Jumapili, 15 Juni 2014

NAPE AITEKA KIMARA BARUTI


 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akipokelewa kishujaa baada ya kuwasili eneo la mkutano Kimara Baruti,mkutano huo ulioandaliwa na Jumuiya ya Wazazi CCM Kata ya Kimara ,wilaya ya Kinondoni.
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akiwapungia wananchi mkono wakati akiwasili eneo la mkutano kwenye viwanja vya mbele ya ofisi za TRA kimara Baruti.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akipiga Gitaa kabala ya kupanda jukwaani kuhutubia wakazi wa Kimara Baruti.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Ramadhani Madabida kabla ya kupanda jukwaani na kuhutubia wakazi wa Kimara Baruti.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa Kimara Baruti kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mbele ya ofisi za TRA Kimara Baruti ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa tatizo kuwabwa la foleni linadhoofisha uchumi hivyo linatakiwa kupatiwa ufumbuzi mara moja,pia alisema atazungumza na viongozi wa ngazi za juu wa CCM kuwapa kipaumbele wakazi wa Ubungo na Kawe waweze kupata maji mwanzoni katika miradi ya maji inayokuja.
 Baadhi ya Wana CCM waliohudhuria mkutano huo wa hadhara uliofanyika Kimara Baruti.
 Baadhi ya Wana CCM waliohudhuria mkutano huo wa hadhara uliofanyika Kimara Baruti wakimsikiliza kwa makini Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye alipohutubia wakazi wa Kimara Baruti leo.
 Hamida Issa Selemani akielezea umati wa wakazi wa Kimara uamuzi wake wa kujiunga na CCM baada ya kuchoshwa na siasa chafu za chama cha  CUF.Hamida alishakuwa Diwani na Kaimu Katibu wa CUF Wilaya ya Biharamulo na mgombea Ubunge wa CUF jimbo la Biharamulo Magharibi
 Rashid Idd aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF wilaya ya Biharamulo akimpa mkono Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye baada ya kutangaza kujiunga rasmi na CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kimara Baruti.
  Rashid Idd aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF wilaya ya Biharamulo pamoja na Hamida Issa Selemani na wanachama wengine zaidi ya 420 wakila kiapo cha kuwa wanachama watiifu wa CCM Jumuiya ya Wazazi.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiondoka eneo la mkutano akiongozana na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni Ndugu Salum Madenge.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiagana na wakazi wa Kimara Baruti mara baada ya kumaliza mkutano wa hadhara .
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Ndugu Nape Nnauye akicheza bao na Bi Agustina Batromeo mara baada ya kuzindua shina namba 770 la wacheza bao Kimara Baruti.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akipandisha Bendera ya Chama baada ya kufungua shina la wakereketwa wa CCM Gereji Butcher. Zaidi ya mashina manne ya Jumuiya ya Wazazi CCM yamefunguliwa leo na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi katika kata ya Kimara.
(Picha na Adam Mzee)
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu