Jumatano, 8 Oktoba 2014

KINANA AENZIWA KALENGA, APEWA HESHIMA YA KICHIFU, AHUTUBIA WANANCHI AKIWA KWENYE KILIMA CHA CHIFU MKWAWA


 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akivishwa, majoho na Chifu wa sasa wa Wahehe, Abdul Adam Sapi Mkwawa (kulia), kwenye kilima alichokuwa akitumia Chifu Mkwawa, enzi hizo katika Kata ya Kalenga. Kinana alipewa heshima hiyo kabla ya kuhutubia wananchi kwenye kilima hicho. Oktoba 6, 2014, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM Iringa Vijijini.
 Katibu Mkuu wa CCM akiwa na viongozi wa Kichifu baada ya kuvishwa vazi la heshima na kupewa mkuki na viongozi hao.
 Abdul Mkwawa akimshika mkono Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kwenda kuketi baada ya kupewa heshima hiyo.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa na viongozi wa Kichifu kabla ya kuhutubia
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisindikizwa na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye kwenda jukwaani kuhutubia wananchi, Okboba 6, 2014.
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi kwenye Kata ya Kalenga, wilaya ya Iringa Vijijini mkoani Iringa.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipokea kadi ya Chadema kutoka Rehema  Said, wakati alipopokea wanachama wapya kutoka Chadema kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Kalenga. Wanachama wapya 21 wa Chadema walijiunga na CCM
 Kinana akionyesha kadi za Chadema alizokabidhiwa wakati wa mkutano huo
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Kilima cha Mkwawa, Kata ya Kalenga Iringa Vijijini
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu akihutubia wananchi kwenye mkutano huo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki kuvua samaki kwenye mradi wa visima vya ufugaji samaki cha kina mama katika kata ya Kalenga, wilaya ya Iringa Vijijini.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimwagilia dawa ya kuua wadudu alipotembelea mradi wa kilimo cha nyanya wa kinamama wa kata ya Kalenga
 Kinana akiwasalimiana wananchi alipowasili kukagua kikundi cha kina mama wajasiriamali wafuga samaki kata ya Kalenga
 Kinana wakimkaribisha Kinana jimbo la Kalenga
Kinana akiwa na mjumbe wa shina namba moja
 Mkuu wa mkoa wa Iringa Christian Ishengoma akisoma taarifa mbele ya Kinana
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu akimkaribisha Karibu Mkuu wa CCM Kinanakuzungumza katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Iringa Vijijini jimbo la Kalenga.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimia kwenye kikao hicho
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumza kwenye kikao hicho cha wajumbe wa Halmashauri Kuu wilaya ya Iringa Vijijini Jimbo la Kalenga
Wajumbe wakimsikiliza Kinana
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu