Alhamisi, 28 Agosti 2014

DAKTARI BINGWA WA MAGONJWA YA SARATANI YA MATITI KUTOKA INDIA ATUA NCHINI, KESHO KUENDESHA MHADHARA HOTELI YA PROTEA COURT YARD SEAVIEW JIJINI DAR ES SALAAM


 Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira (kulia), akimtambulisha kwa madaktari (hawapo pichani), Daktari Bingwa wa magonjwa ya saratani ya matiti, Profesa Anthony Pais, kutoka Bangorole India,  Dar es Salaam jana. Daktari huyo kesho jioni anatarajia kufanya mhadhara na madaktari wa Kitanzania na wadau wa sekta ya afya kujadili ugonjwa huo katika Hoteli ya Protea Court Yard. Daktari huyo yupo nchini kwa mwaliko maalumu wa mshauri huyo wa Kimataifa.
 Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira (kulia), akiwa na daktari huyo (katikati), Kushototo ni Mama Benedicta Rugemalira. (Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
 Profesa Anthony Pais (katikati), akizungumza na madaktari wa Tanzania. Kushoto ni Dk.Maleare na Dk. Fredy
 Profesa Anthony Pais (kulia), akizungumza na madaktari wa Tanzania.
Wadau wa sekta ya Afya wakiagana na daktari huyo nyumbani kwa Mshauri wa Kujitegemea wa Kimataifa, James Rugemalira Makongo Juu jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam, Tanzania
DAKTARI Bingwa wa ugonjwa wa saratani ya matiti , Profesa Anthony Pais, kutoka Bangorole nchini India kesho Agosti 28, 2014  anatarajia kutoa muhadhara kuhusu ugonjwa huo.

Akizungumza na Mtandao wa www.habari za jamii.com. Dar es Salaam leo Mshauri wa Kimataifa wa Kujitegemea, James Rugemalira alisema ujio wa daktari huyo hapa nchini ni fursa kwa watanzania kutokana na changamoto kubwa iliyopo kuhusu ugonjwa huo.

"Daktari huyu amebobea katika ugonjwa wa saratani ya matiti na amefanya operesheni nyingi za ugonjwa huo ni wakati mzuri kwetu kwenda kumsikiliza kesho jioni Hoteli ya  Protea Court Yard" alisema Rugemalira.

Alisema kesho daktari huyo atatoa mhadhara kwa madaktari wa kitanzania na wadau wa sekta ya afya kuhusu ugonjwa huo na jinsi ya kukabiliana nao.

Rugemalira alisema daktari huyo atakuwepo nchini kwa siku kadhaa na leo alitembea Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Taasisi ya Kansa ya Ocean Road na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

Daktari huyo yupo nchini kwa mwaliko maalumu wa mshauri huyo wa kimataifa ili kuona namna ya kusaidia tatizo hilo. 
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu