Unordered List


NCHI ZIMILIKI MAGEUZI YA SEKTA ZA USALAMA: TANZANIA


Na Mwandishi Maalum
Tanzania,  imeungana na mataifa mengine katika kusisitiza umuhimu wa nchi kumiliki mchakato wa Mageuz iya Sekta za Usalama ( Security Sector Reform).
Akichangia majadiliano ya Baraza Kuu la Usalama  la Umoja wa Mataifa ambalo lilikutana kwa siku nzima ya Jumatatu  wiki hii, kujadili taarifa ya Katibu Mkuu kuhusu SSR,  Naibu Mwakilishiwa Kudumu wa Tanzania katika  UN, Balozi Ramadhan Mwinyi amesema, Tanzania kama ilivyo kwa nchi nyingine nyingi inapenda kuona kwamba mageuzi ya sekta za usalama yanamilikiwa na nchi zenyewe zikiwamo nchi zinazotoka katika machafuko.
Katika Mkutano huo, Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, lilipitisha kwa kauli moja na kwa mara ya kwanza Azimio linalojitegemea kuhusu mchakato wa Mageuzi ya Sektaza Usalama,kupitia azimio hilo namba 2151 (2014)  pamoja na kusisitiza umuhimu wa dha nazima ya mageuzi ya sekta za usalama na umuhimu wake kwa usalama, amani na ustawi wa mwanadamu.
 Azimio linasisitiza kwamba umiliki wa nchi katika mageuzi hayo ni jambo la muhimu.
Akaongeza kuwa makundi ya wapiganaji na ambao wameka silaha zao chini na kuingia katika mchakato wa majadiliano wanapaswa pia kuwa sehemu ya mageuzi ya sekta za usalama.
Akasema kwa kuyashirikisha makundi hayo ya wapiganaji na mengine kutasaidia ujenzi wa Amani na usalama na pia kuepusha kujirudia kwa mapigano.
Aidha Balozi Mwinyi, ameleza kwamba, nchi zinazopakana na nchi zinazotoka kwenye machafuko pia zinayo nafasi na wajibu wa kutoa ushirikiano na uzoefu wao katika ujenzi wa sekta za usalama.
Vile vile Balozi amebainisha kwamba katika miongo ya miaka mitano iliyopita imedhihirisha wazi umuhimu wa jumuia za kikanda katika uzuiaji wa mapigano, ulinziwa Amani naujenziwa Amani.
Majadiliano hayo yalifunguliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na yaliitishwana Nigeria ambayo ni Rais wa Baraza hilo kwa Mwezi huu wa April. Waziri wa Mambo ya Nje wa Nigeria  Bw. Aminu Wali aliongoza majadiliano.
Wawakilishi kutoka nchi 42 wanachama waUmojawa Mataifa, zilizungumza wakati wa majadiliano kuhusu dhana hiyo ya mageuzi ya sektaza usalama, na bila ya kujali tofauti zao,  kila moja ilisisitiza hoja ya nchi kumiliki mchakato huo hata kwa zile ambazo zimetoka katika machafuko au mapigano.
Aidha pamoja na kusisitiza haja na umuhimu wa nchi kumiliki mchakatohuo, zimeongeza kuwa bado kuna haja ya Jumuiya ya Kimataifa,  kuziwezesha nchi hasa zile zinazotoka katika machafuko kuweza si kujenga upya sekta hizo za usalama bali pia kuzifanyia mageuzi.
Vile vile ilisisitizwa pia kuwa mageuzi hayo ya sekta za usalama ni muhimu katika kuziimarisha nchi ambazo ndiyo kwanza zimetoka kwenye machafuko. Na kwamba mageuzi hayo yatapewa kipaumbele katika utekelezaji mamlaka za ulinzi wa Amani  na misheni maalum za Kisiasa.
Wajumbe wengine walikwenda mbalizaidi, kwa kueleza kwamba mageuzi hayo ya sektza za usalama yanapashwa kuwajumuishi kwa maana ya kushirikisha makundi mengine ya kijamii. Lakini kwa msisitizo kwamba serikali ndiyo iwe na mamlaka ya kuamua mfumo wa sekta zake za usalama.
Katika salamu zake za ufunguzi Ban ki Moon,  alisema,  lengo la kutekeleza mageuzi ya sekta za usalama ambazo ni pamoja na jeshi, polisi na vyombo vya usalama ni kuwawezesha wananchi ambao ndiyo walengwa kuishi maisha yenye usalama.

“Sektaza Usalama ndiyo muhimili mkuu wa makubaliano kati ya serikali na wananchi wake. Mamlaka ya kutumia nguvu nilazima yaendane na wajibu wa kulinda raia na kuheshimu haki za binadamu” akasemaKatibuMkuu.
Kwa mujibu wa Ban Ki Moon,  sekta za usalama zinazotekeleza majukumu yake chini ya misigi ya utawala wa sheria zina uwezo wa kuimarisha imani ya wananchi kwa serikali yao na hivyo kuchangia katika uimara wa ujenzi wa Amani namaendeleo.

Chapisha Maoni

0 Maoni