Jumatatu, 24 Novemba 2014

BALOZI SEIF IDDI ZIARAN NCHINI CHINA

Ujumbe wa Zanzibar uliokuwa nchini China kwa ziara ya Kiserikali ukipata mlo kwenye Tafrija maalum waliyoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania Nchini China.
Wa kwanza kutoka kushoto ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mh. Said Hassan Said, Meya wa Manispaa ya Zanzibar Mstahiki Khatib Abdulrahman Khatib, Waziri wa Ardhi, Makazi, Maji na Nishati Mh. Ramadhan Abdulla Shaaban,Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mh. Said Ali Mbarouk na Mwakilishi wa Jimbo la Chaani Mh. Ussi Jecha Simai.
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi akiwa pamoja na Mke wa Balozi wa Tanzania Nchini China Mama Mary Antony Tairo pamoja na Afisa wa Ubalozi huo Nd. Kitokezi Juma Kitokezi wakiwa kwenye Tafrija iliyoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania Nchini China kwa ujumbe wa Zanzibar.
Mkuu wa Ufundi wa Kampuni ya Kimataifa ya Ujenzi ya China { BCEG } Mhandisi Tiger Nzu akimpatia maelezo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na ujumbe wake ulipofanya ziara ya kutembelea uwanja wa Kimataifa wa Beijing Nchini China ambao umejengwa na Kampuni hiyo ya BCEG.
Nyuma ya Mhandisi Tiger Nzu ni Waziri wa Habari Utamaduni, Utalii na Michezo Mh. Said Ali Mbarouk, kati kati ya Balozi Seif na Mh. Said ni Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar Balozi Silima Kombo, kushoto ya Balozi Seif ni Waziri wa Ardhi, Makazi, Maji na Nishati Mh. Ramadhan Abdulla Shaaban na nyhuma yake ni Mwakilishi wa Jimbo la Chaani Mh. Ussi Jecha Simai.
Balozi Seif akizungumza mara baada ya Tafrija iliyoandaliwa na Kampuni ya Ujenzi ya BCEG kwa ajili ya Ujumbe wake baada ya kumaliza kutembelea uwanja wa ndege wa Beijing Nchini China.
Mbele ya Balozi Seif aliyevaa miwani na kukaa ni Naibu Meneja wa Kampuni ya BCEG Bwana Dinng Chuanbo.

Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ. 

Mashirika Taasisi za Umma na zile binafsi pamoja na wazazi wanaowadhamini kimasomo wafanyakazi na watoto wao Nchini Jamhuri ya Watu wa China wanapaswa kuwasiliana na Uongozi wa Ubalozi wa Tanzania Nchini humo ili kuepuka utapeli unaofanywa na baadhi ya mawakala wa sekta hiyo.
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Nchini China Balozi Abdulrahman Amir Shimbo alitoa kauli hiyo wakati wa dhifa maalum aliyouandalia Ujumbe wa Zanzibar ulioongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ulipofanya ziara yake Nchini humo.
Dhifa hiyo iliyoshirikisha pia wafanyakazi wa Ubalozi huo ilifanyika katika Ofisi ya Ubalozi Wa Tanzania uliopo katika Bara bara ya Liang Ma He Naulu Mtaa wa Sanlitum Mjini Beijing Nchini China.
Balozi Shimbo alisema yapo matatizo mengi yanayoendelea kuwakumba Wanafunzi wengi wanaotoka Tanzania kwa kutumia Mawakala wababaishaji licha ya kwamba baadhi yao wamepata ufadhili usio na usumbufu.
Alisema kitendo cha baadhi ya wafadhi pamoja na wazazi wa wanafunzi hao kutumia mawakala husababisha kuibuka kwa matatizo na gharama kubwa zinazoweza kuepukwa sambamba na kuuongezea mzigo Ubalozi.

Balozi Abdulrahman alieleza kwamba hivi sasa wanafunzi wengi wanapata fusa za masomo Nchini China ambapo wengi kati yao hupata ufadhili wa Serikali, Taasisi na Mashirika ya Umma pamoja na Wazazi binafsi.
Balozi huyo wa Tanzania Nchini China aliuelezea ujumbe huo wa Zanzibar kwamba mwaka ujao Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China imeongeza nafasi 100 za masomo ya juu kwa Wanafunzi wa Tanzania kupata taaluma ya vyuo vikuu mbali mbali Nchini humo.
Alifahamisha kwamba Ofisi yake itawasiliana na Serikali zote mbili ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya Mapinduzi ya Zanzibar katika uratibu wa kuzitumia nafasi hizo ili ziwafaidishe Vijana wa pande zote mbili za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akigusia ziara mbali mbali za Viongozi wa ngazi za Juu wa Tanzania wanaotembelea China Balozi Shimbo alisema Wafanyakazi wa Ofisi ya Ubalozi huo wamepata faraja kubwa kufuatia ujio wa Viongozi hao.
Balozi Shimbo alisisitiza kwamba Uongozi wa Ubalozi huo unaendelea kufuatilia utekelezaji wa makubaliano au ahadi zilizotolewa kufuatia ziara za Viongozi hao wakuu wa Tanzania China.
Alisema ziara hizo kwa pande zote mbili kati ya china na Tanzania kwa kiasi kikubwa zimeleta na kuimarisha zaidi uhusiano uliopo kati ya pande hizo mbili rafiki.
Akitoa shukrani kwa niaba ya ujumbe aliouongoza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliwakumbusha wafanyakazi wa Ubalozi huo wa Tanzania Nchini China kuzidisha mashirikiano yao kwa lengo la kupata ufanisi zaidi.
Balozi Seif alisema mashirikiano hayo yataendeleza sifa ya watendaji hao kufanya kazi katika misingi ya umoja na upendo kama utamaduni wao ulivyowalea na kuwanyooshea njia.
Akigusia ziara yao nchini China Balozi Seif alisema ujumbe wake umeona na kushuhudia maendeleo makubwa yaliyofikiwa na China katika kukuza uchumi na kuimarisha maendeleo ya ustawi wa Jamii.
Alisema licha ya kujifunza huko lakini pia ziara ya ujumbe huo wa Zanzibar imesaidia kuimarisha uhusiano wa kihistoria unaoendelea kukua siku hadi siku kati ya China na Tanzania na Zanzibar kwa jumla.
Alifafanua kwamba Zanzibar na China hasa kisiwa cha Jimbo la Hainan zimekuwa na mafungamano makubwa ya ushirikiano wa muda mrefu uliokuja kutokana na kufanana kwa mazingira ya visiwa hivyo viwili vilivyoko katika ukanda wa joto.
Balozi Seif alimuhakikishia Balozi wa Tanzania Nchini China Balozi Abdulrahman Shimbo kwamba mambo yaliyokubalika ndani ya ziara hiyo yatafuatilia ili kuona ufanisi unapatikana.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza Wafanyakazi wa Ubalozi huo kwa dhifa maalum waliyouandalia ujumbe wake jambo ambalo ni moja kati ya utamaduni uliojengeka miongoni mwa Watanzania.
Mapema Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Ujumbe wake walipata fursa ya kutembelea maegesho ya ndege katika uwanja wa Kimataifa wa Beijing sehemu ya Tatu { Terminal Three } iliyojengwa na Kampuni hiyo ya Beijing Construction Engeneering Group.
Mkuu wa ujenzi wa Kampuni hiyo Mhandisi Tiger Nzu aliueleza ujumbe huo wa Zanzibar kwamba uwanja huo wenye urefu wa kilomita tatu una sehemu 96 zenye uwezo wa kuhudumia abiria mbali mbali wa safari za Kitaifa na Kimataifa.
Mhandisi Tiger alifahamisha kwamba huduma zote zinazopaswa kupatiwa abiria wakiwemo walemavu na watu wenye mahitaji maalum kama watoto a Wagonjwa zimepangiwa utaratibu maalum katika viwango vinavyokubalika Kimataifa.
Wakati wa Tafrija ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Kampuni hiyo ya BCEG Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba uzoefu na utaalamu mkubwa uliyonayo Kampuni ya Kimataifa ya ujenzi ya Jamuhuri ya Watu wa China { Beijing Construction Engeering Grouop -BCEG } unatoa matumaini makubwa kwa kumalizika kwa mafanikio uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar.
Alisema kazi kubwa inayoendelea kufanywa na Kampuni hiyo inayojenga maegesho ya uwanja wa ndege wa Zanzibar inatoa matumaini ya kuufanya uwanja huo kufikia hadhi ya Kimataifa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliupongeza Uongozi na Wafanyakazi Kampuni hiyo ya { BCEG } kwa umakini wake ambao ndio saabu unayoupa fursa nyingi za tenda za ujenzi kampuni hiyo katika Mataifa mbali mbali Duniani hasa nchi za Bara la Afrika.
Naye Naibu Meneja wa Kampuni ya Ujenzi ya BCEG Bwana Ding Chuanbo alisema kukamilika kwa ujenzi wa maegesho ya ndege kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar kutaiwezesha Zanzibar kupiga hatua kubwa za kimaendeleo.
Bwana Ding alisema mabadiliko ya Kiuchumi ya Zanzibar yatazidi kuimarika kufuatia kuongezeka kwa mapato kupitia sekta ya Utalii inayoonekana kuchukuwa nafasi ya juu katika uchumi wa Zanzibar.
Naibu Meneja huyo wa Kampuni ya BCEG aliueleza ujumbe huo wa Zanzibar kwamba Kampuni hiyo iliyoasisiwa mwaka 1953 tayari imefanikiwa kiuzalishaji hali inayoifanya kuwa na Idara 24 za fani tofauti za utaalamu.
Balozi Seif na Ujumbe wake amemaliza ziara yake Nchini Jamuhuri ya Watu wa China akipitia Mjini Dubai kwa mapumziko mafupia ambapo anatarajiwa kurejea nyumbani mwisho mwa wiki hii.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu