Unordered List


MTEMVU: WAPINZANI HATA WAKIUNGANA CCM ITAWABWAGA, AWASHANGAA WANAOMSEMA KUWA ANA MASLAHI BINAFSI KUTETEA MAMALISHE TEMEKE

NA BASHIR NKOROMO, TEMEKE


BUNGE wa Temeke Abbas Mtemvu amewananga wapinzani akisema hata wakisimamisha mgombea mmoja mmoja, katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015, CCM itawabwaga.

Amesema, uhakika huo anao na hata wapinzani wenyewe wanajua hilo, kwa kuwa hawaizidi CCM kwa weledi wa kisiasa, kwa akili wala wingi wa wanachama.

Mtemvu amsema hayo wakati akifungua kikao cha Baraza Kuu la Jumuia ya Wazazi Wilaya ya Temeke, kilichofanyika leo, Juni 27, 2014, kwenye Ukumbi wa Manispaa ya wilaya hiyo, mjini Dar es Salaam.

"Wapinzani baada ya kuona kuwa hawatuwezi kwa kila chama kivyake, sasa mnaona wanavyotapatapa, mara eti huo Ukawa walioanzisha wanataka pia kuutumia kwenye chaguzi, kuweka mgombea mmoja mmoja kwa wote, mimi bado naamini hata wafanyeje CCM itawabwaga tu", alisema Mtemvu.

Mtemvu alisema, pale ambapo wapinzani wamekuwa wakipenya na kunyakuwa ubunge au udiwani ni pale ambapo CCM wenyewe wanakuwa wamejichanganya.

"Ikifika acheni mambo ya kuanza mizozano ya ndani kwa ndani kutokana na makundi ambayo husababishwa na baadhi ya wagombea au wanachama wanaowataka wagombea kwa lazima, tukiachana na hili nawahawakikhieni wapinzani hawapati hata kiti kimoja cha cha mtaa", alisema Mtemvu.

Mtemvu aliwataka wana-CCM pia kuachana na mambo ya kushughulika tu na wanaotaka nafasi ambao wana fedha, akisema, kufanya hivyo kunasababisha baadhi kuwa wagombea kutokana na uwezo wa fedha tu na siyo wa uongozi.

Aliwataka mtu anapowajia kwa fedha kuzipokea na kuzila, lakini wakati waanapofikia maamuzi muhimu kwenye uchaguzi wahakikishe wanachagua yule wanayemfahamu kwa thati kwamba anao uwezo wa uongozi.

Alisema, wapo baadhi ya wanachama wa CCM wanao uwezo wa kuongoza lakini hawana fedha, hivyo watu wa aina hiyo wasitoswe kwa sababu ya ufukara wao.

Mtemvu alisema kiongozi mwenye uwezo ni yule anayekubalika na watu, saa zote yupo na watu na anajali maslahi ya wanyonge siyo wale anaowajua kuwa ni wake tu.

"Mfano ni kama hivi tunavyofanya sasa wabunge wa mkoa wa Dar es Salaam. Kila mara tunapigania wanyonge, juzi nimepambana kuwatetea mamalishe wasifukuzwe hovyo, japo baadhi ya watu tena waliopewa malmaka na Rais waknibeza eti nina maslahi binafsi, khaa, yaani mimi niwe na maslahi na mamalishe huu kama siyo uzushi ni nini?" alisema Mtevu.
 Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu akifungua Kikao cha Baraza Kuu la Jumuia ya Wazazi ya CCM, wilaya ya Temeke, leo katika ukumbi wa Manispaa ya wilaya hiyo jijini Dar es Salaam.
 Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu ambaye pia ni Mjumbe wa NEC, akimkabidhi hati ya pongezi , Zaitun Lukinga, ya kuwa kiongozi wa Jumuia ya Wazazi awamu zaidi ya moja katika nafasi ya Katibu wa Jumuia ya wazazi Kata ya Kurasini, wakati wa mkutano huo leo
 Washiriki wakiwa kwenye mkutano huo. Habari Picha na Bashir Nkoromo- CCM Blog

Chapisha Maoni

0 Maoni