Jumamosi, 25 Oktoba 2014

DAIMOND APELEKA MAGWANDA POLISI

Diamond asalimisha magwanda polisi


MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Naseeb Abdul 'Diamond', amekiri kuhojiwa na polisi baada ya kukutwa na hatia ya kuvaa mavazi yanayoaminika kuwa ni sare (magwanda) ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Hata msanii huyo alidai kwamba mavazi hayo hayakuwa sare za jeshi hilo na kwamba yeye aliyanunua alipokuwa Ujerumani ingawa baada ya kuhojiwa aliyasalimisha.
Diamond alipanda jukwaani Jumamosi iliyopita katika onyesho la Fiesta jijini Dar es Salaam akiwa na mavazi hayo jambo ambalo liliibua mjadala.
Akizungumza jana Alhamisi, Diamond alikiri kupata ujumbe uliomtaka kufika Kituo cha Oysterbay, Dar es Salaam na madansa wake akiwa na nguo hizo.(P.T)
"Awali Meneja wangu alishikiliwa kwa muda na mimi nikatakiwa kufika na zile nguo nikiwa na madansa wangu ambao pia walizivaa, nilifanya hivyo na kuziacha nguo baada ya taratibu zote za kisheria kukamilika," alisema.
"Nisingeweza kukaidi amri ya dola, nilifika na yale mavazi na nikahojiwa kwa saa kadhaa. Nikaeleza kwamba yalikuwa yakifanana tu na ya jeshi na hayakuwa sare rasmi za jeshi, kikubwa nilihitaji kumaliza tatizo," alisema.
Diamond alifafanua pia kwamba si kweli kwamba alichukuliwa dhamana na Chief Kiumbe, ukweli ni kwamba alisindikizwa na mdau huyo wa sanaa kama kaka tu kutokana woga aliokuwa nao, lakini hakushikiliwa na kutakiwa kutoa dhamana yoyote.
Chanzo:Mwanaspoti
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu