• UVCCM TAIFA

  SAUTI YA VIJANA,SAUTI YA UMMA.CCM MPYA,TANZANIA MPYA.

 • UVCCM TAIFA

  MWAKA MMOJA WA SERIKALI YA AWAMU YA TANO.

 • This is default featured slide 3 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

 • This is default featured slide 4 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

 • This is default featured slide 5 title

  Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

Jumatatu, 28 Julai 2014

RAIS KIKWETE AANDAA FUTARI KWA YATIMA,WALEMAVU WA NGOZI NA WATOTO WAISHIO KWENYE MAZINGIRA MAGUMU IKULU DAR ES SALAAM


Yatima, walemavu wa ngozi na watoto walio katika mazingira magumu wakipakua futari waliyoandaliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni
Yatima, walemavu wa ngozi na watoto walio katika mazingira magumu wakipakua futari waliyoandaliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni
Yatima, walemavu wa ngozi na watoto walio katika mazingira magumu wakipakua futari waliyoandaliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni
Yatima, walemavu wa ngozi na watoto walio katika mazingira magumu wakipakua futari waliyoandaliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa meza kuu  na viongozi wa vituo mbalimbali vya yatima, walemavu wa ngozi na watoto walio katika mazingira magumu wakati wa futari  aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni
Yatima, walemavu wa ngozi na watoto walio katika mazingira magumu wakipakua futari waliyoandaliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni
Vijana kutoka Chama cha Albino Wilaya ya Kinondoni wakimshukuru Mama Salma Kikwete kwa futari 
Vijana kutoka Chama cha Albino Wilaya ya Kinondoni wakipata picha ya pamoja na Mama Salma Kikwete baada ya  futari waliyoandaliwa na Rais Kikwete

Rais Kikwete akipita meza moja baada ya ingine kuwasalimia yatima, walemavu wa ngozi na watoto walio katika mazingira magumu wakati wa futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni
Rais Kikwete akipita meza moja baada ya ingine kuwasalimia yatima, walemavu wa ngozi na watoto walio katika mazingira magumu wakati wa futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni
Rais Kikwete akipita meza moja baada ya ingine kuwasalimia yatima, walemavu wa ngozi na watoto walio katika mazingira magumu wakati wa futari aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwashukuru kwa kuja viongozi wa vituo mbalimbali vya yatima, walemavu wa ngozi na watoto walio katika mazingira magumu katika futari  aliyowaandalia Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni
Mama Salma Kikwete akitoa neno la shukurani kwa waalikwa kwenye futari hiyo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongozana na mtoto Khaitham Jumbe Jumbe ambaye alimuandalia zawadi
Rais Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wakipokea zawadi toka kwa mtoto Khaitham Jumbe Jumbe mwenye umri wa miaka saba na mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi ya Yemen iliyoko Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Rais Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wakipokea zawadi toka kwa mtoto Khaitham Jumbe Jumbe mwenye umri wa miaka saba na mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi ya Yemen iliyoko Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Aliyeketi kushoto ni Bi. Mwajuma Hassan wa Chama cha Albino Wilaya ya Kinondoni.

Wageni waalikwa wakifurahia zawadi walizopewa kwenye futari hiyo
Yatima, walemavu wa ngozi na watoto walio katika mazingira magumu wakipakua futari waliyoandaliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni
Yatima, walemavu wa ngozi na watoto walio katika mazingira magumu wakipakua futari waliyoandaliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni
Yatima, walemavu wa ngozi na watoto walio katika mazingira magumu wakipakua futari waliyoandaliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni
Rais Kikwete akipakua futari  Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni
Yatima, walemavu wa ngozi na watoto walio katika mazingira magumu wakiswali swala ya Magharibi wakati wa  futari waliyoandaliwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam jana Jumapili jioni.
PICHA NA IKULU
Share:

Jumanne, 22 Julai 2014

KATIBU MKUU WA UVCCM MH. SIXTUS MAPUNDA AFUTURU NA VIJANAShare:

UVCCM TAIFA INAMUOMBEA MJUMBE WA BARAZA KUU SYLVESTER YARED APONE HARAKA KWA UWEZO WA MUNGU


Mjumbe wa Baraza Kuu Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Viti Vitano Bara Mh. Sylvester Yared akiwa katika Moja ya Majukumu yake ya Kuijenga Chama.    GET WELL SOON JEMBEMjumbe wa Baraza Kuu Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Viti Vitano Bara Mh. Sylvester Yared akizungumza na Wananchi Mkoani Simiyu.
Mjumbe wa Baraza Kuu Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Viti Vitano Bara Mh. Sylvester Yared akiwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Rais Jakaya Mrisho Kikwete
Mjumbe wa Baraza Kuu Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Viti Vitano Bara Mh. Sylvester Yared akiwa na Vijana wa Mkoa wa Mwanza.
Mjumbe wa Baraza Kuu Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Viti Vitano Bara Mh. Sylvester Yared akipanda Mti Zanzibar wakati wa Matembezi ya Miaka 50 ya kuyaenzi Kumbukumbu ya Mapinduzi Matakatifu ya Zanzibar.
Mjumbe wa Baraza Kuu Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Viti Vitano Bara Mh. Sylvester Yared akiwa kwenye Pozi.            

Share:

Jumatatu, 21 Julai 2014

NAPE: WANAOTAKA URAIS 2015 RUKSA KUTANGAZA NIA, KUPIGA KAMPENI KOSA LA 'JINAI'


NA BASHIR NKOROMO
CCM imeweka wazi kwamba kwa mujibu wa taratibu zake, wanaotaka urais kupitia chama hicho wako huru kutangaza nia, na kusisitiza kwamba ugomvi wake mkubwa ni kwa wanaofanya kampeni kabla ya wakati.

Imesisitiza kwamba, kitawachulia hatua stahiki kwa mujibu wa katiba na taratibu za chama, bila kuwaonea huruma wala aibu, kutokana na namna yoyote ikiwemo uwezo wa fedha, nafasi zao za uongozi au umaarufu walionao wale wote watakaobainika kutangaza nia na kisha wakafanya kampeni kabla ya muda rasmi, kwa namna yoyote kutaka kuwania kuteuliwa na CCM kuwania Urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani.

Hayo yamesemwa na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, wakati akizungumza katika kipindi cha 'Baragumu' kwenye Kituo cha Televisheni cha Chanel ten, leo Julai 21, 2014, kilichokuwa na mada 'Urais na Makundi ndani ya Chama'.

"kwanza kabisa Chama chetu kina wanachama wengi, tena wenye sifa za uongozi katika nafasi mbalimbali, katika wingi huu wa wanachama kutakuwa na watu wengi wenye uwezo wanaotaka urais na nafasi nyinge za uongozi,  kwa maana hiyo kelele za kutaka zitakuwa nyingi kwa maana na ushindani na ndiyo maana wenzetu huvizia wawili watatu wanaokosa na kuwafanya wagombea wao", alisema Nape.

Nape alisema, wingi na ubora huu wa wanachama kuwa na sifa za kuwania uongozi ikiwemo urais, bado haiwezi kuwa sababu ya kuacha kila mmoja kutafuta nafasi kwa kupitia utaratibu anaotaka yeye, kila anayedhani kuwa anafaa kuongoza kupitia CCM, lazima kuhakikisha anazingatia kanuni za uongozi na maadili na kanuni za uchaguzi ndani ya CCM.

Alisema kwa mujibu wa kanuni ya Uchaguzi za CCM mwanachama anaruhusiwa kutangaza nia, lakini ni marufuku kuita watu na kuwashawishi kwa maneno, fedha au takrima vyote vikiwa na sura ya kampeni.

Nape alisema, lengo la kanuni hizo za chama ni kuzuia makundi ya mapema ambayo husababisha mtafaruku na mgawanyiko mkubwa ndani ya Chama jambo ambalo alisema, chama kinalikemea kwa lengo la kulinda imani na nguvu ya chama.

Alisema, baadhi ya waliotangaza nia ya kuwania Urais na kupewa onyo kali kwa kipindi cha miezi sita, baada ya kubainika kufanya kampeni kwa namna moja au nyingine,wasipojirekebisha, kwa mujibu wa kanuni wataongezewa adhabu ya karipio kali adhabu ambayo ni ya miezi 18, ambapo utekelezwaji wake utamfanya mhusika kukosa sifa ya kuwania uongozi wa ngazi yoyote kupitia Chama.

Nape alitoa mwito kwa wanaotaka kuwania uongozi hasa urais kwa tiketi ya CCM, kujitahidi kuzingatia kanuni na taratibu zilizopo, ili wasije wakapoteza sifa ya kuwania nafasi wanazotaka.

"Tena, mimi nawaambia hawa, waache kujaribu kujenga makundi kabla ya wakati kwa sababu hata wao hawatanufaika, maana hata wakija wakapata kuteuliwa huku CCM ikiwa vipande vipande hawatapata wanachotaka", alionya Nape.

Akizungumzia sifa za kuwania Urais, Nape alisema, zinazozingatiwa na chama ni zile zilizopo hata kwa mujibu wa Katiba ya nchi, na siyo vigezo vingine kama baadhi wanavyojaribu kutaka kubebwa kupitia ukanda, jinsia, hali au umri.

CCM NI MZAZI HALALI WA MUUNGANO, NI KAZI YA MIKONO YAKE, LAZIMA IUPIGANIE USIFE
Akizungumzia vuguvugu la kutafuta katiba mpya, Nape alisema mchakato wa kaptiba mpya hauzuii maisha kuendelea na ndiyo sababu shughuli nyingine zinaendelea.

Alisema, licha ya shughuli nyingine kuendelea, suala hilo la Katiba mpya CCM imelipa umuhimu wa kutosha kuhakikisha ushiriki wake kama chama utatoa katiba yenye manufaa kwa Watanzania wote.

Nape alisema, madai ya wapinzani kwamba Bunge la Katiba halijadili rasimu ya wananchi ni kivuli cha ajenda yao binafsi lakini ukwli ni kwamba kinachojadiliwa ni rasmu halali ambayo iliwasilishwa na tume ya Katiba.

"Hawa jamaa wanapodai kuwa kinachojadiliwa siyo rasimu ya Katiba, sasa kinachojadiliwa ni nini?, mbona wabunge wameshajadili sura ya kwanza na ya sita ya rasimu hiyo, sasa hawa wanataka kutuambia kwamba mabilioni ya fedha yanayotumika ni ya nini na kwa faida gani", Nape alisema na kuhoji.

Nape alipuuza pia wapinzania wanasema Bunge la Katiba halina mamlaka huku wakijua kwamba kanuni zinazolipa mamlaka bunge hilo, zimetungwa humo humo kwenye bunge la Katiba na wapinzani wenyewe akiwemo Mbunge wa Chadema, Tundulisu Lisuusa.

Kuhusu muundo wa muungano katika mchakato huo wa Katiba, Nape alisema, kinachopiganiwa ni maslahi ya wanasiasa kutaka nafasi za uongozi, lakini ndiyo sababu wapinzania wanafikia zaidi muundo wa serikali tatu ambao kwa vyovyote utaua Muungano.

Nape alisema, baada ya kuona CCM ni wamoja sana kwenye suala la maslahi ya kulinda iliouchojenga kwa miaka 50, wapinzania wameanzisha kikundi walichokiita Umoja wa Katiba ya wananchi- Ukawa,a mabcho alisema, ni 'kijikundi' kidogo tu japo kina kilele sana, kwa kudhani wataweza kupata njia ya mkato.

"Muungano japokuwa ni wa Watanzania wote ni kazi halali ya miko  CCM, yeyote anayeleta chochote kinachotaka kuua muungano huu tutashughulika naye kwa hoja na nvugu zetu zote", alisema Nape.

Akizungumzia hoja ya Rais Jakaya Kikwete kutoa maoni yake kwamba serikali tatu ndiyo mfumo utakaouweka salama muungano, Nape alisema, Rais alitoa hilo kama mlezi wa nchi lakini wabunge wa bunge la Katiba hawakuzuiliwa kujadili kwa kina rasim kadri watakavyoona inafaa kwa faida ya taifa la Tanzania.

"Mimi nampongeza Rais Kikwete, kwa sababu kama kiongozi mkuu wa nchi ni kama baba ndani ya nyumba, ilimpasa kutoa angalizo lake lakini pia akatoa uhuru kwa wabunge kuamua watakavyoona inafaa, kufuata ushauri wake au kuuacha", alisema Nape.

Alimsifu Rais Kikwete kuwa ni kiongozi muungwana sana, akisema, kwamba, angekuwa Rais dikteta angeweza kuielekeza Tume ya Katiba chini ya jaji na Waziri Mkuu mstaafu Joseph Warioba, kufuata maelekezo yake kwa kuondoa kwanza asiyo yataka kabla ya rasimu kupekwa kwenye Bunge la Katiba.
Share:

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AKABIDHI ZAWADI ZA WASHINDI WA MASHINDANO YA QUR-AN JIJINI DAR


  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati alipokuwa mgeni rasmi kukabidhi Tuzo za washindi wa mashindano ya kuhifadhi qur-aan, yaliyofanyika leo Julai 20, 2014, kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam. Picha na OMR

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi, mshindi wa pili wa mashindano ya kuhifadhi Qur-an, ambaye ni Mtanzania, Said Omary Said, wakati wa hafla ya hitimisho la mashindano hayo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, leo Julai 20, 2014. Wa pili kushoto ni Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi. Picha na OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi, mshindi wa kwanza wa mashindano ya kuhifadhi Qur-an, Hatham Sadar, kutoka nchini Kenya wakati wa hafla ya hitimisho la mashindano hayo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, leo Julai 20, 2014. Wa pili kushoto ni Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi. Picha na OMR
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi na baadhi ya viongozi wakiwa katika picha ya pamoja na washindi watatu wa mashindano hayo baada ya kukabidhiwa zawadi zao. Picha na OMR

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi na baadhi ya viongozi wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mashindano hayo baada ya kukabidhiwa zawadi zao. Picha na OMR

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi na baadhi ya viongozi wakiwa katika picha ya pamoja na washindi watatu na majaji wa mashindano hayo baada ya zoezi la kukabidhi zawadi. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislam, wakati akiondoka kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee baada ya kukabidhi zawadi za washindi wa mashindano ya kuhifadhi Qur-an, yaliyomalizika leo Julai 20, 2014, jijini Dar es Salaam. Picha na OMR
Share:

RAIS JAKAYA KIKWETE AFUNGUA BARABARA YA PERAMIHO-MBINGA 78KM


 Barabara ya Peramiho -Mbinga yenye urefu wa Kilometa 78 iliyofunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa  Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na viongozi wengine wa Serikali wakivuta utepe kuashiria ufunguzi wa barabara ya Peramiho-Mbinga yenye urefu wa Kilometa 78.

 Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa barabara ya Peramiho-Mbinga 78Km huku akiwa  na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na viongozi wengine wa Serikali.

 Mamia ya wakazi wa Mbinga wakifurahia wakati Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa anamshukuru Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa Utendaji wake mzuri wa kuwajali wakazi hao kwa kuwajengea miundombinu bora.
 Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wa kwanza kulia akizungumza na Waziri wa Ujenzi Dkt.John Magufuli kabla ya uzinduzi wa barabara ya Peramiho-Mbinga 78km .Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu.

 Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katikati akimshukuru balozi wa China nchini aliye kushoto kwake kwa kazi nzuri iliyofanywa na Mkandarasi kutoka China Kampuni ya Synohdro. Kushoto ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli akishuhudia pamoja na Mawaziri wengine waliohudhuria ufunguzi wa barabara hiyo.Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katikati akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na baadhi ya Makatibu Wakuu na Mawaziri waliohudhuria katika ufunguzi wa barabara ya Perahimo-Mbinga (Km 78)
Share:

Ijumaa, 18 Julai 2014

MANGULA AKUTANA NA KATIBU MKUU WA CAPP DAR ES SALAAM


 Makamu Mwenyekiti wa CCM(Bara) Ndugu Philip Mangula akimkaribisha Katibu Mkuu wa CAPP Dk. Nafie Ali Nafie kutoka Khartoum Sudan kwenye ofisi Ndogo za CCM Lumumba.
 Makamu Mwenyekiti wa CCM(Bara) Ndugu Philip akiwa kwenye mazungumzo na Katibu Mkuu wa CAPP Dk. Nafie Ali Nafie kutoka Khartoum Sudan kwenye ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini Dar es Salaam,Julai 18,2014.
 Makamu Mwenyekiti wa CCM(Bara) Ndugu Philip Mangula akiagana na Katibu Mkuu wa CAPP Dk. Nafie Ali Nafie kutoka Khartoum Sudan
Makamu Mwenyekiti wa CCM(Bara) Ndugu Philip Mangula akiagana na Balozi wa Sudani nchini Tanzania Dk.Yassir Mohamed Ali nje ya Ofisi Ndogo za CCM Lumumba ambapo Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) alikuwa na mazungumzo na Katibu Mkuu wa CAPP Dk. Nafie Ali Nafie kutoka Khartoum Sudan.(Picha na Adam Mzee wa CCM Blog)
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Gadget

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu