Jumamosi, 10 Mei 2014

KINANA: VIONGOZI WAJIFUNZE KUTOKA KWA WANANCHI


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Igunga kwenye viwanja vya Sokoine na kutaka Viongozi wajifunze kutoka kwa wananchi ili waendane na kasi ya mabadiliko.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Igunga waliojitokeza kwa wingi kwenye viwanja vya mikutano vya Sokoine na kuwaambia wanasiasa waache kuwababaisha watu na suala la muundo wa serikali badala yake waje na hoja zinazogusa maisha ya kila siku mfano changamoto la mbegu za Pamba ,Afya na maendeleo kwa ujumla.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimpokea wanachama mpya wa CCM ambaye alikuwa Katibu wa CUF wilaya ya Igunga Malko Maganga Katamija ,zaidi ya watu 20 wamerjea CCM kutoka vyama vya CUF na Chadema.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisoma mabango yenye ujumbe mbali mbali wakati akiwasili kwenye uwanja wa mkutano wa Sokoine,kulia kwake ni Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Tabora Munde Tambwe

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia ua la Alizeti kwenye shamba la mradi wa kilimo la Vijana katika kijiji  cha Iborogelo kata ya Ziba mkoani Tabora ambapo hekari 25  zimelimwa na vijana kwa kutumia jembe la plau.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionja alizeti kwenye shamba la mradi wa kilimo kwa vijana wilayani Igunga kwenye kijiji cha Iborogelo kata ya Ziba.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa katikati ya shamba la alizeti ambalo ni mradi wa vijana wilayani Igunga na ni moja ya mpamgo wa serikali wa matokeo makubwa sasa.


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Igunga Ndugu Elibariki Kingu,Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Igunga Ndugu Costa Olomi na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakiwa kwenye picha ya pamoja na vijana wanaoshiriki kwenye mradi wa kilimo cha alizeti katika Kijiji cha Ibologero,kata ya Ziba wilaya ya Igunga baada ya kutembelea na kujionea shamba lililolimwa na vijana hao.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimkabidhi kadi ya uanachama wa NSSF Bi.Zawadi Zakaria Magira ,Katibu Mkuu aligawa kati 15 kati ya 250 ya wanachama wapya waliojiunga na NSSF wilayani Igunga.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kama ishara ya kukabidhi matrekta kwenye vikundi vya wakulima wa kawaida ambavyo vinadhaminiwa na Vijana Saccos Igunga.
 Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akijaribu trekta mojawapo kabla ya kulikabidhi rasmi kwa vikundi vya wakulima wa kawaida ambao wamedhaminiwa na Saccos ya Vijana Igunga, wananchi wa Igunga asilimia 90 ni wakulima na 10 ni wafanyakazi.Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akinunua mahindi ya kuchoma kwenye mitaa ya Igunga mjini baada ya kumaliza kuhutubia mkutano mkubwa wa hadhara.
(Picha na Adam H.Mzee)
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu