Ijumaa, 14 Novemba 2014

HALIMA MDEE AMKIMBIA SIXTUS MAPUNDA TANGAkatibu mkuu wa umoja wa vijana wa ccm ndugu SIXTUS MAPUNDA  leo kwa kushirikiana na mkuu wa wilaya ya korogwe Mh Mrisho Gambo na mbunge wa korogwe vijijini  Prof Majimarefu  wameezeka maabara  moja na kumimina zege la lenta katika maabara ya pili kwa ushirikiano mkubwa na wananchi wa korogwe
awali kulikuwapo na taarifa kuwa Halima mdee angekuwa na mkutano mombo lakini baadae uliahirishwa baada ya kusikiwa kuwa sixtus angeenda kuezeka maabara pia mombo,wapashaji wanasema mdee alistuliwa kuwa kwa mazingira ya mombo sasa watu wangeenda kwenye tukio la kujenga maabara zaidi kuliko kuja kwenye mkutano wa hadhara hivyo wakamsihi asogeze mbele mkutano wake jambo ambalo alilifanya.
sixtus mapunda amekabidhi mabati 450 kwa wilaya ya korogwe vijijini.na baadhi ya vitendea kazi vingine vingi
huu ni muendelezo wa ziara za  katibu mkuu wa uvccm mara baada ya kumalizika kwa baraza kuu la vijana  Nov 9 ambapo alishakagua ofisi ya uvccm mkoa wa Arusha na Kilimanjaro na sasa yupo Tanga

akizungumza katika mkutano wa hadhara ktk kata ya Hale korogwe , sixtus alisema;
“…VIJANA WENZANGU NA WASIHI SANA KUENDELEA KUILINDA AMANI YETU NA KUSHIRIKIANA NA VIONGOZI WETU KATIKA KUJILETEA MAENDELEO
MNAJUA KUNAWATU WALE KAZI YAO NI MANENO TU,CCM KAZI YAKE  NI KUTENDA,NAWAOMBA PIA MJITAHIDI KUISOMA KATIBA MPYA NA KUIPIGIA KURA YA ‘NDIO’ HAPO  APRIL30  KWAKUWA NI KATIBA YENYE MAMBO MAZURI KWA WATANZANIA,NI KATIBA INAYOLINDA ARDHI YETU,MALIASILI ZETU,IMETUPA BARAZA LETU VIJANA,IMETOA HAKI KWA WANAWAKE NA MAMBO MENGINE MENGI,NI MUHIMU KUACHA KUSIKILIZA RADIO MBAO,TUISOME WENYEWE
NAWAOMBA TUENDELEE NA MOYO WA KUCHANGIA MAENDELEO YETU KAMA AMBAVYO MNASHIRIKIANA NA MBUNGE WENU NA MKUU WA WILAYA YENU,JUU YA KUPATIWA BIMA YA AFYA NA KUJENGA MAABARA,SISI TUPO NA TUTAENDELEA KUSAIDIANA KWA HALI NA MALI..”

Share:
UVCCM TANZANIA. Inaendeshwa na Blogger.

Gadget

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

Mdau Janza fomu hii

Jina

Barua pepe *

Ujumbe *

Followers

Google+ Followers

WANAOPERUZI KWA SIKU

VideoBar

Maudhui haya bado hayapatikani kupitia miunganisho iliyosimbwa kwa njia fiche.

YALIYOMO

Follow us by Email

FAHADI SIRAJI

FAHADI SIRAJI
Mtengenezaji na Msimamizi Mkuu wa Blog hii

WAJUMBE WA BARAZA KUU UVCCM TAIFA

IKO KATIKA MAREKEBISHO

My Blog List

Translate/chagua lugha

MAKATIBU WAKUU WA ZAMANI UVCCM

Kumbukumbu la Blogu