Jumamosi, 4 Oktoba 2014

KINANA AFANYA MKUTANO WA KIHISTORIA TANGA

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi waliofika kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Tangamano kata ya Tangamano wilaya ya Tanga mjini.
Wananchi wakiwa na bango lao kwenye mkutano wa hadhara wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye uwanja wa mikutano Tangamano.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana , Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kwa pamoja wakiwapungia wananchi waliofika kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya mikutano Tangamano, Tanga mjini.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipeana mkono na Mzee Athumani Makalo wakati akiwasili kwenye uwanja wa mkutano wa Tangamano.
Wananchi wa Tanga mjini wakishangilia ujio wa Katibu Mkuu wa CCM kwenye viwanja hivyo ya mikutano.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wananchi wote waliohudhuria mkutano kwa kuwapingia mikono yote miwili.
Wananchi nao hawakuwa nyuma kumpungia kiongozi wao.
Mkuu wa wilaya ya Tanga mjini Mh.Halima Dendegu akiwasalimia watu waliofurika uwanjani kwenye mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Kila mwananchi wa tanga alikuwa na shauku ya kusikiliza mkutano huo
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwapungia mkono maelfu ya watu waliofurika kwenye mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana uliofanyika kwenye uwanja wa Tangamano.
Wananchi wakishangilia kwa nguvu wakati wa hotuba ya Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia kwenye uwanja wa Tangamano
Wadau wa CCM mkoa wa Tanga wakifuatilia mkutano
Kila mtu wa Tanga alikuwepo kwenye mkutano huo.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa  Tanga mjini na kuwaambia watendaji wa serikali kutoka maofisini na kwenda kwa wananchi ambao wanamaswali ya matatizo yao na wanahitaji majibu.
Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Tanga Mama Aisha Kigoda pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Tanga mjini Mh.Halima Dendegu wakifuatilia kwa makini hotuba za viongozi kwenye mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana uliofanyika kwenye viwanja vya Tangamano.
Mbunge wa Jimbo la Tanga mjini Mh.Omari Nundu akihutubia wananchi wa Tanga mjini kwenye mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Tanga mjini ambapo aliwaambia muda wa kuwaambia watanzania maendeleo yapo kwenye mipango umekwisha na kutaka viongozi kutimiza wajibu wao.
Maelfu ya wakazi wa Tanga wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa anahitimisha ziara yake ya siku 11 kwenye mkoa wa Tanga.
Wananchi wakimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambapo pamoja na yote alizungumzia uchumi wa Tanga ambapo aliwaambia wananchi hao lazima reli na bandari zifanye kazi ili uchumi wa mkoa wa Tanga ubadilike.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisitiza jambo wakati akihutubia wakazi wa Tanga mjini.
Katibu Mkuu wa CCM akiwa kwenye picha ya pamoja na wanachama waliojiunga na CCM kutokea chama cha CUF
Mzee Athumani Makalo akitoa salaam za pongezi kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kwa hotuba nzuri zilizobadilisha siasa ya Tanga .
Mzee Makalo akimvisha Katibu Mkuu joho  zawadi kutoka kwa wazee wa Tanga mjini.
Katibu Mkuu wa CCM akiagana na watu baada ya kumaliza mkutano
Watu wakigombania kumshika mkono Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati akiondok kwenye uwanja wa mikutano
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwapungia mkono wananchi kama ishara ya kuwaaga baada ya kumaliza mkutano mkubwa mjini Tanga.
Kila mtu alimuaga Katibu Mkuu wa CCM kwani mkutano wake wa leo aliongela masuala ya msingi yanayohusu mkoa wa Tanga.

Na Sufyan Omar
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu