Unordered List


KINANA AANZA ZIARA YA SIKU 10 MKOA WA TABORA

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasili kwenye kijiji cha Makomero wilaya ya Igunga kwa ziara ya siku 10 mkoani Tabora ambapo atakagua miradi ya maendeleo ikiwa pamoja na kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Nzega Dk.Hamisi Kigwangala mara baada ya kuwasili Igunga tayari kwa ziara ya mkoa wa Tabora,Katibu Mkuu ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Tabora Munde Tambwe .
 Wananchi wakiwa na nyuso za furaha wakati wa mapokezi ya Kinana.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakisalimiana na wananchi wa Tabora mara baada ya kuwasili Wilaya ya Igunga kwa ziara ya siku 10.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Kada wa CCM Mussa Tesha.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Makomero mara baada ya kuwasili kwenye wilaya ya Igunga.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimia wananchi wa kijiji cha Makomero wilaya ya Igunga mara baada ya kuwasili mkoani Tabora ambapo anategemea kufanya ziara ya siku 10 mkoani hapa.

Chapisha Maoni

0 Maoni