Unordered List


KINANA AMALIZA ZIARA YAKE WILAYA YA MBULU KWA MAFANIKIO

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Mbulu na kuwataka kutumia muda mwingi kwenye shughuli za kimaendeleo kwa kushirikiana na serikali.Katibu Mkuu alisisitiza serikali kuchukua hatua za haraka kwa wale wote waliojichukulia mali ya serikali bila utaratibu hasa nyumba za madaktari.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Mbulu na kuwaambia vyama vingi vya upinzani vinakufa kwa sababu ya kuwa na sera zisizoaminika kwa Watanzania na ameshukuru kwa Watanzania wengi kuelewa hilo kiasi cha kurejea CCM.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wanakijiji cha Bashei ambao walimueleza kuwa wanalima sana kitunguu saumu lakini soko si zuri na kumuomba awasaidie kutafuta soko la kdumu, tatizo jingine ni ucheleweshaji wa kujenga bwawa la maji, Katika ziara hizi za Katibu Mkuu wananchi wamekuwa na imani kubwa na CCM kwa ushirikiano wanaoupata kwani majibu ya maswali yao yanakuwa ya kuridhisha.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Anatory Choya akijibu maswali ya wananchi wa Yaeda Chini ambao wamekuwa wakivamiwa na kufukuzwa kwenye ardhi yao,Mkuu wa Wilaya alisema kwanza walishaweka mipango ya matumizi bora ya ardhi kuondoa migogoro ya wakulima na wafugaji ,pili atafanya jitihada za dhati kuwakamata wale wote wanaofukuza na kunyanyasa wananchi wengine kwenye masuala ya ardhi.
Diwani wa Kata ya Eshkesh kutoka chama cha CUF Ndugu Naftal Z Kihandu akishukuru kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwa kuwasikiliza wananchi wa kata yake na kufungua njia kwa kuchangia mabati na saruji kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa nyumba ya mwalimu wa shule ya sekondari Yaeda chini.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Hydom na kuwaambia wapunguze muda na mambo ya siasa ,watumie muda mwingi kushikama na kujenga maendeleo yao.
 Wananchi wa Hydom wakinyoosha mikono yao kuunga mkono jitihada za CCM katika kuleta maendeleo nchini.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kadi ya Chadema iliyorudishwa kwake na aliyekuwa Katibu wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA) Victoria Mshanga ambaye amjiunga rasmi na CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Hydom.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akipiga picha ya wanakijiji cha Eshkesh pamoja na Richard Mwaikenda maarufu kama Kamanda wa Matukio,Wananchi wa Eshkesh wanashida ya maji na Zahanati ambapo maji yatapatikana karibuni kutokana na mipango ya halmashauri lakini zahanati pia itaanza kujengwa baada ya Katibu Mkuu wa CCM kuhamasisha kwa kuanza kuwachangia mabati na Simenti na halmashauri na wanakijiji hao wataongezea nguvu kukamilisha.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongea na watumishi na wanafunzi wa uuguzi wa Hospitali ya Hydom .Katibu Mkuu aliupongeza Uongozi pamoja na Watumishi wa hospitali hiyo kwa kazi nzuri wanayoifanya hasa katika kupunguza vifo vya mama na mtoto.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wakati wa ujenzi wa daraja la Qorong'aida linalounganisha Kilimapunda na Kidarafa na linategemewa kugharimu zaidi ya bilioni moja.

Chapisha Maoni

0 Maoni