Unordered List


KINANA AISASAMBUA CHADEMA NYOLOLO MKOANI IRINGA, KATIBU WA KATA WA CHAMA HICHO AHAMIA CCM


*NI ALIYEPEWA TENDA NA CHADEMA KUJENGA MNARA WA MAREHEMU MWANGOSI
*ADAI CHADEMA ILIMTALIPELI ITAMLIPA KWA KAZI HIYO LAKINI HADI SASA PATUPU
*ANG'OKA CHADEMA NA VIJANA  27
 Katibu wa Chadema Kata ya Igowole, wilayani Mufindi mkoani Iringa,  Josephat Soda akitangaza kukihama chama hicho, mbele ya maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadhara wa Kinana uliofanyika leo, Oktoba 10, 2014, kwenye mjini mdogo wa Nyololo. Soda amesema ameamua kukihama chama hicho baada ya kubaini kuwa ni matapeli waliompa kazi ya kujenga mnara wa kumbukumbu wa  mwandishi wa habari David Mwangosi, aliyeuawa katika mapambano cha Chadema na Polisi wakati wa maandamano yaliyofanywa na chama hicho mwaka juzi katika mji huo mdogo wa Nyololo ambapo aliujenga mnara huo wa gharama zake na kukopa saruji kwa ahadi ya kulipwa na viongozi wa Chadema lakini hadi leo ameambilia patupu.
 Soda akikabidhi kadi yake ya Chadema kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana baada ya uamuzi wake wa kuamua kuhamia CCM kwenye mkutano huo.
Kinana akionyesha kadi ya Soda na vijana wengine  27 waliohamia CCM kumfuata Soda
 Soda akizungumza mbele ya Kinana. Kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenzi nape Nnauye aliyefanyakazi ya kumkaribisha Soda jukwaani.
 Vijana walioamua kumfuata Soda kuhamia CCM wakionysha kadi zao za Chadema kabla ya kumkabidhi Kinana
Kinana akimkabidhi Soda kadi ya CCM. Wapili kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iriga, Jesca Msambatavangu
 Kadi mpta ya CCM aliyokadhiwa Soda
 Vijana waliomfuata Soda kuhamia CCM wakipewa kadi za CCM na Kinana
Wananchi wakishangilia baada ya Kinana kumpokea Soda na vijana hao
 Soda (kulia) akiungana na wenzake kula kiapo baada ya kukabidhiwa kadi za CCM na Kinana
 Baadhi ya waandishi wa habari walioko kwenye msafara wa Kinana mkoani Iringa, wakiwa kwenye mnara uliojengwa na Soda kwa ajili ya kumbukumbu ya Mwangosi. Hata hivyo mnara huo hauna maandishi wala chochote kinachoonyesha kuwa umanhusu marehemu Mwangosi
Kiongozi wa bendi ya CCM ya Mafinga, akiongoza kuimba wimbo maalum wa CCM inavyotekelza ilani ya Uchaguzi, wakati wa mkutano huo
 Katibu Mkuu wa CCM, Kinana (kulia) akiungana na wananchi kuselebuka wimbo huo maakum wa CCM
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa na wanamuzi wa bendi hiyo ya CCM baada ya wimbo huo
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana na Nape wakiitazama albamu ya wimbo huo maalum wa CCM. Picha zote na Bashir Nkoromo-CCM Blog kwa hisani ya Sufyan Omar

Chapisha Maoni

0 Maoni