Jumatatu, 16 Juni 2014

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHUDHURIA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA NCHI ZA G77 NA CHINA JIJINI SANTA CRUZ, BOLIVIA


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokewa na wenyeji wake wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Bolivia juzi Juni 13, 2014 kwa ajili ya kuhudhuria maadhimisho ya miaka 50 ya Nchi za G 77 na China, yanayofanyika leo Juni 15, 2014, jijini Santa Cruz, Bolivia. Picha na OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Meya wa Jiji la Santa Cruz,  Percy Fernandez, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Bolivia juzi Juni 13, 2014 kwa ajili ya kuhudhuria maadhimisho ya miaka 50 ya Nchi za G 77 na China, yanayofanyika leo Juni 15, 2014, jijini Santa Cruz, Bolivia. Kushoto ni Mama Zakhia Bilal. Picha na OMR

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Rais wa Bolivia, Evo Morales, walipokutana kabla ya kuhudhuria maadhimisho ya Miaka 50 ya nchi za G77 na China yanayofanyika jijini Santa Cruz, Bolivia, jana Juni 14, 2014. Katikati ni Mkalimani wa Rais wa Bolivia. Katika mazungumzo hayo Rais Morales aliishukuru Tanzania kushiriki katika maadhimisho haya na akasisitiza kuwa uhusiano wa nchi za G77 unapaswa kuenziwa huku Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Bilal akifafanua kuwa Tanzania inatambua na kuheshimu jitihada zinazofanywa na umoja huo na kwamba ni kipindi kizuri kuadhimisha miaka 50 kwa kutafakari kuhusu kutanua fursa za kukuza uchumi ili kuendeleza wananchi wa nchi hizo. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jmahuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiagana na Mwenyeji wake Rais Evo Morales, Rais wa Bolivia baada ya kufanya mazungumzo saa chache kabla ya kuhudhuria Maadhimisho ya Miaka 50 ya nchi za G77 na China yanayofanyika jijini Santa Cruz, Bolivia. Katika mazungumzo hayo Rais Morales aliishukuru Tanzania kushiriki katika maadhimisho haya na akasisitiza kuwa uhusiano wa nchi za G77 unapaswa kuenziwa huku Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Bilal akifafanua kuwa Tanzania ni inatambua na kuheshimu jitihada zinazofanywa na umoja huo na kwamba ni kipindi kizuri kuadhimisha miaka 50 kwa kutafakari kuhusu kutanua fursa za kukuza uchumi ili kuendeleza wananchi wa nchi hizo. Picha na OMR
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu