Unordered List


MWENYEKITI WA CHADEMA AHAMIA CCM IRINGA

 Mwenyekiti wa Chadema katika kata ya Ihimbo Jimbo la Kilolo, Iringa Vijijini,Seleman Kiponda  akikabidhi kadi ya Chadema kwa Katibu wa CCM mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga, baada ya kutangaza kuhamia CCM makabidhiano yaliyofanyika katika ofisi za CCM mkoa wa Iringa.
 Mwenyekiti wa Chadema katika kata ya Ihimbo Jimbo la Kilolo, Iringa Vijijini,Seleman Kiponda  akikabidhi bendera ya Chadema kwa Katibu wa CCM mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga, baada ya kutangaza kuhamia CCM makabidhiano yaliyofanyika katika ofisi za CCM mkoa wa Iringa.
 Mwenyekiti wa Chadema katika kata ya Ihimbo Jimbo la Kilolo, Iringa Vijijini,Seleman Kiponda  akizungumza nia yake ya kuhamia CCM.

diwani wa kata ya Ihimbo Hezron Nganyagwa akimkabidhi bendera ya CCM aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema kata ya Ihimbo katika jimbo la Kilolo Selemani Kipondi.

 Katibu wa CCM mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga akizungumza wakati wa kumkaribisha aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema katika kata ya Ihimbo Jimbo la Kilolo,Seleman Kiponda baada ya kuhamia CCM katika ofisi za ccm mkoa wa Iringa.

Na Denis Mlowe, Iringa

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kata ya Ihimbo jimbo la Kilolo  mkoani Iringa,Selemani Kiponda ameamua kuachana na chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kukosa ushirikiano na uongozi wa juu.
 
Kiponda alifikia uamuzi huo juzi kwa kile alichosema amekuwa kiongozi wa chadema kwa  miaka minne na ameweza kushawishi wakazi wengi katika maeneo mbalimbali katika kata ya Ihimbo kujiunga na  chama hicho lakini hawajawahi kupata ushirikiano kutoka uongozi wa juu wa chama wa mkoa hadi taifa.
 
“Nilijiunga na Chadema mwaka 1993 wakati ndio kwanza upinzani umeingia nchini na nimekuwa kiongozi kwa miaka zaidi ya minne lakini hakuna ushirikiano kutoka uongozi wangu hivyo nimerudi ccm kwa kuwa ndio chama changu ambacho kwa kweli nilikuwapo tangu enzi za Tanu na hivyo kwa hiari yangu nimeamua kurudi ndani ya chama makini na chenye sera zenye kueleweka” alisema Kiponda”
 
Aidha alisema kuwa hatua ya yeye  kurudi CCM imetokana na maendeleo yanayofanywa na diwani wa kata hiyo Hezron Nganyagwa pamoja na mbunge wa jimbo la kilolo profesa Peter Msola kwa kuwa ushirikiano umekuwa mkubwa kuliko ambavyo sikutegemea uwepo kwa kuwa nilikuwa chama cha upinzani.
 
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa CCM mkoa wa Iringa, Hassan Mtenga alisema Kiponda amefanya maamuzi sahihi ya kurudi CCM kwa kuwa muda mrefu amekuwa Chadema hivyo ameona tofauti iliyoko miongoni mwa vyam hivyo pinzani.
 
Mtenga alisema kuwa viongozi na wanachama wa CCM  wataendeleza ushirikiano katika kuwarudisha wanachama wa Chadema wengine waliobaki Ihimbo kwa kuwa kimefanikiwa kuwaunganisha wananchi katika kujiletea maendeleo kutokana na uongozi imara wa chama hicho.
 
Naye diwani wa kata ya Ihimbo Hezron Nganyagwa aliahidi kutoa ushirikiano katika shughuli za maendeleo kama ilivyokuwa mwanzo walipokuwa wakishirikiana ingawa walikuwa wapinzani.
 
Kurudi kwa kiongozi huyo kunaongeza idadi ya wanachama  wanne waliohama Chadema hadi sasa wakiwemo Katibu wa Chadema jimbo la Mufindi Kusini, Emannuel Ngwalanje, Zawadi Waziri Shombe ambaye alikuwa ni mjumbe wa oparesheni ya M4C Nyanda za Juu Kusini, pamoja na Bernado Lugenge.

Chapisha Maoni

0 Maoni