Ijumaa, 19 Septemba 2014

KINANA AMALIZA ZIARA WILAYA YA MAFIA, AREJEA NYAMISATI KWA USAFIRI WA MASHAKA WA BOTI YA KIZAMANI Katibu Mkuu wa CCM, akipanda boti ya kizamani, tayari kwa ajili ya safari kutoka Kisiwa cha Mafia kwenda Nyamisati wilayani Rufiji, baada ya kumaliza ziara yake katika wilaya ya Kisiwa hicho, leo Septemba 17, 2014, akiwa katika ziara ya mkoa wa Pwani, kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua katika mkoahuo. Boti hiyo ambayo pia hutumiwa na wananchi kusafiria kati ya kisiwa hicho cha Mafia na Nyamisati Kinana amesafiri nayo kwa saa nne tangu saa sita mchana hadi saa 11 jioni.
 Katibu Mkuu wa CCM akipanda boti hiyo kwa ukakamavu
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa kwenye boti hiyo. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza, ambaye aliwasili wilayani Mafia kwa ndege lakini akalazimika kusafiri na Kinana kwa boti hiyo kurejea Nyamisati. Watatu kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani Mwinshehe Mlao.
 Katibu wa NEC, Itikadina Uenezi, Nape Nnauye (watatu kushoto), akiwa kwenye boti na abiria wengine waliosafiri pamoja na Kinana kutoka Mafia hadi Nyamisati leo.
 Baadhi ya maofisa wa CCM na Waandishi wa habari wakiwa kwenye boti hiyo wakati wakisafiri na Kinana kutoka Mafia hadi Nyamisati leo.
 Mkurugenzi wa Mawasiliano na Umma wa Makao Makuu ya CCM, Daniel Chongolo (watatu kushoto) akiwa na abiria wenzake katika boti hiyo kutoka Mafia hadi Nyamisati leo.
 Abiria wengine wakiwa katika boti hiyo kutoka Mafia kwenda Nyamisati leo. Kushoto ni Mwandishi wa Clouds TV/Radio Salum Mwinyimkuu.
 Baadhi ya viongozi wa UVCCM na CCM wakiwa kwenye boti hiyo wakati wakisafiri na Kinana kutoka Mafia kwenda Nyamisati.
  Baadhi ya viongozi wa UVCCM na CCM wakiwa kwenye boti hiyo wakati wakisafiri na Kinana kutoka Mafia kwenda Nyamisati.
 Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mama Salma Kikwete ya Wama iliyopo wilayani Rufiji, baada ya kutoka Mafia. Kushoto ni Mkuu wa shule hiyo, Suma Mesa. Kinana amempongeza Mama Salma kwa uamuzi wake wa kuanzisha shule hiyo ambayo ni maalum kwa ajili ya kutoa elimu kwa watoto yatima kutokamikoa mbalimbali nchini.
 Watoto wa shule hiyo wakimsikiliza Katibu Mkuu Kinana.
Kinana akiondoka kwenye shule hiyo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Pwani Mwinshehe Mlao na watatu kushoto ni Mwandishi wa habari wa gazeti la Jamboleo, Saidi Mwinshehe na kulia ni Chongolo. Kinana anatarajiwa kuendele na ziara yake katika mkoa wa Pwani kesho, Septemba 18, 2014. Maelezo/Picha zote na Bashir Nkoromo wa theNkoromo Blog Kwa hisani ya Sufyan Omar
 
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu