Jumamosi, 13 Septemba 2014

KINANA AONGOZA KIKAO CHA MAKATIBU WAKUU WA VYAMA VYA UKOMBOZI

Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana akiongoza kikao cha Makatibu Wakuu wa Vyama Rafiki vilivyopigania Ukombozi wa Nchi Kusini mwa Afrika (FLM). Kushoto kwa Kinana ni Katibu Mtendaji Mkuu wa ZANU-PF ya Zimbabwe Comrade Didymus Mutasa na anayefuata ni Katibu Mkuu wa ANC ya Afrika Kusini Comrade Gwede Mantashe. Kulia kwa Kinana aliyevaa miwani ni Katibu Mkuu wa MPLA ya Angola Comrade Juliao Mateus Paulo 'Dino Matrosse' na anayefuata ni Katibu Mkuu wa SWAPO Party ya Namibia Comrade Nangolo Mbumba.

Mkutano huo wa siku moja umefanyika leo tarehe 10 Septemba, 2014 Jijini  Johannesburg, Afrika Kusini na ulikuwa na ajenda Kuu ya Ujenzi wa Chuo cha pamoja cha Vyama kitakachojengwa Ihemi, Iringa Tanzania. Madhumuni ya Chuo hicho ni kubadilishana uzoefu na kurithisha historia ya Ukombozi kwa vizazi vijavyo.

(Imetolewa na Ofisi ya Katibu Mkuu wa CCM)
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu