Jumatano, 8 Oktoba 2014

KINANA AUNGURUMA JIMBONI KWA WAZIRI LUKUVI LEO, ASHIRIKI KAZI ZA MAENDELEO


 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo, Oktoba 7, 2014, katika Kijiji cha  Magozi, Kata ya  Ilolo Mpya, akiwa katika ziara ya kukagua na kuhimiza utekelezaji wa ilani ya CCM katika jimbo la Isimani la Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uratibu na Bunge, William Lukuvi katika wilaya ya Iringa Vijijini, mkoani Iringa.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano huo
 Mbunge wa Isimani, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uratibu na Bunge, William Lukuvi akieleza alivyotekeleza ilani ya CCM wakati wa mkutano huo
 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu akieleza sera za Chama wakati akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kuzungumza na wananchi kwenye mkutano huo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimfagilia jukwaaani, Lukuvi wakati wa mkutano huo, ambapo alisema, Mbunge huyo ambaye pia ni waziri anatosha kuwahudumia wananchi wa jimbo la Isimani kwa kuwa ni mchapakazi kwa vitendo.
 Mbunge wa Isimani William Lukuvi akiwa amemkabidhi kompyuta Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari ya William Lukuvi, iliyopo Kata ya Ilolo Mpya,  Charles Mgimwa (kulia ) wakati wa mkutano huo. Mbali na kuwakabidhi kompyuta walimu wa shule mbili za sekondari aliwataka wananchi kuwa tayari kuunganishiwa umeme wa bei nafuu ambao alisema utaaingia kwenye kata hiyo hivi karibuni.
 Lukuvi akiselebuka na wananchi katika kucheza ngoma wakati wa mapokezi ya Kinana kwenye mkutano huo
 Wananchi wa Jamii ya Kimasai wakicheza ngoma kumpokea Kinana wakati wa mkutano huo
 Wananchi wa Jamii ya Wasukuma wakicheza ngoma kumlaki Kinana kwenye mkutano huo
 Mabinti wa Kimasai wakiwa katika mavazi yao nadhifu wakati wakiingia kwenye mkutano huo
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikagua ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Magozi, Kata ya Ilolo Mpya akiwa katika ziara ya kikagua utekelezaji wa ilani ya CCM katika jimbo la Isimani, wilaya ya Iringa Vijijini leo. Kushoto ni Mbunge wa jimbo hilo, William Lukuvi
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsisitizia jambo Lukuvi baada ya kukagua ujenzi wa zahanati hiyo.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa nyumba ya mwalimu shule ya sekondari william Lukuvi  Ilolo Mpya.
 Mjumbe wa shina namba sita, Changula Mlula akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwenye kikao cha shina hilo, Kijiji cha  Magozi, Ilolo  Mpya jimbo la Isimani. Kulia ni Mbunge wa Isimani William Lukuvi
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza kwenye shina hilo. Kulia ni Katibu wa NEC, Itikadi na uenezi Nape Nnauye akifutailia hali yab mambo
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akzindua Ofisi ya CCM Kata ya Ilolo Mpya katika kijiji cha Luganga, jimbo la Isimani
 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na Lukuvi wakishiriki kufyatua matofali ujenzi wa Zahanati Kijiji cha Magozi Ilolo Mpya
VIJANA WA CCM: Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnaye akiwa na Katibu wa CCM mkoa wa Iringa Hassan Mtenga, wakati wakiongozana na Kinana katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM jimbo la Isimani Iringa Vijijini, leo, Oktoba 7, 2014. Picha zote na Bashir Nkoromo-CCM Blog kwa Hisani ya Sufyan Omar
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu