtoto wake apate kumuona Kinana alipohutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kalambo, Aprili 2, 2014.
Kijana Ramadhani Ali wa Kijiji cha Kasanga kilichopo mwambao wa ziwa Tanganyika katika wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa akitoka ziwani na samaki wake aina ya migebuka. Picha zote na Bashir Nkoromo wa CCM Blog

Chapisha Maoni

1 Maoni