Unordered List


Je ulijua kama Kondo la Nyuma au 'Placenta' huliwa?




Hugeuka kuwa uchafu pindi mamaanapojifungua , sasa kwa nini baadhi ya wanawake wanaamua kula Kondo la nyuma au Placenta ikiwa mbichi ?
Kondo la Nyuma huwa ni sehemu ya mwili wa mama anapokuwa mjamzito, sehemu hiyo humsaidia mtoto kupata chakula na hewa kutoka kwa mama akiwa tumboni.
Pindi mama anapojifungua kazi ya Kondo la Nyuma huisha papo hapo na hivyo hutupwa , lakini sio kila mtu ana mtazamo huu.
Baadhi ya wanawake wanaamini kuwa madini yanayopitia kwa mkondo wa Nyuma hadi kwa mtoto ili kumuwezesha mtoto kukuwa huwa bado yanaweza kutumika na kwamba sio vizuri kuitupa.
Njia za kula Kondo la Nyuma
Husagwa na kuwa majimaji kama Sharbati vileInaweza kukaushwa na kutengezwa kama tembeKupikwa kwa kukaangwa kama vile nyama
Wanasema kuwa mama bado anaweza kupata madini muhimu wakati anapoendelea kupata nafuu baada ya kujifungua na pia anapoanza kuonyonyesha kwa kula Kondo la nyuma.BBC (V.S)

Chapisha Maoni

0 Maoni