Unordered List


DK. ASHA-ROSE MIGIRO ATINGA KWA KISHINDO OFISI ZA UMOJA WA MATAIFA NCHINI MAREKANI

 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki  Moon akiwa  na Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja huo, ambaye sasa ni Waziri wa Sheria na Katiba wa Tanzania, Dk. Asha-Rose Migiro (Mb), Walipokutana Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani, jana Jumatatu.
        Hii  ni mara ya kwanza kwa Dk. Asha-Rose kufika  Umoja wa Mataifa tangu alipostaafu Unaibu Katibu Mkuu miaka miwili  iliyopita.
       Kabla ya  Viongozi hao wawili kupiga picha hii rasmi, walikuwa na mazungumzo ya faragha.
       Waziri Dk. Asha-Rose, yupo Umoja wa  Mataifa kuhudhuria mkutano ulioitishwa na  Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu  mchango wa  Haki za Binadamu na  Utawala wa Sheria katika   Maendeleo  Endelevu baada ya 2015    
 Naibu Katibu Mkuu  Mstaafu akipokea shada la Maua  kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa  Ofisi Binafsi ya Katibu Mkuu. Ujio wa   Dkt Migiro, uliamsha shamra shamra zaina yake kutoka kwa Katibu Mkuu mwenyewe ambaye  kila wakati alikuwa akiachia tabasamu pana, Baraza lake la Mawaziri pamoja na wafanyakazi wa ofisi yake Binafsi pamoja na ofisi Binafsi ya Naibu Katibu Mkuu.
" Hili  ua zito ngoja tukupokee" ndivyo wanayoelekea kusema  Katibu Mkuu Ban Ki Moon na Mkuu wake wa Itifaki.
 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  Ban Ki Moon na timu yake akiwa ukumbini katika mazungumzo na Dk. Asha- Rose Migiro ambaye alifuatana na    Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa  Mataifa  Balozi Tuvako Manongi na Naibu wake, Balozi Ramadhan Mwinyi.  Katika  mazungumzo hayo,  Katibu Mkuu alisema, Rais Jakaya Mrisho Kikwete amefanya jambo jema kumteua Dkt. Asha-Rose  Migiro kwanza kuwa mbunge na kisha kumteua kuwa  Waziri anayeshughulikia  Sheria na Masuala ya Katiba, akasema uzoefu wake na mchango wake  siyo tu kwamba ni muhimu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bali ni muhimu pia katika Jumuiya ya Kimataifa.  Ban Ki Moon alishindwa kuficha hisia zake pale aliposema mbele ya  Maofisa  wake kwamba  siku zote amekuwa akimkumbuka Asha- Rose Migiro na kwamba amefurahi sana kwamba amepata nafasi yakufika  Umoja wa Mataifa
 " welcome back" ndivyo anayosema afisa huyu wakati wakisalimia kwa furana ha  Naibu  Katibu Mkuu Mstaafu  Dk..  Asha-Rose Migiro huku Katibu Mkuu akiangalia  kwa furaha
Salaam za kumlaki Dk. Asha-Rose zikiendelea kwa kila aina ya bashasha
  Ban Ki Moon akiagana na  Dkt. Asha-Rose Migiro baada ya  mazungumzo yao
 Naibu Katibu Mkuu, Bw. Jan Eliasson akimkumbatia kwa furaha Dk. Asha- Rose Migiro kabla ya kumkaribisha ofisi kwake kwa mazungumzo
 Wakielekea ofisini kwa mazungumzo
 Naibu Katibu  Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Jan Eliasson akiwa na  Dkt. Asha- Rose Migiro. Bw. Eliasson alimueleza   Naibu Katibu Mkuu  Mstaafu kwamba anajitahidi kufuata nyayo zake na kwamba anayo mapenzi makubwa sana na  Tanzania  na Afrika kwa Ujumla,  Bw. Eliasson aliwahi kufanya kazi  Tanzania   kama  mwanadiplomasi chini ya  Uongozi wa Rais wa wakati huo wa Sweden   Marehemu  Olof Palme
  Dkt. Asha- Rose Migiro akiagana na  Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Jan Eliasson ( Leo Jumanne ) Waziri wa Sheria na Masuala ya Katiba Dkt. Asha- Rose Migiro ( Mb) atakuwa miongoni wa wanajopo ( Panellist) watakaoendesha  majadiliano kuhusu  mchango wa haki za binadamu na utawala wa sheria katika uungaji mkono juhudi za kitaifa na kimataifa  katika kuutokomeza umaskini na  maendeleo endelevu. Majadiliano hayo ni sehemu ya mkutano wa siku mbili ambao umeitishwa na   Rais wa Baraza  Kuu la Umoja wa Mataifa  Bw. John Ashe na  kufunguliwa na Katibu Mkuu  Ban Ki Moon.
 Picha zote na  Mpigapicha Maalum, UN

Chapisha Maoni

0 Maoni