Jumatano, 11 Juni 2014

TWAWEZA YATUNUKU TUZO WAANDISHI 37 KWA MAONI YAO KUHUSU KUBORESHA UTOAJI HUDUMA SEKTA ZA ELIMI, AFYA NA MAJIDAR ES SALAAM, Tanzania
Twaweza, kama sehemu ya kazi zake kwenye Mpango wa kuendesha shughuli za serikali kwa uwazi (OGP), imetoa tuzo za kompyuta (aina ya laptops) na taa zinazotumia nishati ya jua kwa waandishi 37 kutokana na mawazo yao juu ya namna Serikali na wananchi wanavyoweza kuboresha utoaji huduma kwenye sekta za elimu, afya na maji.

Shindano hili la kutafuta maoni ya wananchi lilizinduliwa kwa ushirikiano wa Twaweza pamoja na Serikali ya Tanzania mwezi Desemba 2012.

Twaweza iliisaidia Serikali kukusanya maoni haya kwa kusambaza taarifu kuhusu shindano hili na maelezo yake kwenye vijitabu takriban milioni tano vyenye kueleweka kiurahisi na pia ilipitia na kuchambua maoni yaliyowasilishwa.

Kati ya maoni 250 yaliyopokelewa, 12 bora walizawadiwa kompyuta na maoni 25 yaliyofuatia walipewa pongezi kubwa na taa zinazotumia nishati ya jua. Majina ya washindi hao ni:-

Washindi 12 bora zaidi: Rahma Chanzi, Yavan N. Eslon, Amani Frank, Kingstone W. Kahumuza, Sarah Lucas Kisusange, Castory Luoga, Noely Sosimaria Mapunda, Allen Richard Materu, Abdul Walter Moshi, Einoth Justine Ngotoroi, Editha M. Tairo na Godwin Waziri.

Washindi 25 waliofuatia: waliopata pongezi na taa inayoitumia nishati ya jua ni- Godfrey Baraka, Sande John, KenethKammu ,Gabriel Erick Mvingira, Fatuma M. Athumani, Joseph Mathew Buyende, Rachel Philip Bwathondi, Johanita Chimwanga, Christina K. Christopher, William Gabriel Lugis Benjamin John, Specioza Joseph Kalekwa, Kelvin CosmasMacha, Kaliro M. Magoro, Emmanuel Deus Malimi, Filipo Faraja Maliwa, Mariamu Omary Mcholo, Simon Sabaya Mollel, Dorcus Ayoub Mollel, Mary Richard Msukwa, Dativa Mugashe, Abubakar Khasim Mweli, Erick Rwelamila, Vincent Deo Simba na Hedwiga Medard Tairo.

 Baadhi ya mawazo yaliyoshinda yalikuwa pamoja na:
· Uwepo wa gazeti maalum linalochapishwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuwajulisha wanafunzi, walimu, wazazi na watu wengine kuhusu maendeleo ya sekta ya elimu na takwimu muhimu kama vile viwango vya kufaulu mitihani, mitaala na matukio mengine muhimu.

· Upungufu wa wafanyakazi wa afya nchini Tanzania kwa sehemu unaweza kuhusishwa na ukosefu wa wanafunzi waliosomea masomo ya sayansi. Ili kukabiliana na tatizo hili Serikali inapaswa kuanzisha mfumo wa motisha, kama vile kutoa zawadi, ili kuvutia wanafunzi kusoma masomo ya sayansi.

Zawadi zilitolewa kwenye mkutano ulioitishwa na Serikali ya Tanzania ili kushauriana na wadau juu ya rasimu ya pili ya Mpango wa Kuendesha Serikali kwa Uwazi (OGP).. Mgeni rasmi, Mheshimiwa George Mkuchika, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais -Utawala Bora, aliwazawadia wanafunzi vyeti na tuzo zao.

OGP ni jitihada ya kimataifa inayolenga kuziongoza Serikali kuwajibika zaidi kwa wananchi kwa kukuza uwazi, kuwawezesha wananchi, kupambana na rushwa, na kutumia teknolojia mpya kuimarisha utawala. Hadi sasa, ni mataifa 64 yaliojiunga na OGP, Tanzania ikiwa mmoja wapo.

Mpango Kazi wa  kwanza  wa OGP kwa Tanzania inapatikana hapa: http://bit.ly/1mZCPj4. Mpango huu umeweka kipaumbele kwenye utoaji huduma na upatikanaji wa taarifa kama nguzo muhimu kwenye harakati za Tanzania kuelekea Serikali wazi. Mpango Kazi wa pili wa Tanzania kwa sasa uko hatua za mwisho kukamilishwa kufuatia mashauriano na wadau mbalimbali.

Rakesh Rajani, Mkuu wa Twaweza, alisema "Mawazo mapya yanatoka sehemu mbali mbali na shindano hili lilikuwa ni njia moja ya kuibua michango mipya kutoka kwa vijana. Huu ndiyo moyo wa OGP; kutambua kuwa serikali haina ukiritimba juu ya ufumbuzi wa changamoto zetu kuu na huitaji kutoa nafasi na fursa kwa wengine kuchangia mawazo."
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu