Jumamosi, 1 Novemba 2014

Aliyasaliti Mapinduzi Ya Umma, Na adhabu Imemfika... COMPAORE


Ndugu Zangu,
Najisikia furaha katika siku hii ya leo kuwaona vijana wale wa Burkinafaso, kwa kuamua kuingia mitaani wamemlazimisha Blaise Compaore kuachia ngazi.
Siku hii ya leo inanikumbusha Jumamosi moja mwaka 1990. Nilikuwa Kidato cha Sita pale Sangu Sekondari. Vijana tuliandaa debate kwa Kiingereza. Nilipata nafasi ya kusimama jukwaani kumzungumzia Mwanamapinduzi Captain Thomas Sankara. Pale ukumbini tulikuwa na Emmanuel Nchimbi pia. Namkumbuka pia Alfred Mwambeleko. Captain Sankara alikuwa Rais kijana, Mjamaa na mwanamapinduzi. Nakumbuka ziara yake ya kwanza baada ya kuchukua madaraka ilikuwa Tanzania kuonana na Mwalimu.
Huko nyuma nimepata kutoa mifano kadhaa ya viongozi walioacha hiba nyuma yao, hiba njema na mbaya; nilimtolea mfano Captain Thomas Sankara. Kuwa aliacha hiba njema ya kuenziwa ndani ya nchi yake, Afrika na duniani.
Mwanamapinduzi huyu alikuja kuawa kwa kupigwa risasi na wapinga mapinduzi na maendeleo ya Burkina Faso. Na aliyempindua ni Blaise Compaore, rafiki yake. Sankara alipata kukaririwa akisema;(P.T)
"Ningependa kuacha nyuma yangu, imani ya kuwa, kama tunaimarisha kiwango fulani cha uangalifu na oganaizesheni, basi, tunastahili ushindi. Kamwe huwezi kuleta mabadiliko ya kimsingi bila ya kuwa na kiwango fulani cha uwendawazimu.
Hali hii inatokana na kutoshinikizwa na taratibu zilizozoeleka, kuwa na ujasiri wa
kuzipa mgongo kanuni za kizamani, ujasiri wa kuanzisha mustakabali.
Ni wendawazimu wa jana waliotuwezesha kuyafanya tuyafanyao leo.
Ninataka kuwa mmoja wa wendawazimu hao." ( Hayati, Kapteni Thomas Sankara)
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu