Alhamisi, 15 Mei 2014

DHULUMA KWA WAKULIMA WA TUMBAKU YAMHUZUNISHA KINANA


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Mgambo kitongoji cha Lukula  kata ya Kitunda wilayani Sikonge mkani Tabora ambapo aliwaomba radhi wakulima wa Tumbaku kwa kadhia waliyo nayo kutokana na kunyonywa na kutopata haki zao za malipo kwa miaka 3.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Mbunge wa Jimbo la Sikonge Said Mkumba wakiwasomea wananchi wa kijiji cha Lukula maeneo yatakayopata umeme mwaka huu katika wilaya ya Sikonge.
 Mbunge wa Jimbo la Sikonge Said Mkumba akihutubia wananchi wa kijiji cha Lukula kata ya Mgambo na kuwaambia wale wote waliodhulumu wakulima wanatakiwa kuchukuliwa hatua na pia alisisitiza sheria zingatiwe za wanasiasa kutojihusisha na masuala ya vyama vya ushirika.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipitia taarifa mbali mbali kabla ya kuhutubia wakazi wa kata ya Mgambo,Katibu Mkuu wa CCM amehuzunishwa sana na baadhi ya viongozi wa Serikali kutofika kwa wananchi na kujua matatizo yao badala yake wamesababisha wananchi kuumia sana.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya ujenzi wa jengo la upasuaji na Dk.Silvanus Kabutura Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya cha Kata ya Kitunda wilayani Sikonge,Daktari Kabutura  alimueleza Katibu Mkuu wa CCM changamoto kubwa uhaba wa maji katika kituo hicho.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akitoka kukagua jengo la upasuaji la kituo cha afya cha Kitunda wilayani Sikonge mkoani Tabora ambalo limechelewa kukamilika kwa zaidi ya mwaka mmoja na huku Wizara ya Afya kushindwa kuchukua hatua mpaka sasa .
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu