Unordered List


SOPHIA MFAUME: MAHAKAMA YA KADHI SIO KULETA UTAWALA WA SHARIA


 
               MAHAKAMA YA KADHI

Watu wengi hatujapata kuelewa nini wanamaanisha wanaposema mahakama ya kadhi itambulike kikatiba.
⏳Pengine wengi wetu tunadhani labda mahakama ya kadhi ikihalalishwa itakua kama kukubali SHARIA, kitu ambacho si kweli.

Hata kabla Tanzania haijapata uhuru tulikua na taratibu zetu sisi kama waTz, ambapo tulikua masuala yetu kama mirathi, haki ya kumiliki mifugo, migongano itokeayo kama wizi wa ng'ombe na mambo mengine yalitatuliwa/yalitolewa hukumu na mahakama zetu za kimila au tamaduni au dini. 

Hivyo kuanzishwa kwa mahakama ya kadhi kutasaidia uharaka, haki na utatuzi wa migongano na matatizo madogomadogo kama talaka na urithi ; Na kuiachia mahakama ya serikali kesi kubwakubwa za saiz yake. ⏳
Mahakama ya kadhi itasaidia kutatua kesi na migogoro mingi hivyo kusaidia ufanisi na kuokoa muda.

MAHAKAMA YA KADHI SIO KULETA UTAWALA WA SHARIA

Chapisha Maoni

0 Maoni