Alhamisi, 17 Aprili 2014

KINANA AMALIZA ZIARA YAKE MKOANI KATAVI


 Kattibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikagua mradi wa ujenzi wa nyumba zinazojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa katika wilaya ya Mpanda mkoani Katavi ambapo nyumba 70 zimekamilika kati ya 90 zitakazojengwa wilayani hapo.
 Nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa zinazojengwa katika wilaya ya Mpanda mkoani Katavi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishuka kwenye ngazi baada ya kukagua mradi wa maji wa Ikorongo,Katibu mkuu ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa Balozi Ali Abeid Karume,mradi huu utakamilika mwezi juni 2014.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kutandaza mabomba kwenye mradi wa maji wa Ikorongo wilayani Mpanda mkoani Katavi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa Mpanda mjini kwenye uwanja wa shule ya Msingi Kashaulili na kuwapongeza kuwa wachapakazi hodari katika kusimamia maendeleo yao na kuwataka kuwa makini na wanasiasa kwani mwisho wa siku hoja zao haziwasaidii wao kwenye maisha yao ya kila siku.
 Katibu wa NEC Itkadi na Uenezi Nape Nnauye akipiga gitaa baada ya kumaliza mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Kashaulili wilayani Mpanda.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wakazi wa shina namba 32 Makanyagio Mpanda na kuwasihi wakazi hao kuchagua viongozi sahihi na wenye sifa za kuwaongoza.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimia wakazi wa shina namba 32 Makanyagio wilaya ya Mpanda walipomtembelea Balozi wa Shina Ndugu Tobias Kazimzuri.
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu